PSL god
JF-Expert Member
- Nov 18, 2023
- 8,435
- 6,476
Tupe kisa basi pleasehapo ni kwa mkemia tuu, hosp za kawaida wife ataenda kuhonga, nina story za hivi vitu ila kuhadithia ndo shughuli
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupe kisa basi pleasehapo ni kwa mkemia tuu, hosp za kawaida wife ataenda kuhonga, nina story za hivi vitu ila kuhadithia ndo shughuli
Aseee ikawaje?? Jamaa lazima ilimuuma aseemahakamani utaambiwa uende ustawi wa jamii kuchukua kibali na utaratibu jinsi ya kupima na gharama zake ni laki moja kupima,ila muhimu kujiongeza kwa wale maafisa wa ustawi ili jambo liende kiuwepesi afu kama mkeo alikuchezea rafu lazima alete upinzani kwenye hilo jambo na lazima atajaribu kuhonga, embu mpe na yeye heka heka kidogo na ikiwezekana kabla ya mahakamani watafute maafisa wa ustawi wa jamii uongee nao kabisa then ukifika mahakamani katika kujieleza sema ya kwako na usikubaliane na talaka moja kwa moja we kazia kwanza kwenye DNA ili mnapoachana uwe na uhakika unahudumia damu yako kiroho safi. Natamani kungekuwa na voice note nikuhadithie kisa cha jamaa yangu jinsi alivyolea mtoto si wake na huyo mwanamke walikutana chuo mwaka wa pili sijui ndo kuzaa kumbe alibambikiwa mimba sasa kaja kupata safari ya marekani yani kuhamia huko pale ubalozi lazima watoto wapimwe DNA kujiridhisha ni watoto wake huwezi amini huyo mwanamke alikataa kabisa mwanae kupimwa DNA , ikabidi jamaa atumie mbinu mbadala dah majibu yanatoka sio mtoto wake.
Haya ni maajabuWewe jamaa unayopitia ni mimi mtupu miaka kadhaa iliopita, mimi tulipoitwa kwa mchungaji alietufungisha ndoa nilienda, kwingine kote niligoma mpaka talaka inatoka,
Na sikung'ang'ania chochote, nilikaa kimya kizito kilichomshtua hata yeye ,nilichukua vyeti vyangu tu nikaondoka.
Mungu anaongea nasi kwa njia nyingi,hapo amekuonesha mtu ulie nae.
Ila cha ajabu ,baada ya Talaka na muda kupita tulizaa nae tena.
Kuna uzaifu na ustaarabu, mleta maadq ni mstaarabuWewe ni mdhaifu
Nimehadithia baadhi kwenye commentTupe kisa basi please
Ok nimeonaNimehadithia baadhi kwenye comment
Ndo hivyo aliumia sana ukizingatia mtoto kahangaika nae sana mpaka akawa hawatunzi watoto wake wengine huyo mwanamke alikuwa kakaba kisa kaolewa na alimpitisha huyo jamaaa kwenye heka heka mpaka wanapeana talaka drama kibao , Mungu si athumani jamaa Mungu kamkunia nazi kasepa zake kwa trump na watoto wake wale ambao yule mwanamke alifanya wasipate matunzo mazuri kutoka kwa baba yao.Aseee ikawaje?? Jamaa lazima ilimuuma asee
Duuuh huyo mwanamke vipi kaolewa? Ana hela? Yukoje saivi au kachunda!?Ndo hivyo aliumia sana ukizingatia mtoto kahangaika nae sana mpaka akawa hawatunzi watoto wake wengine huyo mwanamke alikuwa kakaba kisa kaolewa na alimpitisha huyo jamaaa kwenye heka heka mpaka wanapeana talaka drama kibao , Mungu si athumani jamaa Mungu kamkunia nazi kasepa zake kwa trump na watoto wake wale ambao yule mwanamke alifanya wasipate matunzo mazuri kutoka kwa baba yao.
Hapo hakuna wema achukue watoto wake mpasuko ndio ishatokea hapo hao watoto baadae watajuana watapotambua yupi mzazi ana akiliNi vyema watoto wakalelewa na mmoja tu ili kuepusha mpasuko wa watoto wenyewe kwa wenyewe huko mbeleni. Hii inaweza ikaja kuwa vita mbaya zaidi.
