Baada ya WB na Denmark kusitisha misaada na uhusiano wanaofuata ni Scandinavia, EU, UK, Canada na Marekani

Baada ya vita vya Kagera nchi iliyumba mno kiuchumi na hakukuwa na fedha za kigeni kwa ajili ya kununulia bidhaa muhimu kama mafuta nk ndipo IMF wakaitaka Tanzania kushusha kabisa thamani ya shilingi dhidi ya dola ndio serikali iweze kukopeshwa.

Baada ya Nyerere kukataa hili sharti na kupelekea waziri wa fedha wa wakati huo Mr. Edwin Mtei kujiuzulu ndipo hali ikawa mbaya zaidi na kupelekea Nyerere kulazimika kuachia ngazi na wakati huo pia ndio akawa amenusurika kupinduliwa.

Hakuna nchi duniani inayokosana na hawa wazungu eti ikabaki salama kiuchumi, hakuna kwa sababu wao ni kama umeme na wengine ni kama Electric Appliances ambazo bila umeme hazifanyi kazi.

Ni lazima tuwe macho kwani hatuna njia mbadala japo tunaweza tukajifanya kujaribu kutunisha msuli ambayo ndio itakuwa kitanzi chetu. Uchumi ukiharibika, Tanzania ikawa "Basket Case" hata watawala wajue usalama wao utakuwa kwenye mashaka makubwa.
 
Sijakuelewa ndiyo maana nimeuliza serikali ya upinzani ndiyo ipi.
Rejea majadiliano yetu.

Kifupi upinzani unadai Serikali iliyoko madarakani inafeli. Kama ni kweli, ni kete ya kisiasa upinzani kuunda Serikali ili kuirudisha nchi kwenye mstari. Ndivyo mada kuu ilivyotaka tuelewe.

Hivyo basi nilishauri kuwa Uchaguzi Mkuu 2020 hauko mbali ili upinzani ushinde na kuunda Serikali yabidi ujipange vizuri na siyo tunavyoona kwa sasa viongozi wake wanavyoendesha siasa za matukio, kejeli na kuzodoa, pasipo hoja za kipi kifanyike nchi isiende mrama. Hata mleta mada mlengo wake ulikuwa huo huo kuhabarisha kuwa Serikali imeshindwa!!!
 
Huyo dereva alipokataa uliripoti panapohusika nao wakakataa kukuhudumia.
Mkuu unapokwenda kwenye kituo cha taxi kama ilivyo pale posta, dareva akakataa kukuhudumia kwa sababu zake, unaenda kumshitaki wapi kwanza, pili una muda huo wa kuanzisha mashtaka?. Kwa upande wangu, madereva wengine walijitokeza kunihudumia na njia nzima nilisikiliza taralila za kuomba radhi kwa yule mwenzake, fani yake na nchi yake.
 
Unaforce sana habari hii ila umepuuzwa!!!!!!
 
Sijakuelewa ndiyo maana nimeuliza serikali ya upinzani ndiyo ipi.
Kumbuka mada yako umehitimisha kwamba Tunapobeza umuhimu wao tutegemee kuzorota kwa uchumi pengine hali inaweza kuwa mbaya zaidi ya Zimbabwe, maana yake Serikali imefeli ila ingekuwa Serikali ya Chama kileeee, hali ingekuwa tofauti. Lakini najiuliza Serikali ya Chama kileeee ambacho RUZUKU viongozi wake hawaelezi inafanya nini, na wakati uleule Wabunge wakichangishwa kila mwezi!!

Angalau ya Serikali iliyoko madarakani tunashuhudia ujenzi na uboreshaji wa miundo mbinu na huduma za jamii. Najua una macho unaona hadi viongozi wa upinzani wanakejeli ati demokrasia na uhuru kwanza siyo vitu.

Mkono mtupu haulambwi
 
Unataka kuniaminisha kuwa Zitto ana akili kubwa na ushawishi kuliko uongozi wote wa serikali yangu pendwa?
 
ziro brain ni ZIRO tu kwaiyo alishindwa kusoma upepo likalopoka tu ujinga wake cheki majanga aliyoyasababisha kibaya zaidi bado hataki kuona upuuzi alioufanya aachie wadhifa dah ameshindwa kuwajibika kama liberman
 
Maendeleo ya kweli sasa ndo yanakuja...manyang'au bye bye
 
Mm naunga mkono kujitegemea. Lakin je tumejiandaaje kujitegemea ? Tuko vizuri kiuchumi kiasi kwamba hao jamaa tunaweza wafukuza.. ? Tusihitaj msaada wowote kutoka nje?
Yani kuna watanzania washenzi sana Hani yeye anapenda kupewa siku zote huu ni ulofa zaidi ya ule wa Sumaye.. Now lazima tu jitegemee kwa vyovyote vile
 
Mm naunga mkono kujitegemea. Lakin je tumejiandaaje kujitegemea ? Tuko vizuri kiuchumi kiasi kwamba hao jamaa tunaweza wafukuza.. ? Tusihitaj msaada wowote kutoka nje?
Nowdays lazima tuamue sio tumejipangaje ndo tuanze sasa ili tusitengeneze kizazi cha kutegemea wakoloni
 
Government of Canada.

Exercise a high risk of caution in Tanzania due to rising crime levels and the threat of terrorism.

Tuendeleeni kujidanganya.

 
Kuamua bila mipango ni kukurupuka . Mwangalie kagame ana sera zimefanana na za kwetu. Laki anahudhuria mikutano ya kitaifa isitoshe kwa uchumi wa nchi yake hajavurugana na serikal za nje. Hakuanza kwa kuvurugana na nchi zingine badala yake anajijenga kimya kimya.. akishapata anapunguza misaada.

Ninachosema ni kwamba ..is not about maamuzi, is about wakati. Hii ishu ingefanyika kimya kimya.. tuhakikishe tumevuka lengo mpaka uchumi wa kati then baada ya hapo sasa tunaweza tukapunguza misaada au kuacha kabisa.
Nowdays lazima tuamue sio tumejipangaje ndo tuanze sasa ili tusitengeneze kizazi cha kutegemea wakoloni
 





yote hayo uloandika wameyaandika..labda kam hukubahatika kufika shule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…