Baadhi ya wanawake ni wakatili kuliko wanaume toka enzi na enzi

Baadhi ya wanawake ni wakatili kuliko wanaume toka enzi na enzi

Huyo alisema ana body kali hadi wanaume wenzie wanamtolea udenda,,
Heeeeeeeh tena!! No wonder na kichaa cha mimba anakikataa kitu ambacho wataalamu wanakubali🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️
 
Huo ndio ukweli, msiwe mnatishwa na machozi ya wanawake hata siku moja.

Mwanamke ni mtu katili sana ambae anaweza kukushangaza matendo yake hadi ukaduwaa!

Fikiria mtu anabeba mimba bila kulazimishwa halafu baadae anaitoa hiyo mimba, au anazaa kabisa baadae kwa mikono yake anayonga na kuua mtoto!

Kiasili mwanaume ameumbwa na huruma sana, mwanaume anaweza kuhudumia mke na watoto miaka kibao hadi anakufa na hautosikia kelele, ukiyumba kidogo kiuchumi upewe sapoti kidogo na mwanamke taarifa zitafika hadi kwa mjumbe wa mtaa, hadi uliosoma nao chekechea watajulishwa haraka sana!

Vitabu vyenu vimeandika tuishi nao Kwa akili kubwa sana.
Unamaanisha Samia ni mwanamke katili ?
 
Tena hiyo misukosuko imkute hadi huko alikojibanza
Hivi hii compaign ya kuwavisha wanawawake ubaya kiiila kukicha hapa jukwaani ina agenda gani nyuma yake!! Ili wanawake waonekane ni mashetani kisha waoane wao kwa wao au🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️
 
Heeeeeeeh tena!! No wonder na kichaa cha mimba anakikataa kitu ambacho wataalamu wanakubali🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️
Tungemuombea akipate lakini sasa ndo hata afanyeje hawezi kubeba mimba
 
Hivi hii compaign ya kuwavisha wanawawake ubaya kiiila kukicha hapa jukwaani ina agenda gani nyuma yake!! Ili wanawake waonekane ni mashetani kisha waoane wao kwa wao au🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️
Ndo maana yake mi napambana nao kila siku, wivu na ushindani ni mkali sana kwa hii jinsia ya mabibi na mabwana
 
Ndo maana yake mi napambana nao kila siku, wivu na ushindani ni mkali sana kwa hii jinsia ya mabibi na mabwana
Kuna uzi uliwahi anzishwa, sikumbuki jina la member, ulikuwa unasema jf ni kimbilio la mashoga. Akaongelea namna vita ilivyo dhidi ya mwanamke kutoka kwa hao viumbe, maana wanahisi wanawazibia riziki zao. Aaah slishambiliwa na uzi ulifutwa shwaaaa. Ila sasa njoo uzi wa kupondea wanawake, utadumu balaa.
 
KAma alivokatili huyu mama tulienaye sa hvi katili hakubaliki na ni kero
 
Kuna uzi uliwahi anzishwa, sikumbuki jina la member, ulikuwa unasema jf ni kimbilio la mashoga. Akaongelea namna vita ilivyo dhidi ya mwanamke kutoka kwa hao viumbe, maana wanahisi wanawazibia riziki zao. Aaah slishambiliwa na uzi ulifutwa shwaaaa. Ila sasa njoo uzi wa kupondea wanawake, utadumu balaa.
Jf inafanya kazi kinyume nyume nyakati hizi, mada zisizo na mantiki zipo zinatrend mashoga yapo yanatrend, limebaki jina ila ladha yake inazidi kuisha
 
Sisi ndo makatili.

Ogopa mtu anayeweza kuua viumbe milioni 3 ndani ya dk 2 kwa mkono tu bila silaha yeyote. Kwanza dk 2 nyingi....😅

Natania

Mleta mada unajaribu kuhukumu kundi zima la watu kwa makosa ya wachache.

Unajaribu kuwalinganisha wanaume na wanawake kwa mapungufu yao, kitu ambacho hakiwezekani kwasababu hayo makundi yana tofauti za kujitosheleza, yanapitia hali tofauti kwenye maisha.

Na isitoshe hujajaribu hata kuweka sawa mizani, ungesema na wanaume wanakosea wapi.

Unakosea.
 
Na ngoja nikuelemishe kidogo, hakuna kitu kama kichaa cha mimba, hiko kitu mmetunga ili kujitetea, ni kwamba mwili kipindi cha mimba una produce hormones nyingi, hormones zina-affect mood and emotions, ndo maana mkiwa na mimba mnajikuta mpo moody sana, ila hio haimaanishi una kichaa au kicha cha mimba sijui, acha uongo.
😂😂😂 biologists in work......
 
Uliyosema hapo ni pure nonsense, kwann?
Unaposema kusaidia majukumu ya nyumbani, wanaume tunasaidia sana majukumu ya nyumbani sio tuu kukulisha wewe na watoto.
Talaka 80% are initiated by women kwa sababu zisingo za msingi, na sababu kubwa utakuta mwanaume kukwama kiuchumi na utakuta mwanamke hapo amejitapa anaingiza hela viela zaidi ya mumewe bac anamuona mumewe fala haiendani nae tena.

