Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

Paskali safari hii hadi uathirike kisaikolojia - kama unaogopa hukumu za kidunia. Unaandika kwa nakshi kupita kiasi. Sisi Watanzania si wasomaji wazuri sana; unajua hilo. Sasa hizo mbwembwe zako na kuturundikia mabandiko yanayopandiana ili eti tufanye rejea ya masuala, zimeishia kukutwisha zigo la u-“snitch”.

Halafu ndio unaharibu zaidi kwa kutaka kujitakasa kwa mtindo uleule - au ni janja ya kuibua upya mjadala wa Kabendera kwa ‘namna’ ingine? Tuseme una wasiwasi kuwa wako wengi watakaoamini kuwa hii ishakuwa “case closed” baada ya “Roma locuta”? Sisi waelewa hatuna shida na wewe. I have no doubt of your innocence. Sijui unalenga kujisafisha kwa nani hasa?
 
Na sisi hilo tumeona halina uhalisia,tunaamini kabambikiziwa kesi na ni shinikizo la Mabeberu limempa uhuru mapema!
 
In this day and age ya information overload.., summarization ni muhimu sana.., bandiko lako lingeweza kujibu haya kwa sentensi tatu au mbili tu

a) Ulishutumiwa kwa yapi
b) Umesafishwa kwa lipi
c) Ukweli upi umejulikana
 
Eric Kabendera na Pascal Mayalla wakiwa jukwaa moja kujadili mustakabali wa uhuru wa habari na wa kujieleza bila kujikita kuchafuana ktk majukwaa ya Habari na Mawasiliano.


Source: JamiiForums
 
Lakini Mzee Pasko, Erick anaonekana kabisa hakuwa na jinsi. Na yote hao turejee tu kwenye ukamatwaji wake. Kama kawaida humo ndani ujumbe "haswa" uliotaka utufikie umeshatufikia.
 
Wewe ni mtu mzima, sio kijana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umemsamehe nani sasa? na Kwa kosa lipi? yanayofanyika gizazi kuna siku yatamulikwa na watu watajionea
 
Hivi Rais akihujumu uchumi anapelekwa mahakama ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…