Kwanza wewe mwenyewe tambua unataka nini,hii utakusaidia kufanya kitu unachokipenda sababu field za IT zina badilika sana so unachokifanya hakikisha unakipenda,labda unataka Database(MySql,Oracle),Programming(python,Java,C++,PHP,Go),Networking (Cisco,Juniper,Huawei nk),Server,Cyber,System Analysis and Design.
Ukishajipima wewe mwenyewe unachokiweza na kukipenda,sasa ingia youtube mule kuna tutorial nyingi tu,download utapata maelekezo yote au ingia torrent napo kuna tutorial nyingi download video na vitabu,baada ya hapo soma sana theory na practical,ukishajilizisha sasa unaweza kwenda level za juu ktk hiyo field.
Husiogope mwanzo mgumu,mimi networking nimeijulia baada ya kumaliza chuo.Chuo nimetoka mweupe mimi na cheti changu ila skills sina,nilisoma Network YouTube na kuna vitabu nilivisoma ndivyo vilivyonisaidia.