Baada ya Vyama vya Ukombozi kuziharibu nchi zao kwa kuingiza siasa kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Kagame avifundisha nini maana ya Uongozi!

Mbona kagame mwenyewe amekuwa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi? Amekuwa akishutumiwa kuwapoteza wapinzani wake hata wenye jinsia ya ke , analaumiwa kwa kukandamiza demokrasia kama ilivyo kwa Yoweli Kaguta Museveni, Robert Mugabe na waliofanyiwa mapinduzi ya kijeshi Somalia, Mali, Ghana na Niger
Tofauti yao na sisi, wao wanafanya kwa maslahi mapana ya kwao kiuchumi wakiangalia mbele zaidi kitaifa zaidi.

Sisi tunafanya kwa maslahi ya CCM ili waendelee kula keki ya taifa.
 
Kwa wataalam wa masuala ya Ulinzi na Usalama aibu waliyoipata SADC baada ya Mission yao kufeli nchini Congo DRC, sio jambo lililotokea kwa bahati mbaya.

Baada ya kuingia siasa za ushindani kusini mwa Bara la Afrika, Vyama vinavyofahamika kama vyama vya ukombozi ambavyo vingi vinatawala nchi za Kusini mwa Bara hili, kwa uchu tu wa madaraka, viliamua kuingiza siasa kwenye majeshi yao na vyombo vya dola ili viendelee kubaki madarakani.

Vyama hivyo, CCM( hapo awali TANU) ANC, ZANU PF, FRELIMO, SWAPO na BDP kutokana na hofu ya kuwa vyama pinzani badala ya kuwekeza katika kuzijenga nchi zao kimaarifa na hatimaye kuwa imara katika Dunia hii inayozidi kuwa na ushindani kila siku viliamua tu kwa makusudi kuingiza siasa kwenye mifumo yake ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuvilinda na hatimaye kuvifanya vyombo vyao vya Ulinzi na Usalama kuwa vya kisiasa badala ya kutimiza majukumu yake ya Ulinzi na Usalama.

Ushahidi wa siasa kuingia kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mataifa haya ni namna vyombo vya ulinzi na usalama katika mataifa hayo vilivyokuwa vinatumika katika kulinda rushwa na tawala mbovu katika nchi hizo ( Mfano Tanzania, Zimbabwe na Msumbiji)

Kuingia kwa siasa kwenye majeshi na taasisi za intelejensia za nchi hizo sio tu kumefanya kukua kwa rushwa katika nchi hizo bali pia kuanguka kwa mifumo thabiti ya ulinzi na usalama iliyokuwepo hapo awali katika block hii ya SADC

Pia kuingia kwa siasa katika nchi taasisi za majeshi na intelejensia za vyombo hivi kumesababisha ombwe kubwa la uongozi hasa kutokana na nchi hizi kushindwa kujilinda dhidi ya maadui wa ndani na nje.

Mfano wa kwanza wa kufeli kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hizi ni matukio ya kigaidi yaliyoikumba nchi ya Msumbiji. SADC kama block kongwe katika Afrika ilishindwa kabisa kuisadia msumbiji kijeshi kupambana na Magaidi hadi pale Rwanda alipojitokeza kupeleka vikosi vyake Kaskazini mwa Msumbiji ambavyo vimesifika kwa kufanikiwa kurudisha hali ya utulivu.

Mfano wa pili kwa kufeli kwa nchi hizi kutokana na kuingiza siasa katika majeshi yao na taasisi zao za intelejensia ni namna Walivyoshindwa kusoma vizuri hali ya usalama ya Mashariki mwa Congo hadi vikosi vyao vilivyoenda kwa mbwembwe kufeli mission yao ya kuondoa vikosi vya uvamizi mashariki mwa Congo.

Kwa bahati nzuri sana, anayewafundisha nchi hizi namna ya kutumia Taasisi za Majeshi na Intelejensia kwa weredi na sio kisiasa ni Paul Kagame ambaye anazijua vizuri sana hizi nchi za SADC kihistoria na mwenendo wake wa sasa kwa sababu kwa miaka mingi alizitumia kufundisha majeshi yake.

Kagame akiwa Rais wa nchi ndogo sana iliyo na very limited resources amevifundisha vyama vya ukombozi vya nchi za SADC kuwa majeshi yanatakiwa kujikita kwenye masuala yake ya kijeshi na sio siasa kwa faida ya nchi kiuchumi. Na anafanya hivi kwa kutumia jeshi lake kuipaisha Rwanda kiuchumi.

Kagame anavifundisha vyama vya ukombozi kuwa intelejensia inatakiwa kutumika kwa maslahi mapana ya kijeshi na kiuchumi kwa faida ya nchi na sio kukandamiza tu upinzani na kuiba chaguzi tu.

