Baadhi ya marafiki wakifanikiwa kipesa tu kidogo, wanaanza maneno ya kejeli

Baadhi ya marafiki wakifanikiwa kipesa tu kidogo, wanaanza maneno ya kejeli

Hakika mkuu wangu....

Haswaaa... ...

Jamii yetu HAIJIPENDI kiukweli....kwani mwenye kujipenda kidhati atajiamini vyema kwa hali yeyote uliyokuwa nayo........

Huku mitaani kunachekesha sana....sana yaani.....

Ukiwa na maisha ya afadhali kipato na ukaishi hulka za "DOWN TO EARTH" wandewa wanashangaa sana....watakuita majina tofautitofauti ...mara mshamba...mara mchawi na mshirikina wa ngende....🤣🤣

#Hatujawa duniani tuyaishi maisha ya wengine

#Siempre JMT🙏
🤣🤣🤣🤣
 
Hahaha hata hivyo maskini hapendi ukweli.
Umaskini uko kama kile ukimwambi ukweli wewe kilema anakwambia unamnyanyapaa.

Hao wazee mafaller tu...huyo Msaki ndio namjua alikuwa dalali wa mchanga lkn ni mpambanaji mwanzo mwisho.
😲😲

Mkuu sasa unamuona mtu ni mlemavu kabisa halafu tena unamwambia wewe ni kilema tu ?!!!
 
Kuna siku moja nilikuwa kwenye kijiwe cha draft hapa dar, mzee mmoja alisema msaki (mmiliki wa kibo complex) anatuona Sie wote hapa hatuna akili, nilidhani wanaongea hivyo sababu wanamwonea wivu Ila baadaye nilikuja gundua maneno yao yana ukweli kwa kiasi flani, wala si wivu..

Yani utakuta rafiki yako kabahatika kupata tenda yenye mshahara mnono anaanza kukwambia maneno kama haya Katika nyakati tofauti mkiwa mnapiga story:

1)Huna hata baiskeli
2)Fulani hana pesa anaishi maisha magumu Kama wewe
3)Una akili za kimaskini na za kifukara kabisa..

Wakati hapo mwanzoni kabla mambo hayajamnyookea, hakuwa na kauli hizo. Ni kauli za kuumiza roho ila kwavile ni mshkaji unazipotezea.

Yani mtu anakwambia hivyo wakati yeye alivyokuwa kwenye kipindi kigumu kiuchumi, na wewe uko kwenye neema hukuwahi kumtamkia kauli hizo.

Waliowahi kukutana na hali kama hizi nje hapa mtoe shuhuda zenu
Ni kweli inaumiza,lkn zinakupa akili ya kuhaso kutafuta cash.
 
surely also he shud learn to celebrate people when they r winning🤍
Mkuu mm sinaga wivu mtu wa karibu yangu akifanikiwa kipesa, kwasababu najua huenda one day yeye anaweza kuNisaidia, shida inakuja pale ambapo waliofanikiwa wanatoa kauli za kujiona wao ni demi gods

Nina bamdogo wangu mmoja huyo Rip alipata kazi hazina, yenye mshahara mnono, naye alikua na tabia ya kuita wengine maskini na kuwauliza kama wana hela plus dharau kibao Paubae5
 
kwani mkuu huwezi kufanikiwa na ukaendelea kuwa neema na baraka kwa wenzako badala ya kuwabagaza?

Ni ushamba huo. Tena matajiri wenyewe halisi hawana vimaneno vya kiswazi kama wakinamama wa Tandale
Mara nyingi waliokosa maisha bora(kula vyema na KUSHIBA utotoni ,kusoma vyema,malezi bora ya heshima na adabu kwa utu na kwa wengine) ndio wakipata FEDHA ukubwani huwa na hulka hizo....🤣

Ni "CHILDHOOD ABUSE" inayotengeneza POST-TRAUMATIC STRESS DISORDER....
 
Ni kweli inaumiza,lkn zinakupa akili ya kuhaso kutafuta cash.
Mkuu kwani wote tusio na pesa ni kwa sababu hatuhaso? na wewe ni wale wale tu. Mtu kama hana pesa basi mnamwita mvivu, mjinga, hakui kitu🤣🤣

Paul Makonda sasa hivi ni bilionea lakini enzi z nyuma akiwa kama mimi walimwona hivyo.

Hatuwezi kufanikiwa wakati mmoja tuache dharau. Tutamke maneno mema kwa wenzetu wenye changamoto za kiuchumi.
 
Haha jana nliingia Insta story ya sirjeff dennis, Humu jf anatumia ID ya Ontario, alisema hawezi pokea ushauri kutoka kwa mtu ambaye hajui kesho atakula nini, yeye anatafuta pesa za kula za wajukuu wake Pythagoras Me too chizcom Toxic Concotion
Unajua uzuri wa hii mitandao ya kijamii ipo kinadharia zaidi. Unaweza kuta mtu anajadili kuhusu nyumba yake na gari yake hapa kumbe hata mkokoteni hana na anaishi kwa mjomba akilala sebuleni.

Huyo anaekwambia anatafuta pesa za wajukuu ukute anashinda kijiweni matumaini yake yote yapo kwenye betting, ana bet shilingi 100 kwa matumaini ya kupata mamilioni. Kila analoliandika ni kupitia ndoto zake alizonazo kupitia pesa atakayoshinda siku hiyo kama mkeka ukitiki. Akishindwa anakuja na ndoto nyingine.

Ushauri wangu, usitilie maanani sana matajiri wa mitandaoni, wengi wao hiyo ndio sehemu pekee ya kuishi karibu na ndoto zao kwa kuigiza uhusika wa matamanio yao.
 
🤣🤣🤣🤣ukweli mtupu.
 
Kuna siku moja nilikuwa kwenye kijiwe cha draft hapa Dar, mzee mmoja alisema msaki (mmiliki wa kibo complex) anatuona Sie wote hapa hatuna akili, nilidhani wanaongea hivyo sababu wanamwonea wivu Ila baadaye nilikuja gundua maneno yao yana ukweli kwa kiasi flani, wala si wivu.

Yani utakuta rafiki yako kabahatika kupata tenda yenye mshahara mnono anaanza kukwambia maneno kama haya Katika nyakati tofauti mkiwa mnapiga story:

1) Huna hata baiskeli
2) Fulani hana pesa anaishi maisha magumu Kama wewe
3) Una akili za kimaskini na za kifukara kabisa..

Wakati hapo mwanzoni kabla mambo hayajamnyookea, hakuwa na kauli hizo. Ni kauli za kuumiza roho ila kwavile ni mshkaji unazipotezea.

Yani mtu anakwambia hivyo wakati yeye alivyokuwa kwenye kipindi kigumu kiuchumi, na wewe uko kwenye neema hukuwahi kumtamkia kauli hizo.

Waliowahi kukutana na hali kama hizi nje hapa mtoe shuhuda zenu.
binafsi sijaona kejeri zaidi ya kuona fursa tu katika hayo maneno,mnaweza mkawa marafiki lakini hujawahi hata muuliza ametoboaje mwenzio sasa anajaribu kukushtua kwa maneno ya kero ili uchukue hatua binafsi ningemwomba connection ili hayo anayokuambia yasijirudie
 
Back
Top Bottom