KERO Baadhi ya Watoto wanasoma mpaka Saa 11 Jioni bila kula Wilayani ya Karagwe, hilo si jambo jema

KERO Baadhi ya Watoto wanasoma mpaka Saa 11 Jioni bila kula Wilayani ya Karagwe, hilo si jambo jema

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Jamani mimi kama mdau wa elimu kuna suala nimeliona na naomba lifike kwa mamlaka husika.

Ipo hivi baadhi ya Shule za Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera zinafundisha watoto kuanzia asubuhi mpaka jioni wakati huo mtoto hajanywa uji wala kula chakula cha mchana.

Katika kufatilia nimeambiwa baadhi ya watoto wanachanga chakula kupitia kwa wazazi au walezi wao, ila ambaye hajisikii kuchanga anaacha, hakuna juhudi zozote zinafanyika na wako comfortable na remedial zao.

Kwa hali ya kawaida mtoto huyo mwenye njaa anajifunza nini? Naomba Serikali iingilie kati.
 
Hivi ili swala la wanafunzi haliwezi kubebwa na mapato yatokanayo na halmashauri husika maana ni kero tunaimiza watoto wasome ila bado mazingira hayakai sawa na sio rafiki
 
Kuna tofauti kubwa kati ya elimu Bure na Elimu bila malipo ?

Kwaiyo wewe unataka Nini
Watoto watoke saa 8?
Watoto wale shule?
 
Back
Top Bottom