Hongera Kagame. Sasa Waafrika watajifunza kwako.
Naunga mikono hoja.
 
Huyo Mti mkavu wamemkauishia tu kwa sababu ya sheria za kiusalama ktk ulimwengu wa smartphone,ila angezabuliwa chini kwa chini kama 2014 na kuanza kulia lia.Maneno yalikua hayahaya 2014 kabla ya kuzibuliwa kidogo na kusambaratika
Sio wamemkaushia. Kajipanga kweli na anajua anafanya nini?

Nyie mkiwekeza kwenye uchawa yeye kila siku anasoma weakness zenu na kuwajua inside out.

Kama wanajeshi wetu na hakuna chochote tunamfanya.
 
Taifa lolote likisha fanya rushwa kuwa sehemu ya taifa hilo ni wazi kwamba taifa hilo ni mfu.
Pk anamatatizo yake lakini linapo kuja suala la kuongoza nchi na maslahi ya nchi hacheki na mtu.
Kweli kabisa. Na amezijenga fikra za wananchi wa nchi yake vizuri sana huku sie tukijenga uchawa na kujipendekeza kwa watawala kulamba miguu yao.
 
Kwa wataalam wa masuala ya Ulinzi na Usalama aibu waliyoipata SADC baada ya Mission yao kufeli nchini Congo DRC, sio jambo lililotokea kwa bahati mbaya.

Baada ya kuingia siasa za ushindani kusini mwa Bara la Afrika, Vyama vinavyofahamika kama vyama vya ukombozi ambavyo vingi vinatawala nchi za Kusini mwa Bara hili, kwa uchu tu wa madaraka, viliamua kuingiza siasa kwenye majeshi yao na vyombo vya dola ili viendelee kubaki madarakani.

Vyama hivyo, CCM( hapo awali TANU) ANC, ZANU PF, FRELIMO, SWAPO na BDP kutokana na hofu ya kuwa vyama pinzani badala ya kuwekeza katika kuzijenga nchi zao kimaarifa na hatimaye kuwa imara katika Dunia hii inayozidi kuwa na ushindani kila siku viliamua tu kwa makusudi kuingiza siasa kwenye mifumo yake ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuvilinda na hatimaye kuvifanya vyombo vyao vya Ulinzi na Usalama kuwa vya kisiasa badala ya kutimiza majukumu yake ya Ulinzi na Usalama.

Ushahidi wa siasa kuingia kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mataifa haya ni namna vyombo vya ulinzi na usalama katika mataifa hayo vilivyokuwa vinatumika katika kulinda rushwa na tawala mbovu katika nchi hizo ( Mfano Tanzania, Zimbabwe na Msumbiji)

Kuingia kwa siasa kwenye majeshi na taasisi za intelejensia za nchi hizo sio tu kumefanya kukua kwa rushwa katika nchi hizo bali pia kuanguka kwa mifumo thabiti ya ulinzi na usalama iliyokuwepo hapo awali katika block hii ya SADC

Pia kuingia kwa siasa katika nchi taasisi za majeshi na intelejensia za vyombo hivi kumesababisha ombwe kubwa la uongozi hasa kutokana na nchi hizi kushindwa kujilinda dhidi ya maadui wa ndani na nje.

Mfano wa kwanza wa kufeli kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hizi ni matukio ya kigaidi yaliyoikumba nchi ya Msumbiji. SADC kama block kongwe katika Afrika ilishindwa kabisa kuisadia msumbiji kijeshi kupambana na Magaidi hadi pale Rwanda alipojitokeza kupeleka vikosi vyake Kaskazini mwa Msumbiji ambavyo vimesifika kwa kufanikiwa kurudisha hali ya utulivu.

Mfano wa pili kwa kufeli kwa nchi hizi kutokana na kuingiza siasa katika majeshi yao na taasisi zao za intelejensia ni namna Walivyoshindwa kusoma vizuri hali ya usalama ya Mashariki mwa Congo hadi vikosi vyao vilivyoenda kwa mbwembwe kufeli mission yao ya kuondoa vikosi vya uvamizi mashariki mwa Congo.

Kwa bahati nzuri sana, anayewafundisha nchi hizi namna ya kutumia Taasisi za Majeshi na Intelejensia kwa weredi na sio kisiasa ni Paul Kagame ambaye anazijua vizuri sana hizi nchi za SADC kihistoria na mwenendo wake wa sasa kwa sababu kwa miaka mingi alizitumia kufundisha majeshi yake.

Kagame akiwa Rais wa nchi ndogo sana iliyo na very limited resources amevifundisha vyama vya ukombozi vya nchi za SADC kuwa majeshi yanatakiwa kujikita kwenye masuala yake ya kijeshi na sio siasa kwa faida ya nchi kiuchumi. Na anafanya hivi kwa kutumia jeshi lake kuipaisha Rwanda kiuchumi.

