Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kwa wataalam wa masuala ya Ulinzi na Usalama aibu waliyoipata SADC baada ya Mission yao kufeli nchini Congo DRC, sio jambo lililotokea kwa bahati mbaya.
Baada ya kuingia siasa za ushindani kusini mwa Bara la Afrika, Vyama vinavyofahamika kama vyama vya ukombozi ambavyo vingi vinatawala nchi za Kusini mwa Bara hili, kwa uchu tu wa madaraka, viliamua kuingiza siasa kwenye majeshi yao na vyombo vya dola ili viendelee kubaki madarakani.
Vyama hivyo, CCM( hapo awali TANU) ANC, ZANU PF, FRELIMO, SWAPO na BDP kutokana na hofu ya kuwa vyama pinzani badala ya kuwekeza katika kuzijenga nchi zao kimaarifa na hatimaye kuwa imara katika Dunia hii inayozidi kuwa na ushindani kila siku viliamua tu kwa makusudi kuingiza siasa kwenye mifumo yake ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuvilinda na hatimaye kuvifanya vyombo vyao vya Ulinzi na Usalama kuwa vya kisiasa badala ya kutimiza majukumu yake ya Ulinzi na Usalama.
Ushahidi wa siasa kuingia kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mataifa haya ni namna vyombo vya ulinzi na usalama katika mataifa hayo vilivyokuwa vinatumika katika kulinda rushwa na tawala mbovu katika nchi hizo ( Mfano Tanzania, Zimbabwe na Msumbiji)
Kuingia kwa siasa kwenye majeshi na taasisi za intelejensia za nchi hizo sio tu kumefanya kukua kwa rushwa katika nchi hizo bali pia kuanguka kwa mifumo thabiti ya ulinzi na usalama iliyokuwepo hapo awali katika block hii ya SADC
Pia kuingia kwa siasa katika nchi taasisi za majeshi na intelejensia za vyombo hivi kumesababisha ombwe kubwa la uongozi hasa kutokana na nchi hizi kushindwa kujilinda dhidi ya maadui wa ndani na nje.
Mfano wa kwanza wa kufeli kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hizi ni matukio ya kigaidi yaliyoikumba nchi ya Msumbiji. SADC kama block kongwe katika Afrika ilishindwa kabisa kuisadia msumbiji kijeshi kupambana na Magaidi hadi pale Rwanda alipojitokeza kupeleka vikosi vyake Kaskazini mwa Msumbiji ambavyo vimesifika kwa kufanikiwa kurudisha hali ya utulivu.
Mfano wa pili kwa kufeli kwa nchi hizi kutokana na kuingiza siasa katika majeshi yao na taasisi zao za intelejensia ni namna Walivyoshindwa kusoma vizuri hali ya usalama ya Mashariki mwa Congo hadi vikosi vyao vilivyoenda kwa mbwembwe kufeli mission yao ya kuondoa vikosi vya uvamizi mashariki mwa Congo.
Kwa bahati nzuri sana, anayewafundisha nchi hizi namna ya kutumia Taasisi za Majeshi na Intelejensia kwa weredi na sio kisiasa ni Paul Kagame ambaye anazijua vizuri sana hizi nchi za SADC kihistoria na mwenendo wake wa sasa kwa sababu kwa miaka mingi alizitumia kufundisha majeshi yake.
Kagame akiwa Rais wa nchi ndogo sana iliyo na very limited resources amevifundisha vyama vya ukombozi vya nchi za SADC kuwa majeshi yanatakiwa kujikita kwenye masuala yake ya kijeshi na sio siasa kwa faida ya nchi kiuchumi. Na anafanya hivi kwa kutumia jeshi lake kuipaisha Rwanda kiuchumi.
Kagame anavifundisha vyama vya ukombozi kuwa intelejensia inatakiwa kutumika kwa maslahi mapana ya kijeshi na kiuchumi kwa faida ya nchi na sio kukandamiza tu upinzani na kuiba chaguzi tu.
Hongera Kagame. Sasa Waafrika watajifunza kwako.