Ahaa kumbe Mwanamke mwenyewe ni ana kazi? Huyo ni Mwanaume mwenzako: ushaur tulia hivyo hivyo, ukienda mahakamani wewe shikilia unampenda mke wako na huwezi mwacha kama anakuacha wewe sawa, hapo wao watamuuliza kwa nini anadai talaka, shida iko wapi, itakuwa upande wake kujibu ni kwa nini anataka talaka shida nini? Lako Moja tu mke wangu nampenda siwezi mwacha, hivyo yaanWakuu heshima kwenu. Poleni na majukumu.
Ndugu yenu numerudi tena kuwajuza yale yanayoendelea kunisibu, maana najua hapa wamejaa watu wenye upeo wa kushauri, kutia moyo ,kuonya, kukufungua jicho upate alert na wengine weeengi sana.
Wiki kadhaa zimepita toka nilete mikasa yangu na mazonge ya wife.
Soma: Mshkaji wangu anataka kumroga mama watoto wangu
Pia nikaleta huu: Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?
Sasa ni hivi, kwakifupi ni kwamba, baada ya wife kuamua kuondoka nyumbani, nikamtafuta mara kadhaa simu zikawa hazipokelewi, basi na mimi nikaamua kupiga kimyaa tu.
Si kupiga simu wala kutuma message.
Katika mazingira hayo, ya kutowasiliana, yeye akiwa kwao huko mitaa ya Boko, mimi nikaanza kupokea "samansi" kupitia ngazi za serikali.
Nikapelekwa dawati la jinsia polisi
Nikapelekwa baraza la kata
Nikaitwa kikao cha familia
(Koote huko, ni yeye, na msimamo wangu ulikua, kutafuta suluhu maisha yaendelee ila mwenzangu akagoma na kusisitiza dai la Talaka)
Nikaitwa tena polisi na kutiwa lockup
NIkatolewa kwa dhamana.
Niliporudi home nikakuta kahamisha karibia 50% ya kila kitu mle ndani, ikiwemo vitu vyake na vya watoto wetu wanne vyooote.
Nikafuatilia na kugundua kule baraza la kata ameshachukua form no.3 kwaajili ya kufungua shauri la talaka mahakamaani
Kipindi hiki chooote ni yeye anacheza offensive game ya kuniburuza namna hiyo anavyotaka, mimi nimetulia kwenye mode ya Deffensive game. Sitaki kushindana na mama watoto, hasa ukizingatia aliondoka na watoto.
Nikaona isiwe kesi, huyu mama kweli kadhamiria kuni destroy.
Ikumbukwe kuwa muda wote huo , niko busy na shughuli zangu za kibiashara na kusafiri mikoani, hivyo nalazimika kusitisha kazi na kuja kuitika wito mpaka nawekwa ndani, na kipindi hiki chote niliamua kuacha nyumba na kuhamishia makazi mwanza. Home pakawa pamebaki hapana mtu.
Baada ya muda nikapata wito wa mahakama, wife kafungua kesi ya kutadai talaka.
MImi nimetulia zangu tu wala sishindani naye.
Kila anachofanya, mimi napambana nacho, nachomoka, simtumii text, wala kumpigia kusema labda kumlaumu,au kumtishia au kumuomba msamaha aachane na hizi ishu, au kusalimia watoto, nimekaa kimyaa tuuu.
Mawazo nikaona yananizidia, nisije changanyikiwa, nikarudi nyumbani nyanda za juu kusini kwa baba na mama. Hii kwa kiasi kikubwa ikanisaidia.
ONA SASA,
Sasa week hii karibia na kesi, nikasafiri kurud Dar, kwakua nilikua na majukumu ya kikazi, nikaona isiwe tabu, nikatafuta taarifa za pale nyumbani panaendeleaje ? Nikamtafuta mtu wa jirani, akafika home akakuta pamevunjwa geti na nilimpomsihi anisaidie kuingia ndani na kukagua, akakuta 95% katika vitu vilivyobakishwa na wife alipotoroka nikiwa lockup, pia vimeibiwa.
Basi nilipomalizA majukumu yangu, nikaona nipite pale home, kisha nikaenda ku report polisi juu ya tukio, maana nikawaza, wife kafungua kesi ya talaka na moja ya madai yake ni mgawanyo wa mali kwa maana ya nyumba, sasa japo sikua na hamu tena na chochote juu ya mali, nikataka nipotezee tu hata nisifike home ila nikaona hii isije niletea shida kwenye kesi ya mgawanyo wa mali ikaonekana mimi kwa namna moja au nyingine nime temper na mali ambazo kesi ya wife inataka zigawanywe baada ya talaka.
