Balqior
JF-Expert Member
- Jun 8, 2021
- 2,406
- 8,039
Kuna siku moja nilikuwa kwenye kijiwe cha draft hapa Dar, mzee mmoja alisema msaki (mmiliki wa kibo complex) anatuona Sie wote hapa hatuna akili, nilidhani wanaongea hivyo sababu wanamwonea wivu Ila baadaye nilikuja gundua maneno yao yana ukweli kwa kiasi flani, wala si wivu.
Yani utakuta rafiki yako kabahatika kupata tenda yenye mshahara mnono anaanza kukwambia maneno kama haya Katika nyakati tofauti mkiwa mnapiga story:
1) Huna hata baiskeli
2) Fulani hana pesa anaishi maisha magumu Kama wewe
3) Una akili za kimaskini na za kifukara kabisa.
Wakati hapo mwanzoni kabla mambo hayajamnyookea, hakuwa na kauli hizo. Ni kauli za kuumiza roho ila kwavile ni mshkaji unazipotezea.
Yani mtu anakwambia hivyo wakati yeye alivyokuwa kwenye kipindi kigumu kiuchumi, na wewe uko kwenye neema hukuwahi kumtamkia kauli hizo.
Waliowahi kukutana na hali kama hizi nje hapa mtoe shuhuda zenu.