Kagame anavifundisha vyama vya ukombozi kuwa intelejensia inatakiwa kutumika kwa maslahi mapana ya kijeshi na kiuchumi kwa faida ya nchi na sio kukandamiza tu upinzani na kuiba chaguzi tu.

Hongera Kagame. Sasa Waafrika watajifunza kwako.
Kagame ni mpumbavu kama wapumbavu wengine atakufa mdomo wazi asema Bwana, mda mwalimu.

Kajitu kamekomaaa kimwili kama cadava, katakufa vibaya mpaka nakahurumia ,ajitafakari miaka 20 iliyo pita alikuwa vile alivyo, so ajue futi saba zamhusu apende au asipede ,jinga sana hili jamaa
 
Hata akifa leo. Ametengeneza Taifa imara sana linalowekeza kwenye maarifa ili waweze ku survive.

Atakufa yeye ila ideas zake hazitalufa. Nyie mnaowekeza kwenye uchawa, kujipendekeza kwa watawala, wizi na ufisadi ndo inabidi muwe na hofu juu ya future yenu maana kwa kifupi Tanzania saivi sie ni maiti inayotembea. CCM walishalimaliza hili taifa na mifumo yake ambayo ndo at least tulikuwa tunaitegemea.
 
Kwa wataalam wa masuala ya Ulinzi na Usalama aibu waliyoipata SADC baada ya Mission yao kufeli nchini Congo DRC, sio jambo lililotokea kwa bahati mbaya.

Baada ya kuingia siasa za ushindani kusini mwa Bara la Afrika, Vyama vinavyofahamika kama vyama vya ukombozi ambavyo vingi vinatawala nchi za Kusini mwa Bara hili, kwa uchu tu wa madaraka, viliamua kuingiza siasa kwenye majeshi yao na vyombo vya dola ili viendelee kubaki madarakani.

Vyama hivyo, CCM( hapo awali TANU) ANC, ZANU PF, FRELIMO, SWAPO na BDP kutokana na hofu ya kuwa vyama pinzani badala ya kuwekeza katika kuzijenga nchi zao kimaarifa na hatimaye kuwa imara katika Dunia hii inayozidi kuwa na ushindani kila siku viliamua tu kwa makusudi kuingiza siasa kwenye mifumo yake ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuvilinda na hatimaye kuvifanya vyombo vyao vya Ulinzi na Usalama kuwa vya kisiasa badala ya kutimiza majukumu yake ya Ulinzi na Usalama.

Ushahidi wa siasa kuingia kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mataifa haya ni namna vyombo vya ulinzi na usalama katika mataifa hayo vilivyokuwa vinatumika katika kulinda rushwa na tawala mbovu katika nchi hizo ( Mfano Tanzania, Zimbabwe na Msumbiji)

Kuingia kwa siasa kwenye majeshi na taasisi za intelejensia za nchi hizo sio tu kumefanya kukua kwa rushwa katika nchi hizo bali pia kuanguka kwa mifumo thabiti ya ulinzi na usalama iliyokuwepo hapo awali katika block hii ya SADC

Pia kuingia kwa siasa katika nchi taasisi za majeshi na intelejensia za vyombo hivi kumesababisha ombwe kubwa la uongozi hasa kutokana na nchi hizi kushindwa kujilinda dhidi ya maadui wa ndani na nje.

Mfano wa kwanza wa kufeli kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hizi ni matukio ya kigaidi yaliyoikumba nchi ya Msumbiji. SADC kama block kongwe katika Afrika ilishindwa kabisa kuisadia msumbiji kijeshi kupambana na Magaidi hadi pale Rwanda alipojitokeza kupeleka vikosi vyake Kaskazini mwa Msumbiji ambavyo vimesifika kwa kufanikiwa kurudisha hali ya utulivu.

Mfano wa pili kwa kufeli kwa nchi hizi kutokana na kuingiza siasa katika majeshi yao na taasisi zao za intelejensia ni namna Walivyoshindwa kusoma vizuri hali ya usalama ya Mashariki mwa Congo hadi vikosi vyao vilivyoenda kwa mbwembwe kufeli mission yao ya kuondoa vikosi vya uvamizi mashariki mwa Congo.

Kwa bahati nzuri sana, anayewafundisha nchi hizi namna ya kutumia Taasisi za Majeshi na Intelejensia kwa weredi na sio kisiasa ni Paul Kagame ambaye anazijua vizuri sana hizi nchi za SADC kihistoria na mwenendo wake wa sasa kwa sababu kwa miaka mingi alizitumia kufundisha majeshi yake.