Nikaona acha nipeleke taarifa niwe katika safe side.
Baada ya kumaliza ku report nikarudi tena nyumbani, na kushuhudia hali halisi, baada ya hapo, nikamuita kijana mmoja jirani yangu, nikamwambia achukue kila kitu kilichobaki mle ndani ambavyo wezi waliviacha.
Vitu vile vikubwa kubwa kama makabat na furniture ,na baadhi ya vyombo. Nikamwambia avichukue tu, nimempa, maana hawa wezi wanaweza wakarud tena wakaiba, hivyo bora jirani unufaike wewe ninayekujua. By the way sina mpango tena wa kurud kufanya maisha hapa.
Tukaachana nikaondoka kurudi hotel niilipofikia kusubiri siku ya kesi mahakamani maana imekaribia.
Sasa kitu cha kushangaza ni kwamba, yale niliyokua najiuliza na ku assume kichwani, ndiyo hayo hayo alikua akiyafikiri yule askari aliyenichukua maelezo. Maana yeye siku natiwa lockup na wife, yeye alikuwepo mpaka siku natoka, so mgogoro wetu anaujua.
Akaniuliza katika maelezo "je, katika tukio hili, unamtuhumu nani?".
Nikajibu "simtuhumu mtu wala sijui ni nani aliyetenda"
Akafunga maelezo na kufungua jalada kisha kunipa RB yangu.
Ila "off record" akaniambia " laiti kama mimi ningekua mpelelezi wa kesi hii, ningemtia hatiani mke wako kama mtuhumiwa namba 1"
Nikasema "hapana mimi sifahamu".
Japo kiukweli, ninasukumwa kuamini hili.
Ninaamini kabisa, wife amefikia hatua mbaya sana ya chuki juu yqngu na anajaribu kuni provoke indirectly na kuni push nichukue hatua ngumu, baada ya kuona kila chokochoko zake, mimi naamua kuzipuuzia, na kuingia gharama ya kukubali maumivu anayonisababishia.
Ikumbukwe chanzo cha mgogoro mzima ni mimi kufumania picha zake za uchi akiwa katika safari ya kikazi nikamhoji, akani temea shit, nikamchapa. Ila ndio hivyo anakomaa kuvunja ndoa.
Wakuu, na hayo tu.
NIwatakie mchana mwema
Hajaolewa tena ila ana watoto wengine alizaa tuu na jamaa mwingine, maisha yake ya kawaida tuu na huyo mume wake alikuwa anahudumia mwanae kila kitu sasa sijui sasa hivi kama bado anamuhudumia baada ya kujua alibambikiwaDuuuh huyo mwanamke vipi kaolewa? Ana hela? Yukoje saivi au kachunda!?
Mke kamtumia majambazi halafu arudiane nae tena, atakua na wazimu.Duuh.. Pole sana... huyo kesha rubuniwa... kwakuwa hajitambui nae kakubali kurubunika na kuharibu ndoa yake.... sasa, kwakuwa nimzoefu wa kuona visa vya namna hiyo... nakuhakikishia yafuatayo..
1. baada ya talaka, haitochukua muda mrefu, atakutafuta na kukuomba msamaha muyamalize. hiyo ni kwa sababu bwana mrubuni au mshauri akishaona ndoa imeharibika anakaa pembeni na ndo hapo atakapo ona dunia chungu maana hadi nduguze watamsimanga;
2. Akiona humduatilii ataenda kwa wazazi wako na kwa kasisi/sheikh wenu aliyewafungisha ndoa, akiamini huko ndo wataweza kulainisha moyo wako usahau ya nyuma na ugange yajayo...
3. Atakuwa kila siku akikupigia simu analia na kuomba msamaha huku akisema shetani alimpitia.. na wakati mwingine atakuja nyumbani kwako akishinda mlango huku akilia hivyo na majiriani wakimuangalia.. lengo la kufanya hivyo, umuonee huruma umsamehe.
sasa basi, akiwa anafanya hayo yote 1.wewe endelea kunyamaza hivyo hivyo... ali ajue kuwa, kuna baadhi ya vitu hapaswi kujaribu wala kunusa...
