Baada ya walimu walio kuwa wamejificha kwenye Ofisi za Elimu Msingi, Sekondari na TSD ndani ya Halmashauri kutimuliwa sasa Idadi ya walimu Waongezeka

Baada ya walimu walio kuwa wamejificha kwenye Ofisi za Elimu Msingi, Sekondari na TSD ndani ya Halmashauri kutimuliwa sasa Idadi ya walimu Waongezeka

Nianze kwa kumpongeza Prof Adolf Mkenda kwa kazi nzuri aliyoifanya Baada ya walimu walio kuwa wamejificha kwenye Ofisi za Elimu msingi, sekondari na TSD ndani ya Halmashauri kutimuliwa sasa Idadi ya walimu wa kufundisha madarasa ni Waongezeka.

Hii ni baada ya malalamiko mengi kuandika Jf sasa Hali imetulia na walimu wa kufundisha darasani msingi na sekondari wameongezeka na Hata serikali ikiajiri itaajiri walimu wachache.

Kazi iliyobakia ni kupunguza Idadi ya maafisaelimu waliopo imara ya Elimu msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na kufunganisha hizo idara na kuunda idara moja ya Elimu ndani ya Halmashauri moja.

Prof Mkenda kasi unayokwenda nayo inaridhisha na Uko vizuri.

Pili muundo mpya wa Elimu mkuu wa idara aside na kiwango cha chini ya PhD Ili aweze kusimamia Elimu ipasavyo.

Kuna walimu walikuwa wamefichwa kwa afisaelimu Mkoa ambao walikuwa hawana barua Za uteuzi nao warudishwe madarasani haraka iwezekanavyo.
Kazi zinawazidi hao maafisa ndiyo maana wanaomba wasaidizi kutoka mashuleni, hao walimu hata Kama watarudishwa mashuleni bado watakuwa wanaitwa kila wakati kusaidia
 
Masters elimu hawaitambui, Sasa wanataka na PhD awe mkuu wa idara.

Kwenye sekta nyingine hao PhD wamedeliva nn Cha maana?
Masters na PhD kwenye utawala hawana tija yoyote.
Bachelor iwe kiwango kinachotambulika kama elimu kwa viongozi,
Sifa zingine za uzoefu na historia ya utendaji kazi uliotukuka ndio viwe vigezo vya uongozi katika elimu
 
Kimsingi hizi PhD za hawa viongozi ni za magumashi. Jaribu kutafuta machapisho yao km utayaona.

Ni magumashi kwasababu hivi mwalimu was udsm au udom anawezaje kumsupervise waziri ipasavyo na ahakikishe anapata PhD ya haki. Anawezaje kumsimamia kwa haki na kwa misingi imara ya kitaaluma km siyo kipeana hizi PhD.
Hata kama ni za kweli lakini zina msaada wowote zaidi ya title? Mh Dr Manyau nyau
 
Masters na PhD kwenye utawala hawana tija yoyote.
Bachelor iwe kiwango kinachotambulika kama elimu kwa viongozi,
Sifa zingine za uzoefu na historia ya utendaji kazi uliotukuka ndio viwe vigezo vya uongozi katika elimu
Kibongo bongo hii ni elimu ya juu sn
 
Wewe ni mwalimu na roho yako mbaya kwa wenzako walio kuwa wamebadilishiwa majukumu ndio imekusukuma kuja kuandika hapa
Kwanza hawakwenda halmashauri kwa kujipendekeza isipokuwa sifa zao anaweza kuwa NI mwalimu Ila alipojiendeleza alisoma uchumi, IT na mengine kwa upungufu ulio kuwepo halmashauri ukaona umtumie utalaamu wake kwa kumvuta halmashauri
 
Nianze kwa kumpongeza Prof Adolf Mkenda kwa kazi nzuri aliyoifanya Baada ya walimu walio kuwa wamejificha kwenye Ofisi za Elimu msingi, sekondari na TSD ndani ya Halmashauri kutimuliwa sasa Idadi ya walimu wa kufundisha madarasa ni Waongezeka.

Hii ni baada ya malalamiko mengi kuandika Jf sasa Hali imetulia na walimu wa kufundisha darasani msingi na sekondari wameongezeka na Hata serikali ikiajiri itaajiri walimu wachache.

Kazi iliyobakia ni kupunguza Idadi ya maafisaelimu waliopo imara ya Elimu msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na kufunganisha hizo idara na kuunda idara moja ya Elimu ndani ya Halmashauri moja.

Prof Mkenda kasi unayokwenda nayo inaridhisha na Uko vizuri.

Pili muundo mpya wa Elimu mkuu wa idara aside na kiwango cha chini ya PhD Ili aweze kusimamia Elimu ipasavyo.

Kuna walimu walikuwa wamefichwa kwa afisaelimu Mkoa ambao walikuwa hawana barua Za uteuzi nao warudishwe madarasani haraka iwezekanavyo.
Hii chai.
 
Eti serikali itaajiri walimu wachache. Kwamba walimu sasa wamepatikana. Ni kichekesho. Inaonekana mleta mada hujui kwa kina tatizo la upungufu wa walimu lilivyo.

Pili, Waziri Kama ana uthubutu na anataka shule ziwe na uwiano mzuri wa walimu maeneo ya vijijini basi AHAMISHE WALIMU WALIOLUNDIKANA MAENEO YA MIJINI awapeleke vijijini. Kwa hili utaona jinsi ambavyo nchi hii haina upungufu mkubwa wa walimu, Namaanisha tatizo siyo kubwa km tunavyodhani.

Mara nyingi upungufu unaoimbwa references inayotumika Ni shule za vijijini wakati mijini unakuta mwalimu ana vipindi 6 KWA wiki Kati ya vipindi 40. Baadhi ya maeneo Vijijini walimu wana vipindi hadi 60.

Waziri aangalie suala la walimu kupangwa vijijini na baada ya muda mfupi wanahama kinyemela kwenda mijini, kwa barua zinazotoka moja kwa moja TAMISEMI. TAMISEMI imekuwa sehemu ya tatizo.

Serikali iangalie kwa kina na kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza bila kusahau stahiki za walimu zilizoko kisheria.

Mimi bado naona uhitaji wa afisa elimu kuwa wawili kwasababu mtu mmoja kudili kwa mfano na shule 160 za msingi na pengine 40 za sekondari ktk halmashauri moja Ni kazi nzito tofauti na mtazamo wa watu nje ya ufahamu wa jinsi elimu inavyoendeshwa.

(Nimewahi kufundisha sekondari kwa miaka 15 saba kati ya Hiyo nikiwa Mkuu wa shule)
Wew kweli ni Mwalimu,umeandika ukweli mtupu,mijini walimu ni wengi mno,wafanyiwe msawazo
 
Back
Top Bottom