Kagame akiwa Rais wa nchi ndogo sana iliyo na very limited resources amevifundisha vyama vya ukombozi vya nchi za SADC kuwa majeshi yanatakiwa kujikita kwenye masuala yake ya kijeshi na sio siasa kwa faida ya nchi kiuchumi. Na anafanya hivi kwa kutumia jeshi lake kuipaisha Rwanda kiuchumi.

Kagame anavifundisha vyama vya ukombozi kuwa intelejensia inatakiwa kutumika kwa maslahi mapana ya kijeshi na kiuchumi kwa faida ya nchi na sio kukandamiza tu upinzani na kuiba chaguzi tu.

Hongera Kagame. Sasa Waafrika watajifunza kwako.
Atoke madarakani karne hii wanakuwa na Rais wa milele africa kuna vituko sana
 
Tufauti yake na wengine yeye anabaki madarakani na anatumia mbinu zote kulifanya Taifa lake kuwa Taifa kuwa kiuchumi na sasa kijeshi. Sie wetu wanabaki madarakani kwa faida zao binafsi na familia zao.
 
Nilivyoona JWZT wanafanyishwa usafi na Makonda kisa wapinzani wametangaza maandamano nikaona sasa hamna tena Jeshi
 
Mkuu naona unasifia kichaka.
Kagame mtoto wetu, tumemfundisha hapa, na hawezi kuwa zaidi ya anachotujua.
Jinsi ulivyo mtoto, hujui kwamba Afrika yote Kusini mwa Afrika ilikombolewa wakati wa chama kimoja.
Na nduli Iddi Amin alitandikwa wakati wa chama kimoja.
Mbinu za kijeshi na mapambano huzijui kwa sababu za utoto wako.
Kagame kaua askari wetu wawili Kongo, katika mission ya kweka amani nchi ya kiafrika.
Hatusahau hilo.
Payback time must come, watch this space.
Mmebakiza maneno mengi ya tulimpiga amini unaishi kwa istoria
 
Taifa lolote likisha fanya rushwa kuwa sehemu ya taifa hilo ni wazi kwamba taifa hilo ni mfu.
Pk anamatatizo yake lakini linapo kuja suala la kuongoza nchi na maslahi ya nchi hacheki na mtu.
Nakubaliana na wewe 90% kwa uzalendo wa nchi tu, jamaa ni mfano wa kuigwa
 
Historia inajieleza kwamba vizazi vilivyopita viliweza.
Ninyi vibwengo vya sasa mkisikia mlio tu wa risasi mnjikojolea
Tanzania, Mozambique, Afrika Kusini na Zimbabwe hizi nchi zilishajifia. Saivi zinasubiri maziko tu
 
Hapa hakuna ukweli wowote!

Labda una agenda yako ya kisiasa ama wewe sio mpembuzi yakinifu wa mambo katika eneo hili.

Mzozo wa Congo DR haukuanza leo, ni mzozo wa tangu nchi hiyo ipate uhuru wake enzi za hayati Patrice Lumumba'

Pili kama umesema nchi za SADCC zimefeli kwasababu eti zimeingiza siasa kwenye majeshi yao, hiyo ni hoja mfu na dhaifu sana! Kwanza hebu jiulize na vikosi vya umoja wa mataifa Munusco vyenye zaidi ya wanajeshi 17,000 vikiwa ndio vingi kuliko sehemu yoyote ile duniani, navyo vimeshindwa kurejesha amani kwasababu nao pia wameingiza siasa kwenye vikosi vyao???

Tatu jiulize vile vikosi vya Afrika Mashariki vilivyopelekwa mashariki ya Congo DR kutoka Kenya, Uganda, Sudani Kusini na kushindwa kurejesha amani kisha vikafukuzwa/ vikatimuliwa na kurudi kwao navyo pia vilishindwa kwasababu viliingiza siasa kwenye majeshi yao???

Mzozo wa Congo una mambo mengi mno, hata huyo Paul Kagame mwenyewe ana supportiwa na Marekani, Israel na Ulaya magharibi ndio maana wanamlea hakamatwi
 
Kwanza hapa unajadiliwa mzozo wa Congo au kufeli kwa SADC?

Hujui Kenya nae aliingia kwa maslahi binafsi Congo kama walivyo Uganda na Rwanda hadi akafurushwa?

Alafu tofautisha kufukuzwa walikofukuzwa vikosi vya EAC na mission kufeli hadi kuondoa vikosi kwa aibu walivyofanya SADC.

Hayo maneno ya Marekani mnaongea kwa sababu Kagame kawazidi maarifa na mbinu za kivita. Marekani ndo kamwekea vikwazo sasa kwa nini kawashinda na vikosi vyenu hadi mnaondoka kwa aibu?
 
Inafikirisha sana kuona kazi wanayotakiwa kufanya mgambo wajiji ndio wanapewa JWTZ sawa na kuuwa nzi kwa rungu
 
Back
Top Bottom