Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

Kwani angekaakimya nani angemjibu. Alafu kwanini kuandika Uzi mreeeeefu, na ma reference lukuki yanini.

Vitabu vya dini vinasema majibuyenu yawe ndio, ndio, na sio,sio.
Hakuna haja ya kuandika maelezo meeeeengi,hayata saidia.
Nibora kukaa kimya alafu ukweli nauongo vitajickekecha vyenyewe kadiri muda unavyo kwenda.
Watanzania mna vichwa vibovu Sana , Una ushahidi gan anahusika....?? Ifikie hatua kila mmoja apambane na Hali yake na sio kujibanza kwa mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pasco katika utetezi wako huu ndio umeharibu. Mmoja wa watu walio sema kwa nguvu kuwa makala zako hazikuwa za kumharibia Kabendera ni mie, lakini wote tulijua kuwa kesi alizofunguliwa ni za kutunga hazina uhusiano na yeye maana watesi wake wamesimamia msimamo kuwa Kabendera amekuwa akiichafua nchi nje.

Kwa makala yako nikama unataka tuamini kuwa kilichomtesa sio kazi yake bali ni utakatishaji fedha ndio maana amelipa 100M na atalipa mamilioni mengine for six month.

Pasco, Kabendera kalipa 100M? Au ni mchezo unachezwa kuipa serikali advantage kuwa mashtaka yetu yalikuwa sahihi?

Wewe ni Investigative Journalist, hebu ingia chimbo utuambie hela hizo zilizolipwa kwa DPP zilikuwa zimehifadhiwa bank gani? Na zimepokelewa na kuingizwa account gani ya serikali? Fuatilia kwa wakili wake akupe risiti ( ERV) ya mapokezi ya fedha hizo. TUANZIE HAPO.

Hili shinikizo la wafadhili lingekwepeshwaje kama sio kutumia hadaa? Na Kabendera bado alikuwa anauhitaji Uhuru wake hivyo sio ajabu kukubali maelekezo ya mchezo ili akakae na mkewe!

Anyway, naweza kuwa wrong kiasi Fulani. Lakini kuachiwa kwake sio sababu ya kufuta tuhuma zako dhidi yake bali tuhuma zako juu ya yaliyompata Kabendera zilisha futika siku nyingi kwa ukweli uliouweka hadharani kwa kauli zako. Achana na vibaka waliokuwa wanaendelea kukushikia bango kwa ushabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania ndiyo tulivyo hua tunatuhumu tu kwa hearsay nakufanya ndo ukweli halisia. Ukishawafahamu watanzania hupati shida hata ya kuwaza kusamehe.
 
Kwa nini unamuita kaka, kwani mnauhusiano?
Tazama kichwamaji hiki kinachoamini kumuita mtu kaka au dada ni hadi uwe na uhusiano naye. Kwa taarifa yako, Pascal Mayalla namfahamu tangu nilipokuwa Sekondari na kiongozi wa TYCS akiwa anatoa mada pale Don Bosco. Ni kaka yangu kwakuwa simpati kiumri na nalifahamu hilo. Jitahidi kula samaki na dagaa kuchangamsha akili zako.
 
Mimi ni mmoja wa watu ambao nilikunyoshea kidole na kuandika makala zaidi ya moja. Paskali karma inakutesa tu...kumbuka kua usifanye mambo ya kujua mbele ya wengi wasiojua. Andika vyovyote vile bado deni utalipa tu....Kesho kutwa tunaenda kuhani matanga ( okwabya olufu) pale Katoma - Gera ila kaa ukijua nawe ni mzazi na binadamu tu
 
Pascal Mayalla, dah! okey poa nashukuru kwa msamaha wako kwani nami ni mmojawapo niliyekutwanga bonge la lawama kuhusiana na kabendera, ila naona kama ni mapema mno kwa wewe kujitoa hasa pale ulipojinasibu ulikuwa unamfahamu jamaa vizuri na ni rafiki yako, wengine bongo zetu zinachanganyaga mambo P.
 
Pascal ,,,kabendera kukiri makosa haina maana kuwa amekosa...amefanya hivyo ili asizidi kuumia maana serikali iliyopo ilikua inamkomoa na ndo maana kulikua na makubaliano.Nakuhakikishia ipo siku huu ukweli utajulikana na mtakua uchi.Huwezi kukaa mbali na uchafu huu.

Naisikitikia nchi yangu kwa sasa watu wananunua haki zao kwa mamilioni ya shilingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka Pascal Mayalla wakati mwingine kukaa kimya huepusha na kuponya. Ingekuwa vyema kama ungebaki kimya. Sasa kwenye suala lile kuna ukweli gani uliothibitika? Wewe umetajwa wapi katika kusafishwa? Pole na chukua mkondo wa kubaki kimya.
Huaga napenda tu kumuona Pascal kama my real brother na usingeandika hapa nadhani nami ningeandika kitu kinacho fafana na ulicho kiandika na kwa kua wewe uliyeandika hapa ni mwana sharia kama Pascal, hope atayachukulia maandishi/ushauri wako kwa uzito unao stahiri, Mungu amfungue macho kaka Pascal
 
Zaidi ya kuendelea kumhujumu Kabendera ndani ya uzi wako huu hakuna jipya , ni upi ukweli uliodhihirika ? mbona Kabendera hajalipa chochote na kaachiwa kwa msaada wa Wazungu !
 
Mayala tuliambiwa umezaliwa wakati wa njaa pengine hiyo ndo inakufanya uwe mnafiki.. Unarukaruka kama mahindi ya binsi kikaangoni embu tuambie huo ukweli uliodhihirika ni upi Alafu ngoja tukukumbushe kitu uzalendo sio kutetea serikali uzalendo ni kuitetea nchi kwa maslahi ya Mustakabali wa nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu huo mkataba wa kukiri umekaa kikandamizaji sana:
  1. Ukishakiri kosa unapoteza haki ya kukata rufaa, isipokuwa tu kama rufaa hiyo ni dhidi ya adhabu
  2. Mkurugenzi wa Mashitaka bado ana haki ya kukata rufaa
  3. Kwa kukiri makosa unafutiwa pia mashitaka mengine yaliyoshitakiwa pamoja na hayo uliyokiri, lakini ukikiuka makubaliano makosa hayo yote yatafufuliwa (yaani hii iko kimafia kabisa, mfano kama Eric alivyokiri kosa la kutakatisha fedha amefutiwa pia shitaka la kuratibu kundi la kihalifu, lakini akikiuka makubaliano shitaka hili litafufuliwa, maana yake msoto wa jela na kauli za 'upelelezi haujakamilika' zitaendelea indefinitely)
Hii ni sheria ya ajabu sana.
 
Pascal Mayalla Kabendera amekiri makosa ya ML & tax evation. Wanaojaribu ku -spin hii story eti amelazimika kununua uhuru wake wanamchafulia jina kwa kumfanya mpiga dili za kukiuka mujibu wa sheria. Hamumsaidii kwa Hoja hizo za kitoto, bora mumuwache ajenge reputation yake afresh.Maana sasa huyu sio mshukiwa ni convict wa Kuhujumu Uchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…