2. Hakikisha kwamba amejuta katika maisha ndipo hapo umsamehe... na ukimsamehe muweke katika uangalizi kwanza... (wala usiwe na tamaa Sanaa kushiriki nae tendo)
Mwisho lakini sio kwa umuhimu, naomba ulete mrejesho hatua hii ikifika...
Nami nahisi hili litakuwa jambo muhimu Mleta mada kulifanya, Usiogope kuambiwa fulani siyo wako au wote ni wako, lakini ni jambo muhimu sana katika mahusiano na talaka. Hata ustawi wa jamii wanashauri kwenye kesi zao za usuluhishi hasa linapohusu watoto, DNA ni muhimu kabla ya yote.mahakamani utaambiwa uende ustawi wa jamii kuchukua kibali na utaratibu jinsi ya kupima na gharama zake ni laki moja kupima,ila muhimu kujiongeza kwa wale maafisa wa ustawi ili jambo liende kiuwepesi afu kama mkeo alikuchezea rafu lazima alete upinzani kwenye hilo jambo na lazima atajaribu kuhonga, embu mpe na yeye heka heka kidogo na ikiwezekana kabla ya mahakamani watafute maafisa wa ustawi wa jamii uongee nao kabisa then ukifika mahakamani katika kujieleza sema ya kwako na usikubaliane na talaka moja kwa moja we kazia kwanza kwenye DNA ili mnapoachana uwe na uhakika unahudumia damu yako kiroho safi. Natamani kungekuwa na voice note nikuhadithie kisa cha jamaa yangu jinsi alivyolea mtoto si wake na huyo mwanamke walikutana chuo mwaka wa pili sijui ndo kuzaa kumbe alibambikiwa mimba sasa kaja kupata safari ya marekani yani kuhamia huko pale ubalozi lazima watoto wapimwe DNA kujiridhisha ni watoto wake huwezi amini huyo mwanamke alikataa kabisa mwanae kupimwa DNA , ikabidi jamaa atumie mbinu mbadala dah majibu yanatoka sio mtoto wake.
Yote Muhimu, ila asisahau kuomba kupima DNA kwa watoto asijetunza misukule.kwa mlipofikia, hudhuria Mahakamani..maana hata usipohudhuria shauri litaendelea kusikilizwa upande mmoja na kama ni Talaka itatolewa, ukiwepo utakuwa na uwezo wa kuweka kumbukumbu sawa, na pia uhusike kwenye mgawanyo wa Mali, na mjadala kuhusu watoto wako.
Usipingane na ombi lake la Talaka Mahakamani, ameshaku-push sana, ni muda wa kumpa Haki yake,
Chapili...ni kuhusu watoto, Mahakama yaweza kumpa uangalizi (custody) ya watoto, lakini una Haki ya kuwaona na kufahamu kinachoendelea (access),
au Mahakama yaweza kwenye suala la watoto, kuwapa Rufaa muende Ofisi za Ustawi wa Jamii mkajadiliane mustakabali wa watoto wenu,
Option zote mbili, Hatakuwa na Haki ya kukunyima au kuzuia wewe kuwasiliana na kujenga mahusiano na watoto wako,
ikiwa unahusika kutunza watoto una Haki 100% ya kuwaona/kujua maendeleo ya watoto wako, ikiwa atabaki na uangalizi wa watoto, ni vyema vipindi vya likizo, kwa wale ambao ni wakubwa, ukawachukua ukakaa nao kwa muda huo wa likizo ili waendelee kujenga mahusiano nawewe, hii ni Haki yako sio ombi.
Yakikamilika haya, tuliza kichwa kwa muda, pata huduma za kiroho kwa mujibu wa Imani yako, usikimbilie kutafuta mbadala ili kuonesha kuwa ume move-on, tulia, Relaaax (Darasa), kila kitu kitakuja kwa wakati sahihi, then endelea kupush kete zako za 2025.
Mkishapata wanaume nje mnaanza viburi na dharau , mwanamke akianza kucheat na akili hupotelea huko na kuanza kudharau mtu wake tofauti na mwanaume akicheat bado atakua na heshima na hatodharau mwanamke wake utofauti uko hapoDuuuh pole ndugu,,ila nini kinampa kiburi ivo.....