Baadhi ya marafiki wakifanikiwa kipesa tu kidogo, wanaanza maneno ya kejeli

Kuna siku moja nilikuwa kwenye kijiwe cha draft hapa Dar, mzee mmoja alisema msaki (mmiliki wa kibo complex) anatuona Sie wote hapa hatuna akili, nilidhani wanaongea hivyo sababu wanamwonea wivu Ila baadaye nilikuja gundua maneno yao yana ukweli kwa kiasi flani, wala si wivu.

Yani utakuta rafiki yako kabahatika kupata tenda yenye mshahara mnono anaanza kukwambia maneno kama haya Katika nyakati tofauti mkiwa mnapiga story:

1) Huna hata baiskeli
2) Fulani hana pesa anaishi maisha magumu Kama wewe
3) Una akili za kimaskini na za kifukara kabisa.

Wakati hapo mwanzoni kabla mambo hayajamnyookea, hakuwa na kauli hizo. Ni kauli za kuumiza roho ila kwavile ni mshkaji unazipotezea.

Yani mtu anakwambia hivyo wakati yeye alivyokuwa kwenye kipindi kigumu kiuchumi, na wewe uko kwenye neema hukuwahi kumtamkia kauli hizo.

Waliowahi kukutana na hali kama hizi nje hapa mtoe shuhuda zenu.
Kibo complex sio ya Msaki. Mmiliki wake ni AM.

Sent from my WAS-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna ile wamba wakiona umewamba hawakupigii hata simu tena kama zamani.
 
Waambieni hao wenye dharau kwa sababu ya pesa wanakosea sana wanatakiwa kujirekebisha maana maisha sio pesa peke yake.maisha ni watu.
 
Kuna siku moja nilikuwa kwenye kijiwe cha draft hapa Dar, mzee mmoja alisema msaki (mmiliki wa kibo complex) anatuona Sie wote hapa hatuna akili, nilidhani wanaongea hivyo sababu wanamwonea wivu Ila baadaye nilikuja gundua maneno yao yana ukweli kwa kiasi flani, wala si wivu.

Yani utakuta rafiki yako kabahatika kupata tenda yenye mshahara mnono anaanza kukwambia maneno kama haya Katika nyakati tofauti mkiwa mnapiga story:

1) Huna hata baiskeli
2) Fulani hana pesa anaishi maisha magumu Kama wewe
3) Una akili za kimaskini na za kifukara kabisa.

Wakati hapo mwanzoni kabla mambo hayajamnyookea, hakuwa na kauli hizo. Ni kauli za kuumiza roho ila kwavile ni mshkaji unazipotezea.

Yani mtu anakwambia hivyo wakati yeye alivyokuwa kwenye kipindi kigumu kiuchumi, na wewe uko kwenye neema hukuwahi kumtamkia kauli hizo.

Waliowahi kukutana na hali kama hizi nje hapa mtoe shuhuda zenu.
Ukishakua mkubwa, rafiki pekee wa kweli ni Mungu tu.
Weka imani yako mbele, halafu ishi maisha yako kwa namna unaona inakufaa na kukupendeza.

Wanaokuzunguka wanakusema na kukusimanga kila siku, sipokuwa hujapata nafasi ya kuyasikia au kutajua hayo.

Aidha ana pesa au hana pesa, hizo ndizo tabia za binadamu.

Jali mambo yako, wakuzungukao wape mipaka...ya taarifa zako na taarifa zako pia.
 
Mkuu nina mashaka humjui vizuri Sirjeff Dennis usingekuwa unayaongea haya! Kuna watu wanamaisha.[emoji16][emoji16]
Ujinga mtupu,siku 1 aliweka picha akaandika anashukuru Mungu kaweza kuwajengea nyumba Wazazi wake,jamaa likatoka huko likamwambia aisee bro kwa heshima naomba ufute picha ya nyumba ya Wazazi wangu.Huyo Jeff aka-mute comments na akaifuta picha hio fasta.

Vijana mnatapeliwa kirahisi kwa kuwekewa picha za mtu Yuko mahotelini,Mara anaendesha Gari,Mara Yuko showroom anapiga picha magari huku mkiwekewa zile hashtag za #MONEYMAKER#HUSTLER#CASHMONEY#THEBIGBOSS
 
Hao ndio wamejaa. Baada ya kutembeza bahasha kwa miaka mingi akija kupata wewe ambaye hujapata anakwambia mbona kazi zipo sema hujaamua tu. Maskini kashasahau alikotoka.

Mara nyingi hawa waliozLiwa familia maskini ghafla bin vuu wakapata fursa[emoji1787][emoji1787]

Huwezi kumkuta Rizione wa kikwete anaongea ujinga kama huo wa kutwezana
Jamaa mmoja yeye alikuaga kila baada ya miaka 2 anabadilisha kazi tu leo Co. hii keshokutwa amehamia Co. Nyingine halafu anasema vijana mbona kazi Tz hii zipo nyingi tu,akawa anasema haelewi kwanini vijana wanalalamika ajira hamna.

Lkn kwa Sasa ana miaka 2 Yuko nyumbani anatuma CV lkn hamna kitu.Ambacho alikua anajisahaulisha Ni Kwamba kazi zote alikua anazipata sababu dingi ake alikua na connection hapa mjini na hivyo jamaa kuona watu wengine hawapambani kupata kazi.Baada ya mzee wake kufariki mwaka juzi then ndipo na connection zikakata Sasa anaelewa kwanini kazi hua haziko.
 
Uk

Ukimjua mtu wa hivyo kaa mbali na yeye mwache aishi kivyake achana na urafiki wa hivyo na pia mtu akishatusua ww bado mzee baba hakuna urafiki tena. Kwa maana urafiki unachangamka ikiwa mnafanya kazi sawa
Jibu sahihi kabisa mkuu.Mkishapishana level za Maisha wewe jikatae kimpango wako.
 
Jamaa mmoja yeye alikuaga kila baada ya miaka 2 anabadilisha kazi tu leo Co. hii keshokutwa amehamia Co. Nyingine halafu anasema vijana mbona kazi Tz hii zipo nyingi tu,akawa anasema haelewi kwanini vijana wanalalamika ajira hamna.

Lkn kwa Sasa ana miaka 2 Yuko nyumbani anatuma CV lkn hamna kitu.Ambacho alikua anajisahaulisha Ni Kwamba kazi zote alikua anazipata sababu dingi ake alikua na connection hapa mjini na hivyo jamaa kuona watu wengine hawapambani kupata kazi.Baada ya mzee wake kufariki mwaka juzi then ndipo na connection zikakata Sasa anaelewa kwanini kazi hua haziko.
Hahahaa wapo wengi sana wa namna hii. Hata akina Nape walikuwa wanapata vyeo sababu ya connection sio kwa sababu ya uwezo wao binafsi. Awamu ya tano walipoteana.

Ukibarikiwa Mshukuru Mungu lakini usianze kudhihaki wenzako ukawaona ni wajinga.
 
Hahah nadhani kwa ule upepo waliopitia wa awamu ya 5 watakua wamepata Somo kwama kazi walikua wanazipata not based on merit.
 
Back
Top Bottom