Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

Hao maisha yao ya uzeeni yatakuwa na uhakika wakiishi within their means.., tena unajua ni vema mtu ukafanya kitu ulichozoea sasa mtu ulikuwa Muhasibu miaka yako yote umestaafu eti ukawe mkulima (different lifestyles ) unaweza jikuta unanunua stress na ugonjwa wa moyo au pesa yako kupotea bila habari..., By the way unasema hawa watakuwa na maisha ya shida vipi wazee wa kesho ambao ndio wachuuzi wa leo ambao they are not pensionable.... (Tena hao itakuwa sio tu shida kwao bali Kero kwa jamii ya kipindi hicho kuzungukwa na wazee ombaomba)

 
Kina fanya kazi taasis nyingne ila sio jwtz, waligoma na wanalipwa yote.
Kumbe Jeshini wanakula yote ya Mkupuo??

Nadhani watumishi wengine wangekuwa na Umoja, wangekataa huo upuuzi wa kupewa 33% badala ya kupewa yote kama ilivyo Wabunge na hao JWTZ kama ulivyosema
 
Unaona sasa, halafu mtu aniambie nilale tu
Mawazo ya uzee na maradhi hayajui labda
Kwanza bora kufa ila maradhi ndio mtihani mara pressure, miguu kuwaka moto, maradhi ya kusahau maana akili haifanyi kazi zaidi ya kuangalia kuku za jirani 😄 🤣
Yaani uzee unaleta majanga
Ntafanya kazi hata siku nne kwa wiki tosha kabisa
 
Umesema sahihi, ndiyo maana inashauriwa uwekeze eneo ambalo una ABC nalo

Mfano Engineer wa Ujenzi kuwekeza kwenye Ukandarasi/Local Fundi ama hardware za Vifaa vya Ujenzi

Lakini unakuta ni Engineer halafu unaenda kufungua Maabara ya afya, hapo unaweza kupata stress kwenye usimamizi
 
Hongera sana Kwa huyo Mstaafu mwenzetu kuweza kuwekeza mapema

Mtu wa hivyo hakosi milioni 100 hadi 300 Benki

Kwa Vijana waliopo makazini

Kupanga ni Kuchagua
Kabisa.kijijini kuna fursa nyingi kuliko mjini.mwl ukipangwa kojijini nunua kreti la bia sherekea.mjini utaishia kufundisha vitwisheni uchwara na kua dalali au winga kariakoo.kijijini utalima utafungua ma hard ware shops utafuga utapiga hela.hauna walimu wana maisha mazuri kama wa vijijini
 
Muhimu sana kujishughulisha baada ya kustaafu.

Kwanza unakuwa na direct intact na wateja wako, kwahiyo unafanya socialization. Kwa muda unaachana na Upweke

Lakini pia unafanya seli za mwili kuendelea kufanya kazi Kwa ufasaha, maana unazishughulisha kufikiri n.k

Kwahiyo utachelewa kuzeeka

Lakini pia unakuwa na uhakika wa kusimamia vizuri miradi na Kipato chako moja Kwa moja

Hata kama itakuwa Siku 4 Kwa wiki

Mimi yule Mzee wangu, yupo hai hadi sasa, na kama Mungu akipenda huenda akafika hata 95 huko
 
Ni kweli huko Vijijini Kuna fursa nyingi Kwa Walimu ama Watu wa afya wanaofanya kazi huko

Changamoto yao ni kushindwa kuamka(wengi vichwa vyao vimelala)

Lakini wangekuwa serious unanunua ekari zako 100 ama 50 unalima zako fresh tu

Wakati huo huo unafuga zako Kuku/Nguruwe/Ng'ombe wa Maziwa/Mbuzi ili kuongeza kipato

Shida yetu Watumishi wengi vichwa vimelala
 
Asante Sana ndugu
 
Mkuu Mimi naona Kwa watu wote hata wale wasio ajiriwa!

Unatakiwa itegeshe vitega uchumi vya kudumu biashara ya kudumu ama kilimo endelevu pamoja na ufugaji. Hii itakupa uhakika wa maisha hata kama utapata faida kidogo ni vyako. Ahsantee sana Kwa Uzi huu.

Mzee wangu tulimshauri awekeze kwenye nyuki,ufugaji samaki pamoja na ng'ombe wa maziwa kamwe hakutuelewa kabisa Tena tulionekana sisi tunazitaka Hela zake!

