Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Nipo kwenye nafasi ya ushauri wa suala la biashara fulani ya vijana 2.
Je Kama ungekuwa kwenye miaka 20 hapo, na una nafasi ya umiliki wa eneo lenye potential kiasi chake.
Ukisema uli pangishe ni Kama kutoa sadaka tu, ila kuuza ni Kama una pata mtaji wa maana.
Je ungeuza mkuu au unge endelea kuli miliki, akati mambo yako yapo ndivyo sivyo??
Kwanza kabisa mimi si mtaalamu wa mambo ya ushauri wa kiuchumi na hapa tunapeana elimu ya kiujumla tu, si ushauri wa kitaalamu.
Na pengine kuna haja ya kumtafuta mtaalamu, hususan kama hela zitakazohusika ni nyingi.
Ni vigumu kutoa ushauri wa uhakika bila kupata habari zaidi. Kwa mfano, uhitaji wa pesa ni wa dharula kwa kiasi gani?
Kiujumla, ushauri mzuri kuhusu mambo ya ardhi yenye potential si kuuza, ni kukodisha, au, kutegemea na hati kama zipo, ukubwa na uzuri wa eneo, kutumia ardhi kama collateral katika kuchukua mkopo (hapo unaweza kumaliza tatizo la kupata pesa za kufanyia kazi nyingine bila kuuza hiyo ardhi).
Kwa hivyo, kuna namna ya kuendelea kulimiliki hilo eneo, na pia kupata namna ya kuondoka kwenye matatizo ya kifedha.
Matajiri wengi hununua mashamba makubwa, si kwa sababu wanataka kuyatumia kulima sana, bali kwa sababu wanataka kuyatumia kama collateral katika kuchukua mikopo.