Baada ya WB na Denmark kusitisha misaada na uhusiano wanaofuata ni Scandinavia, EU, UK, Canada na Marekani

Tatizo wengi mnajua sana....no matter what,God is our refuge. ..ukiiombea nchi yako mabaya,basi ya kukute wewe na familia yako.

Mambo mengine Muwe mnatumia personal nouns....wengine tunamlilia Mungu juu ya Taifa.
Ndugu! Huyu Mungu Ni Wetu Sote. Hata Hao Wazungu Wanamwomba Pia. Na Pia Hatuombei Nchi Mabaya.

Principles Za Mungu Haziko Kama Za Mwanadamu. Wewe Unaweza Kusubiri Mungu Akutajirishe Kumbe Yeye Akatumia Mtu Mwingine Akupatie Unachohitaji. Sasa Usipo Behave Utapishana Na Baraka Kila Siku!
 
Amakweli nyani halioni kundu lake!.
 
Mnapoteka na kuua watu huwa ni siri? Mlipowateka wanaharakati wa kimataifa, dunia haikujua? Mlipompiga Lissu risasi, dunia haikujua? Mlipotangaza kukamata msshoga, dunia haikujua?Mnapitangaza Bungeni maamuzi yenu, dunia haisikiii?Mnapofunga wapinzani jela na kuwanyanyasa, dunia haisikii?

Acheni kulaumu watu kwa makosa yenu ya kupenda sifa na kukurpuka.

Ukipanda bangi huwezi kuvuna mahindi.
 
Bunge la Tulia Ackon liko bize kuandaa azimio la kumsifu na kumpongeza Jiwe kuhusu Koro show, ukichallenge chochote unatolewa nje.
Haya twendeni tu wazalendo wa nchi.

Kusikia kwa kenge mpaka damu zimtoke masikioni.
 
Mr president do not allow mambo machafu yatutokee nasema Tanzania tukila msimamo 100% Tutaanza vyema kutafuta vyetu na si kutegemea tena misaada
Nawakilisha.
 
Chini ya Amri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli nawahakikishia tunatoboa, hakuna kupigia wazungu Magoti
 
Tofauti kati ya tajiri na masikini : masikini anaona utajiri ni laana wakati tajiri anaona umasikini ni laana: jiwe anasema wanaoishi kitajiri wataishi kama mashetani kwenye utawala wake,umeelewa nini hapo?
 
Tafuteni 'International convention on civil and political rights' mtaona tz ni signatory. Tz ni sehemu ya dunia hii. Lazima tuheshimu haki za Binadamu. Haki za Binadamu sio suala la blabla. Ni lazima!
 
Nchi hizi ni wadau wakubwa wa maendeleo yetu, ni wadau wakubwa kwenye sekta ya madini, utalii, gas nk. Tunapobeza umuhimu wao tutegemee kuzorota kwa uchumi pengine hali inaweza kuwa mbaya zaidi ya Zimbabwe.

Kwa kweli naombea itokee hivi... tupige magoti tuombe wakate misaada yote.. hata wanyama wanajua ni wakati gani watoto wamekua na waende kujitafutia maisha yao.. Please God.. make this happen!
 
Hhhhhhhh

Waizi wamekuwa Wadau wa Kubwa wa Maendeleo kwa Tz

Tz tupo ndani ya usiku wa milele
Zimwi la misaada,litatumaliza kbs
 
Tatizo wengi mnajua sana....no matter what,God is our refuge. ..ukiiombea nchi yako mabaya,basi ya kukute wewe na familia yako.

Mambo mengine Muwe mnatumia personal nouns....wengine tunamlilia Mungu juu ya Taifa.

Mnachafua nchi kwa ulimbukeni wa madaraka kisha mjifanye mnaiombea? Kwa mwenendo huu miaka miwili ijayo athari za hizi hatua zitakuwa peupe.
 
Hawa watu wana ushirikiano wa hali ya juu, hawana msaliamtume hasa linapokuja suala la haki za binadamu na utawala bora,
Wanaponiudhi mimi hawa watu ni kuona "HAKI ZA BINAADAM" wanapofanyiwa Mashoga tu! Mbona hatuwasikii wakisema chochote wakati haki na utawala bora kwa raia wengine wanaponyimwa haki hizo?

Ndio, ngoja watunyime hiyo misaada, labda akili zitatuingia kichwani. Tumezidi mno kuwa wapumbavu.
Mtu anawekwa madarakani anaamua kuteka kila kitu, tunaona sawa tu!
 


Anapaswa kuongea kila kitu, kama mnafanya uhayawani mlitarajia watu wafumbie macho upuuzi wenu? Mnaumiza wasiokubaliana na mitazamo yenu, mnachezea box la kura na kutunga sheria kandamizi mnategenea watu wakae kimya. Kwa kuwa watu hawana nguvu ya kupambana na huu ubazazi wenu, basi acha itumike mbinu ya kuwatumia wenye nguvu zaidi yenu. Udhalimu hauna nafasi dunia hii.
 
Mnachafua nchi kwa ulimbukeni wa madaraka kisha mjifanye mnaiombea? Kwa mwenendo huu miaka miwili ijayo athari za hizi hatua zitakuwa peupe.
Haihitaji 'miaka miwili' Wakitukazia uzi, mwakani wakati kama huu tutakuwa taaban. Tuvifua tunavyovipiga sasa hivi kwa majigambo tutakuwa tumejaa (blisters) malengelenga, hata pa kupiga patakuwa hakupo tena.
 
na wewe imekuuma misaada kusitishwa? manake magonjwa mtambuka ana pretend kama hataki hiyo misaada kwa kisingizio cha kutatuliwa marinda.

nijibu hoja yako sasa; unaonaje mmutwange risasi huyo zitto mnaye mwona kama msaliti nambari wani kwa taifa kama mlivyo fanya kwa lissu? ukumbuke tayari mmesha anza na shamba lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…