MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Huu ni ujinga wa hali ya juu. Kama mtoto ni wa Popoma muite Clara Popoma badala ya kumpa ubini usio wake.
Single mama baadhi yenu mnawapa ubini wa baba zenu kitu ambacho sio sawa. Hasira zako kwa aliyekupa mimba hazimhusu mtoto.
Yule ni baba yake wa damu hivyo ni haki ya mtoto kuitwa kwa jina lake. Ugomvi wenu usimhusishe mtoto.
Nimeandika kwa hasira baada ya mtoto mmoja wa kike kukosa msaada kwa babu yake baada ya babu kuona mjukuu anatumia ubini wa kwa mama. Kijana wa huyu mzee alizaa na binti na hawakuoana.
Na kijana ni mtu mpuuzi na mlevi ambaye katelekeza damu yake. Baada ya mwanamke kuona mambo magumu ndo akaamua kwenda kwa mkwewe kuomba msaada.
Yule dingi hakuwa na noma ila akatibuka vibaya baada ya kuona mjukuu wake hatumii jina la ukoo wao.
Akasitisha huduma zote na kutaka jina libadilishwe kwanza.