Haya tukija kweny ulemavu uliopatikana ndani ya ndoa, wanawake ndo wanaongoza kuachana na wanaume ambao wamepatwa na majanga/ajali na kuwa walemavu, hii inamaanisha nn kama sio kwamba tangia ulimwengu uumbwe mnajijali nyinyi tuu, a woman only cares about her own welfare, mbona kiwango kikubwa cha wanaume tunabaki kusaidiana majukumu na wake zetu wasiojiweza?

Tukizungmzia ukatili, upo both ways, system za maisha (ambazo kaweka mwanaume huyohuyo) zimemfanya mwanamke kuwa mtu ambaye yupo salama most of the time.

Mwanamke akitaka kutoa mimba kwasababu fulani mnasema "her body her choice" ila mwanaume akimwambia atoe mimba kwasababu hana child support mnaona mnanyanyaswa.

Wanaume wengi wametoa child support kwa watoto ambao sio wao, ikija kuwa proven kwamba hao watoto sio wao, kuna hatua yeyote inachukuliwa kwa huyo mwanamke, je refund ya child support kwa mtoto ambae sio wangu??

Wanaume wengi wapo jela kwa kusingiziwa ubakaji na wamepoteza miaka mingi ya maisha yao, ila wakitoka hao wanawake hawachukuliwi hatua yeyote.

We unadhani the judicial system iko sawa kwa both me and women??

Hakuna wanawake wanapiga wanaume zao?? Wewe ukienda mahakamani kwa kupigwa na mwanaume na mimi mwanamme nikienda mahakamani kwa kupigwa na mke wangu, we unadhani nani atasikilizwa mapema?? We unadhani nani atapewa adhabu kali??

Public Perception ni kitu kibaya sana.
Public Perception imemfanya mwanaume kuonekana kuwa kama mnyama mwenye roho mbaya anayemwonea mwanamke, wakati sio kweli, ukivamiwa na majambazi usiku nani hutoka na kutoa maisha yake kukulinda wewe na watoto?
Utakapo gombana na watu mtaani nani wa kwanza kuja kukusaidia??
Utakapo zimia/ishiwa nguvu ukiwa sehemu yeyote nani wa kwanza kuja kukuinua kukukimbiza hospitali?

Quite the contrary, wanawake hawajaanza kuwa walaghai leo au jana, tokea zamani hayo ni mambo yenu.
Mwanamke hana nguvu, kwaio njia pekee ya kupambana na mwanaume is through innuendo, gossip na reputation destruction, na huwaga hamchukuliwi hatua zozote za kisheria, mkianza kulialia mnasamehewa.

Ngoja niishie hapo kwa leo.
Kwanza kabisa ni wanaume gani hao unaowazungumzia ambao wanasaidia majukumu ya nyumbani au ndio hadi mke awe hoi kitandani, hawa hawa ambao ukiwaambia wasaidie wanasema "sasa nimeoa ili iweje" na mke akisema aweke housegirl unatembea naye kwa kisingizio cha kwamba mke kajisahau kazi zote kamuachia housegirl, kuhusu wanaume kutoka na kupambana na majambazi ni wanaume wangapi wanafanya hivyo siku hizi mbona cases nyingi tunazozisikia ni majambazi kuvamia nyumba na kuwacharanga mapanga familia nzima au wengine kubaka wanawake wanaowakuta humo

Kuhusu suala la mwanaume kuwa katili na kumuonea mwanamke wala siyo public perception ila ndio reality toka enzi na enzi ni vile tu siku hizi kuna sheria nyingi zinawalinda wanawake baada ya kuwa wameshanyanyasika sana miaka na miaka chini ya mfumo dume, bila shaka unafahamu kwamba zamani kulikuwa na mila na desturi nyingi zilizomkandamiza mwanamke ili tu kumnufaisha mwanaume hata utamaduni wa kukeketa wanawake lengo lilikuwa ni kumnufaisha mwanaume na si mwanamke, zamani binti akishaolewa hatakiwi kurudi nyumbani hata mume wake awe msaliti na mnyanyasaji kiasi gani mwanamke anatakiwa kuvumilia tu na akisema arudi kwao baba yake anamtimua kwa kisingizio cha kwamba ameshakula mahari hivyo binti akavumilie tu

Tukija kwenye suala la ngono na mahusiano jamii bado inampendelea mwanaume na kumuandama mwanamke ndio maana hata mwanaume na mwanamke wakizini anayetukanwa ni mwanamke tena kuna jamii hadi leo mwanamke ndio anauawa huku mwanaume akiachwa, mwanamke na mwanaume wakichelewa kuingia kwenye ndoa anayenyooshewa vidole ni mwanamke kwa kisingizio cha maumbile mwanamke na mwanaume wakizaa mtoto kisha wakaachana mwanamke ndiye anayesimangwa na kuitwa single mother, hizo gender stereotypes na brutal judgement kwa wanawake ambazo zililetwa na wanaume na zinapelekea wanawake kujiona unworthy na inferior mnajifanya hamzioni siku hizi ninyi ndio mmeamua kuplay victims na kuwa walalamikaji
 
Back
Top Bottom