Tetesi: Baadhi ya watumishi wa umma hawajapata mshahara

Tetesi: Baadhi ya watumishi wa umma hawajapata mshahara

Umeingia kwa watu wote kwa mfumo mpya. Jaribu kuangalia tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaandika kwa kujiamini kana kwamba una uwezo wa kuangalia salio la account zote Tz, in short had jana jioni ni wachache sana walioingiziwa salary. Bank ya karibu yangu wala haikuwa na watu kama ilivyo desturi. Mimi binafsi sikuingiziwa labda leo.
 
Ni kweli asilimia kubwa ya wafanyakaz hawajaingiziwa mshahara sijui tatizo ni nin
 
Mhhhh,tupo wengi tusiopata mshahara...lakin vp mliopata kuna kilichoongezeka?
 
Mimi sio miongoni mwa wanaotarajia akaunt kusoma kutoka serikalini, huenda maelezo yangu yakawa sio sahihi.

Kwani wafanyakazi wote mna akaunt benki moja ambapo mishahara inapita? Kama ni benki tofautitofauti lazima mishahara ipishane muda au tarehe za kuwekewa kutokana na utaratibu wao wa kuchakata malipo. Pia kwa utaratibu mpya, sijui maelekezo/ malipo yanashughulikiwa na BoT au hazina wanapeleka orodha kwenye mabenki ambapo kuna akaunt za wafanyakazi.

Bado ni mapema mno kuwa na wasiwasi.

Vilevile huu ni wito kuanza kufikiria kuwa na vyanzo vingine vya kipato zaidi ya mshahara.
 
Mshahara umeingia toka jana na subiria mpaka leo mchana usipongia wasiliana na afisa utumishi wako. Kingine hakikisha taarifa zako za kibenki kwa maana majina yako sahihi na ya utumishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inaendelea kufanya kila liwezekanalo ili kufikia jumatatu tatizo liwe limekwisha,msiwe na wasiwasi ni swala la kiufundi na mfumo tu,mana utaratibu wa kuwalipa umebadilika.

Kuhusu nyongeza na promotions fikirieni nje ya box.
 
Back
Top Bottom