Baadhi ya Single mama acheni tabia mbaya ya kuwapa watoto ubini wa kwenu badala ya baba zao halisi

Fatilia vizuri mkuu sakata la USAID kabla ya kutolea mfano. Wao hawajasusa bali wamepata Boss asiewapenda kawakatishia bajeti zao kwa ushauri wa musk.

Babu na USAID ni vitu viwili tofauti
Sawa Ndio maana nimetumia mfano WA USAID mwanzoni walikuwa wanatoa ila baadae wakasusa na huna cha kuwafanya
 
Walimuita mwanangu John Mwampetele badala ya John Shimba ya Buyenze. Wakati wa kwenda shule ulipofika hawa hapa eti wanataka nianze kulipia ada tena academy kabisa. Niliwauliza swali moja tu "Huyo Mwampetele ndiye baba wa mtoto?"

Waliondoka!

Mtoto walinikatalia kumchukua halafu eti wananiletea Umwampetele kha! Mbona walibadilisha jina chap! 💪
Mtoto kama unatoa matunzo na wakakataa kumuita ubini wako una haki ya kughaka sio mtu umekimbia majukumu alafu anataka haki juu ya huyo mtoto ni ujinga.
 
Huu ni ujinga wa hali ya juu. Kama mtoto ni wa Popoma muite Clara Popoma badala ya kumpa ubini usio wake.

Single mama baadhi yenu mnawapa ubini wa baba zenu kitu ambacho sio sawa. Hasira zako kwa aliyekupa mimba hazimhusu mtoto.

Yule ni baba yake wa damu hivyo ni haki ya mtoto kuitwa kwa jina lake. Ugomvi wenu usimhusishe mtoto.

Nimeandika kwa hasira baada ya mtoto mmoja wa kike kukosa msaada kwa babu yake baada ya babu kuona mjukuu anatumia ubini wa kwa mama. Kijana wa huyu mzee alizaa na binti na hawakuoana.

Na kijana ni mtu mpuuzi na mlevi ambaye katelekeza damu yake. Baada ya mwanamke kuona mambo magumu ndo akaamua kwenda kwa mkwewe kuomba msaada.

Yule dingi hakuwa na noma ila akatibuka vibaya baada ya kuona mjukuu wake hatumii jina la ukoo wao.

Akasitisha huduma zote na kutaka jina libadilishwe kwanza.
Hili jambo ni la kitamaduni karibu makabila yote Tz.

Mwanamke akizalia nyumbani bila kuposwa mtoto ni wa kwao, mtoto ataitwa kwa majina ya bibi au babu yake.
 
Kama hakupewa taarifa basi atulie anafoka foka nini mtoto si wao afate taratibu apewe jina la ukoo wake. Saa nyingine mnaepushiwa laana za ulevi kwa jina kuchepushwa
Wewe umeelewa huu uzi au ndo unaleta hasira zako za ki-singo mama?
Kama ambavyo mtoto ana haki ya kuitwa ubini wa baba yake halisi hivyo hivyo mtoto ana haki ya kupata matunzo kutoka kwa huyo huyo baba halisi.
Kama unaona huna haki ya kutunza mtoto hivyo hivyo huna haki yeyote ya kudai ubini wako kwa huyo mtoto.

Hii tabia ya kijinga ya kuzaa hovyo watoto na kuwatelekeza kwa matumaini eti akikuwa atanitafuta ni dhana iliyo pitwa na wakati dunia ya sasa imebadilika.
Kama sasa hivi unazaa mtoto unamtunza, unamsomesha ,unampa kila kitu lakini akisha jitegea hana muda na ww sembuse ambaye ulimtelekeza?
Single mama detected...
 
Fatilia vizuri mkuu sakata la USAID kabla ya kutolea mfano. Wao hawajasusa bali wamepata Boss asiewapenda kawakatishia bajeti zao kwa ushauri wa musk.

Babu na USAID ni vitu viwili tofauti
Sawa maana yangu utakuwa hujanielewa....Babu kaona akisomesha kwa jina la ukoo WA mwingine maana Yake ukoo wake hautaendelea atakuwa amefanya kumnufaisha mama WA mtoto....
 
Wewe umeelewa huu uzi au ndo unaleta hasira zako za ki-singo mama?
Single mama detected...
Mkuu jibu hoja mm ni kati ya watu ni sio penda kitu kinacho itwa singo mother na content zangu nyingi kuhusu hili zinajidhihilisha hebu zifatilie ila katika hili nawatetea.
Mtu unapo komalia eti ubini wa baba halisi ni haki kwa mtoto, je huo ubini ni muhimu kwa mtoto, kuliko uji wa lishe, nguo, matibabu, elimu, chakula na mahitaji ya kila siku kwa mtoto ambayo huyo baba halisi amekataa kuvitoa?
Huyo mtoto unaye ngangania aitwe ubini wako angetelekezwa kama ww ulivyo mtelekeza akafa huo ubini ungemuita nani?
Haki huwa inaenda na wajibu ,huwezi kudai haki kwenye kitu ambacho hujawahi kutimiza wajibu kukihusu utakuwa mjinga na mpumbavu.
Waafirika tusipo acha tabia ya kutaka majibu rahisi kwenye maswali magumu tutaendelea kuwa jamii iliyo jaa wapumbavu na upuuzi mwingi.
 
