Eti serikali itaajiri walimu wachache. Kwamba walimu sasa wamepatikana. Ni kichekesho. Inaonekana mleta mada hujui kwa kina tatizo la upungufu wa walimu lilivyo.
Pili, Waziri Kama ana uthubutu na anataka shule ziwe na uwiano mzuri wa walimu maeneo ya vijijini basi AHAMISHE WALIMU WALIOLUNDIKANA MAENEO YA MIJINI awapeleke vijijini. Kwa hili utaona jinsi ambavyo nchi hii haina upungufu mkubwa wa walimu, Namaanisha tatizo siyo kubwa km tunavyodhani.
Mara nyingi upungufu unaoimbwa references inayotumika Ni shule za vijijini wakati mijini unakuta mwalimu ana vipindi 6 KWA wiki Kati ya vipindi 40. Baadhi ya maeneo Vijijini walimu wana vipindi hadi 60.
Waziri aangalie suala la walimu kupangwa vijijini na baada ya muda mfupi wanahama kinyemela kwenda mijini, kwa barua zinazotoka moja kwa moja TAMISEMI. TAMISEMI imekuwa sehemu ya tatizo.
Serikali iangalie kwa kina na kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza bila kusahau stahiki za walimu zilizoko kisheria.
Mimi bado naona uhitaji wa afisa elimu kuwa wawili kwasababu mtu mmoja kudili kwa mfano na shule 160 za msingi na pengine 40 za sekondari ktk halmashauri moja Ni kazi nzito tofauti na mtazamo wa watu nje ya ufahamu wa jinsi elimu inavyoendeshwa.
(Nimewahi kufundisha sekondari kwa miaka 15 saba kati ya Hiyo nikiwa Mkuu wa shule)