Sasahivi anakumbuka misitu upo binde lipo Hela hamna na sisi tuna mambo yetu ya kuwekeza vilevile anapata laki ama 50k nikiwa nayo au zaidi hata400k mara Moja moja
 

Shida ya kutoelewa unachosoma. kustaafu ni kupumzika hutafanya kazi kama ulivyokuwa mwanzoni, hutaamka na kukimbizana kama mwanzo, hutashinda kazini kama mwanzo.
Utapita kukusanya maokoto ina maana utakwenda kwenye shughuli zako ila si kwa ubize kama zamani, ni kama kusimamia na kuangalia tu kazi zinavvyoenda.
utakaa chini ya mwembe ina maana kuna wakati utapumzika hii haina maana wewe utakaa tuuuu maisha yako yote, nooo kuna vipindi vya kuburudika na kupiga umbea kwa kuwa shughuli zako ulizozianzisha zinaendelea vizuri na kukulipa huna stressss . ukistaafu sio muda wa kusimamia mijengo.... ni muda wa kupokea kinachozalishwa kwenye mijengo uliyonayo. Kutembelea wajukuu maana yake utakuwa na mitoko yako midogo midogo nje ya mkoa wako kwa raha ukasalimie kwenu au kokote utakako. THINK BIG EEEEEE
 
Uwekezaji kwenye masoko ya Fedha pia.wastaafu wengi wako huko
 
Wiki iliyopita nilikuwa morogoro mvomero asee nisiseme Sana ila Tz Kwa upande wa ardhi imebarikiwa sana nitaenda huko kufuga na kulima
 
Kwa Sasa hata kama mkataba wa miezi 3 nssf inakatwa na lazima uwe Tin no.
 
Changamoto iliyopo ni watumishi kukosa msimamo na Umoja, wangekuwa wengine mbona saivi wangekuwa wamepelekewa asilimia ya Mkupuo hadi 100 ama 75/25
Hii nchi umoja haupo, juzi nimetoka sehemu "shamba" ukifika kituo cha mafuta "sheli" hawakupi mafuta wanaswma ulete chombo kinachotumia mafuta, sasa mtu unawaza uyoe pampu km 50 utembee nayo ili ujaze wese, utarudi mara ngapi na pampu, au trekta au mashine zingine za shamba ila watu wapo kimya washakubaliana na hali wanatumiq boda boda unaijaza mnaenda pembeni ndo mnatia kwenye dumu
 
Nimekuelewa vizuri sana tangu mwanzo
Kusimamia shughuli sio kazi ya kunitoa jasho bali ni akili tu isiwe mahali pamoja
Wengi wa wastaafu hapa nilipo wanafanya kazi bado ila ni siku chache kwa wiki
Unakatwa NI number tu ila kodi hulipi na ni wengi sana
Nitakuwa na uwezo wa kula bila kumtegemea mtu ila ntafanya shughuli ndogo ndogo sana za kuni keep occupied

Unapokaribia kustaafu unapata ushauri kutoka kila sehemu serikalini hata bank pia wanatoa nao
Tuombeani kheri maana hata wewe bila umauti nakuombea ustaafu unavyotaka wewe na unavyoona ipi ni sawa kwako
 
Hiyo Kali Mkuu, kwahiyo pamoja na hela yako lakini hawakupi huduma??

Hii Nchi kama ulivyosema, hatuna Umoja kabisa kwenye mambo ya msingi zaidi ya kufarijiana kwenye misiba tu
 
huu ni ushauri BORA na mzuri kwa waajiriwa wa serikalini.
mie mgalatia acha niendelee kupambana na maisha ya mtaa kwa mtaa.
Lakini Mkuu sio waajiriwa pekee, hata wewe uliyejiajiri kupitia shughuli za Kilimo ama biashara bado unaweza kujifunza dhima ya andiko hili

Kwamba tujipange kwaajili ya Uzee wetu

Tujitahidi kuwekeza ili tusiteseke kwenye Uzee wetu
 
Ushauri murua kabisa Mkuu 🙏
 
Kwa Sasa hata kama mkataba wa miezi 3 nssf inakatwa na lazima uwe Tin no.
Hiyo safi, nafikiri watatofautiana kwenye Posho ya Kila Mwezi

Huyu wa Serikalini atakuwa na uhakika wa kuchukua Kila Mwezi

Wakati huyo wa private sector aliyefanya kazi Kwa muda mchache hatokuwa akipata Posho ya Kila mwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…