Kwa hiyo ndg ukilea watoto yatima utawaita ubini wako kisa tu unatoa matunzo!? Kila damu ina asili yake,mstake kubadilisha damu za watu kisa mnatoa matunzo! Huu ujinga alitaka kuufanya Dada yangu kumpaa mtoto jina letu la ukoo na nikamkatilia, nikamwambia mtoto ana baba yake wa damu na ndiyo jina lake apewe hata kama Baba ni chizi!!
 
Jikite kwenye mada na sio kuanza kulilia watu hapa. Ukibadili ubini basi hudumiwa na huyo mwenye ubini na sio tena kutaka familia ya baba halisi ikusaidie.
 
Huu ni ujinga wa hali ya juu. Kama mtoto ni wa Popoma muite Clara Popoma badala ya kumpa ubini usio wake.

Single mama baadhi yenu mnawapa ubini wa baba zenu kitu ambacho sio sawa. Hasira zako kwa aliyekupa mimba hazimhusu mtoto.

Yule ni baba yake wa damu hivyo ni haki ya mtoto kuitwa kwa jina lake. Ugomvi wenu usimhusishe mtoto.

Nimeandika kwa hasira baada ya mtoto mmoja wa kike kukosa msaada kwa babu yake baada ya babu kuona mjukuu anatumia ubini wa kwa mama. Kijana wa huyu mzee alizaa na binti na hawakuoana.

Na kijana ni mtu mpuuzi na mlevi ambaye katelekeza damu yake. Baada ya mwanamke kuona mambo magumu ndo akaamua kwenda kwa mkwewe kuomba msaada.

Yule dingi hakuwa na noma ila akatibuka vibaya baada ya kuona mjukuu wake hatumii jina la ukoo wao.

Akasitisha huduma zote na kutaka jina libadilishwe kwanza.
Wapumzisheni Hawa single mama hamjui masaibu wanayokumbana nayo ata akimuita vyovyote ni sahihi as long as hajavunja Sheria za nchi
 
Huyo Babu ndezi tu alitegemea kubembelezwa wakati hawakulea hata mimba wala kutoa kifuta jasho kwa wazazi wa mwanamke. Azile tu mtoto akikua asije mlaumu kwa kumtelekeza
Numbisa, magombano yako na mzazi mwenzako yaishie kwenu mtoto hausiki kwa lolote. mostly mtoto akikuwa atabaki na ma trauma ya ajabu kwa ujinga wa wazazi.
 
Toxic ulevi wako malizia kilabuni sio unazalisha ovyo bila matunzo ukitegemea utaletewa mtoto atumie ubini wako pole sana. Mtoto atateseka kwa ujinga wako

Nikuulize,
Huyo mtoto uliyempa ubini wa mama akiwa mtu mzima akataka majina ya baba yake haijalishi baba alivuruga vipi akasema anataka majina ya baba yake. Utamsaidi vipi huyo mwanao?
 
Umesema kakua. Utamwambia alipo ataenda mwenyewe kuchambua pumba na mashudu na mahakamani majina yanabadilika vizuri tu atabadili

Hadi kufika hatua ya mtoto kuhangaika mahakamani kubadili majina ni kumuingiza kwenye mafarakano ambayo hayajawai kumuhusu.

Ndio tunasema mtoto hausiki kwenye magombano yako na mzazi mwenzako... usimuhusishe mtoto kwa lolote baya la mzazi mwenzako.

unayapa kazi nzito maua kwa kosa la miba.
 
Kwa hiyo ndg ukilea watoto yatima utawaita ubini wako kisa tu unatoa matunzo!? Kila damu ina asili yake,mstake kubadilisha damu za watu kisa mnatoa matunzo! Huu ujinga alitaka kuufanya Dada yangu kumpaa mtoto jina letu la ukoo na nikamkatilia, nikamwambia mtoto ana baba yake wa damu na ndiyo jina lake apewe hata kama Baba ni chizi!!
Huyo umesha muita yatima ina maana mzazi wake hayupo wenda angekuwepo angeweza kutimiza majukumu yake.
Nimekuuliza huo ubini ni muhimu kwa mtoto kuliko matunzo ya mtoto?
Yaani ww unaona mtoto ana haki ya ubini wa baba yake ila hana haki ya kupata matunzo kutoka kwa baba yake una akili kweli ww?
Mbona kwenye ndoa zenu wamejaa watoto wasio kuwa wa wenu na wanaitwa ubini wenu na si wa baba zao halisi?
vipi wale wanao kataa mimba utamuitaje mtoto ubini wa baba aliye sema hamtambui?
 
Nikuulize,
Huyo mtoto uliyempa ubini wa mama akiwa mtu mzima akataka majina ya baba yake haijalishi baba alivuruga vipi akasema anataka majina ya baba yake. Utamsaidi vipi huyo mwanao?
Vipi kama huyo baba alipelekewa mimba akaikataa kuwa haitambui?
 
Back
Top Bottom