KUna mwanamke mmoja aliolewa na kaka angu lakini waliachana baada ya bro kufukuzwa kazi na yule mwanamke akaolewa na mwanaume mwingine, wakati huo walikua wamezaa mtoto ambae alikua bado mdogo sana nafikiri mwaka mmoja
Hapo kati kuna jitihada za familia zilifanywa kupata access ya mtoto lakini yule mwanamke aliweka uzibe. Miaka imeenda broo amefariki. Mwanamke aligoma mpaka mtoto kuja kwenye msiba na arobaini ya baba ake. Familia tukaona haina shida mtoto akiwa mkubwa atajua ana ndugu zake, akiamua kututafuta au kutupotezea ni maamuzi yake
January kanitafuta yule mwanamke anasema mambo yake yameyumba kidogo nimsaidie kulipa ada ya mtoto. Nikasema sawa nikamwambia anitumie jina la mtoto na jina la shule na namba ya akaunti ya benki nikalipe benki Ile kutuma jina la mtoto naona hana ubini wa broo, nikamwambia silipi iyo ada