Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali

Kuna malaflale mwenzio aliwahi kuleta mada ya kusema β€œ Mwanaume kama unajijua uko nyoronyoro usijaribu kuoa mwanamke wa kinyakyuma maana utateseka sana maisha yako na Pengine kupata kisukari na presha.

Let us reimagine masculinity πŸ’ͺπŸ’ͺ

Hao dawa yao uwe mndava kuzidi wao la sivyo utapata tabu sana.
 
Kwa hiyo mwanamke mwenye hekima anaweza kutaka kuachana sababu ya kupigwa na mumewe ??
Kiburi tu.
Ndiyo ,kama anampiga kila siku! Kwani yeye ni mtoto mdogo ambaye kila siku ni makofi ni ngumi siku atolewe jicho ? Au mwanamke haumii huyo mwanaume yeye kakamilika ?
 
Ndiyo ,kama anampiga kila siku! Kwani yeye ni mtoto mdogo ambaye kila siku ni makofi ni ngumi siku atolewe jicho ? Au mwanamke haumii huyo mwanaume yeye kakamilika ?


Labda Mwanaume awe kichaa kumpiga bila sababu.
Kinachowaponza wengi ni midomo yenu na ukosefu wa adabu na heshima kwa wanaume zenu.
Hakuna wa kukupiga bila sababu labda awe kichaa tu.
Unakuta mwanamke anakosa subira aliambiwa subiri tutaongea hataki anataka usiku mzima msilale umsikilize akilalalamq na kelele chunga nzima, Mwanaume gani anayataka hayo ??!

Kwanini uchane kitabu kuzima sababu ya ukurasa mmoja tu ?!
Hivi mnaijua thamani ya ndoa nyie ?!
Mnajitia wazimu wa kudai talaka Halafu mane da kusumbua manabii na waganga watalaka zenu wawarejee.
Halafu cha ajabu ni kama una kibwana chako kinakupa kiburi cha kudai talaka ili uwe huru ukiachika tu akijua nae anakuacha πŸ‘ŒπŸ‘ŒπŸ‘Œ
Ndivyo walivyo wanaume wengi.
Unaachika unaenda kuwa mchepuko wa kule wa mtu.
Hivi mkoje ?
Huwa mnajistukia kweli nyie ??!
 
Kwahiyo mwanamke huo mdomo wake anajiongelea tu bila sababu? Sikia nikwambie wanaume wengi wa siku hizi hawajui kuishi na wake zao mwanaume hivi unajua mwanamke anaanza kupevuka kuliko mwanaume? Sasa muoe ukizani mdogo, ndiyo maana mmeambiwa ishini na wake zenu kwa akili sio kuishi ishi tu bila kueleweka, unakuta kila siku unarudi jioni, basi weekend Kaa na mkeo muongee lakini napo anashinda mtaani, na akirudi busy kwenye mtandao unategemea nini hapo kama sio huo mdomo unaousema?
 
Wanaume wanakufa haraka kwa sababu ya mambo kama haya, nakufurahi unavyoshea unaondoa uchungu moyoni. Tafadhali usikae kimya ukatengeneza tatizo la moyo bali endelea kushea hapa nasi tutakupa mawili matatu.

Binafsi naamini asilimia mia moja mwanamke ndie anaejenga na kuvunja ndoa yake mwenyewe.

Kuhusu mali, nikushauri mpe zote na nyumba akachukue na ww kaka yangu mzuri nenda kaanze upya utauona mkono wa Mungu atakavyokupigania.

Huyu mke wako atakuja kuomba msamaha siku moja na kujutia yotee, ukweli huchelewa sanaa.

Sasa, focus kwenye kazi zako asije akakurudisha nyuma nimeona hata kwa ndg zangu jinsi wanavyoteseka na wake zao.

Mwisho, waombee watoto wako na uwekeze sana kupandikiza upendo wakuamini kwamba huna shida omba mahakama iweke utaratibu wakuwa na wototo wako. Ukiwa dar waangizie bolt waje wakuone.
 
Mpe talaka. Machine nyumba 100%. Kubali kuendelea kutoa matumizi yq watoto mpaka waffke 18years

Anza maisha mapya haraka sana iwezekanavo. Huyo mwanamke anaweza kukuua muda wowote.
 
Ahsante sana, nashkuru sana mkuu
 
Mpe talaka. Machine nyumba 100%. Kubali kuendelea kutoa matumizi yq watoto mpaka waffke 18years

Anza maisha mapya haraka sana iwezekanavo. Huyo mwanamke anaweza kukuua muda wowote.
Nimeamua kufanya hivyo kaka
 
Ahsante sana, nashkuru sana mkuu
Karibu rafiki natamani niwe nakusaidiaa mawazo ili uishi siku nyingi. Wewe wapende wazazi wako sanaa kupitia wao utapata amani maana hawataacha kukuombea kila siku. Usiache kutumia nguvu na akili kuweka bond kwa watoto wako maana huyo mwanamke anaweza kuwa brainwash watoto wako.
 
Huyo haijui dunia. Subiri kidogo tu atapauka atarudi anajigaragara.Nimeshaona wengi wanaondokaga kwa mbwembwe ila wakipigwa matukio hawataamini macho yao.
 
Hiiii πŸ™†β€β™‚οΈπŸ€¦β€β™€οΈ
Hao ni wajeuri pro max .
Kumbe ndio maana ?!
Lakini Hata wanawake wa makabila mengine wapo wakorofi hivyo hivyo na tamaa za mali na ushirikina.
Dah hata sio kabila ukikutana nalo la kukunyea linakunyea tuπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…