Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali

Aseee ikawaje?? Jamaa lazima ilimuuma asee
 
Haya ni maajabu
 
Aseee ikawaje?? Jamaa lazima ilimuuma asee
Ndo hivyo aliumia sana ukizingatia mtoto kahangaika nae sana mpaka akawa hawatunzi watoto wake wengine huyo mwanamke alikuwa kakaba kisa kaolewa na alimpitisha huyo jamaaa kwenye heka heka mpaka wanapeana talaka drama kibao , Mungu si athumani jamaa Mungu kamkunia nazi kasepa zake kwa trump na watoto wake wale ambao yule mwanamke alifanya wasipate matunzo mazuri kutoka kwa baba yao.
 
Duuuh huyo mwanamke vipi kaolewa? Ana hela? Yukoje saivi au kachunda!?
 
Ni vyema watoto wakalelewa na mmoja tu ili kuepusha mpasuko wa watoto wenyewe kwa wenyewe huko mbeleni. Hii inaweza ikaja kuwa vita mbaya zaidi.
Hapo hakuna wema achukue watoto wake mpasuko ndio ishatokea hapo hao watoto baadae watajuana watapotambua yupi mzazi ana akili
 
Ahaa kumbe Mwanamke mwenyewe ni ana kazi? Huyo ni Mwanaume mwenzako: ushaur tulia hivyo hivyo, ukienda mahakamani wewe shikilia unampenda mke wako na huwezi mwacha kama anakuacha wewe sawa, hapo wao watamuuliza kwa nini anadai talaka, shida iko wapi, itakuwa upande wake kujibu ni kwa nini anataka talaka shida nini? Lako Moja tu mke wangu nampenda siwezi mwacha, hivyo yaan
 
Duuuh huyo mwanamke vipi kaolewa? Ana hela? Yukoje saivi au kachunda!?
Hajaolewa tena ila ana watoto wengine alizaa tuu na jamaa mwingine, maisha yake ya kawaida tuu na huyo mume wake alikuwa anahudumia mwanae kila kitu sasa sijui sasa hivi kama bado anamuhudumia baada ya kujua alibambikiwa
 
Mke kamtumia majambazi halafu arudiane nae tena, atakua na wazimu.
 
Kosa hela usikose nguvu, mko bize na hela utafikiri zitawapeleka mbinguni.

Mko bize mpaka mnasahau afya zenu.

Ona, alichokosa mkeo ni mikito ndio sababu anajiamini na wewe hujiamini
 
Nami nahisi hili litakuwa jambo muhimu Mleta mada kulifanya, Usiogope kuambiwa fulani siyo wako au wote ni wako, lakini ni jambo muhimu sana katika mahusiano na talaka. Hata ustawi wa jamii wanashauri kwenye kesi zao za usuluhishi hasa linapohusu watoto, DNA ni muhimu kabla ya yote.
 
Yote Muhimu, ila asisahau kuomba kupima DNA kwa watoto asijetunza misukule.
 
Duuuh pole ndugu,,ila nini kinampa kiburi ivo.....
Mkishapata wanaume nje mnaanza viburi na dharau , mwanamke akianza kucheat na akili hupotelea huko na kuanza kudharau mtu wake tofauti na mwanaume akicheat bado atakua na heshima na hatodharau mwanamke wake utofauti uko hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…