Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada, mama abaki analia akizunguka kuomba msaada

Unakuta hata uwezo wa kumpa mtoto milo miwili kwa siku hana.

Akirudishiwa mtoto anaanza kushindwa ustawi wa jamii kushinikiza baba wa mtoto ahudumie.

Kumbe anatakiwa amshinikize nani kutoa huduma?

Huwa mnafikiria nini mnapowajaza wanawake mimba?

Baba sio kupandikiza mbegu, ni pamoja na malezi ya hali na mali kwa mtoto.
 
Katika hali ambayo inaweza kuacha maswali mengi na mtazamo tofauti, mtoto Yusuph Issa Juma mwenye umri wa miaka 8, Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Istiqaama iliyopo Ilemela Jijini Mwanza amesafirishwa kwenda Nchini Canada bila ridhaa ya mama yake.

Mtoto huyo ameondoka katika mazingira tata akiongozana na Watanzania wawili wenye asili ya India, baada ya baba mzazi kutoa ruhusa huku mama mzazi akiwa hana taarifa.
View attachment 2701382

CHANZO CHA MKASA
Mama mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Khadija akiwa mfanyabishara maeneo ya Makoroboi, Mwanza, alianza kuzoeana na dada mwenye asili ya India anayefahamika kwa jina la Narina Haji Dawood.

Nariana alimpenda Yusuph kuanzia akiwa na umri wa mwaka mmoja, alipofikisha mwaka mmoja na nusu akawa anamuomba Khadija amchukue mtoto (Yusuph) akae kwake wakati yeye (mama mtu) akiendelea na biashara zake, Khadija hakupinga hilo.

Baadaye Narina akahamia Kiseke kutoka Makoroboi, akiwa huko akaomba akae na Yusuph na amsomeshe kwa makubaliano kuwa mama mtoto anaweza kwenda kumuona muda wowote na mtoto atakuwa anarudi kwa mama mzazi pindi anapopata nafasi.

MKASA UKAANZA
Baada ya kuishi na Yusuph kwa miaka kadhaa, Narina akaomba kwa mama mzazi ruhusa kuwa anataka kwenda likizo Canada aongozane na mtoto, Khadija akakataa ombi hilo.

Miezi kadhaa baadaye Narina akamjulisha Khadija kuwa ana mpango wa kuhamia Canada, akaomba aondoke na Yusuph, mama mzazi akashikilia msimamo wake wa kukataa ombi kwa mara nyingine.
View attachment 2701383

BABA MZAZI AKAANZA KUSHAWISHIWA
Baada ya kuona mama mzazi ameshikilia msimamo, ikabidi Narina aanze kumshawishi baba mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Issa Juma, wakaanza kumpoa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha.

Baada ya muda wakamshawishi kuwa wana mpango wa kwenda na mtoto Canada, ikabidi baba mtu afungue kesi Mahakamani ya kutaka akae na mtoto.

Inadaiwa Mahakama ikaagiza Mtoto Akaishi na baba, ndipo baba mtu akatumia nafasi hiyo kuanza kufanya mipango kwa kushirikiano na familia ya kina Narina kwa ajili ya mtoto kusafiri.

JINA LA MTOTO LABADILISHWA
Ili kufanikisha mtoto kusafiri ikabidi majina ya mbele ya Yusuph yabadilishwe, kutoka Yusuph Issa Juma na kuwa Yusuph Haji Dawood zikatengenezwa nyaraka zinazoonesha Narina amemuasili (adapt) Yusuph na nyaraka nyingine kadhaa kisha Julai 20, 2023 wakasafiri kuelekeza Canada huku mama mtu akiwa ajui kinachoendelea.

BABA AELEZEA
Issa Juma alipoulizwa amesema “Kweli mtoto ameondoka kwenda Canada, familia iliyomchukua imesema itamsomesha, mimi sina kazi ya maana, nauza maziwa tu mtaani na sina uwezo wa kumsomesha, ni kweli pia uamuzi wa kuondoka kwa mtoto umefanywa kwa upande mmoja.

“Mzazi mwenzangu hakukubali uamuzi huo, tumeshazungumza na Ustawi wa Jamii na Uhamiaji kuhusu hili, msimamo wa mama mtoto ni kuwa anataka mtoto arudi.

“Familia iliyomchukua nimewasiliana nao, mtoto yuko salama na wameahidi kuwa watakuwa wanamrejesha kila baada ya miaka miwili kuja kusalimia.

“Ni kweli pia majina ya mbele yamebadilishwa ili kule anapokwenda ionekane kuna uhusiano kati yao.

“Huyo dada aliyemchukua mtoto hajaolewa wala hana mtoto wa kumzaa, anaishi yeye na kaka yake.”

BABA ASEMA YUPO TAYARI MTOTO ARUDISHWE
“Kwa hiki kinachoendelea, sikuzoea kuishi kwa wasiwasi, kama itawezekana basi wamrudishe tu mtoto, sina nia mbaya ndio maana nazungumza kwa uwazi.

“Maisha yangu ni magumu na sio kwamba nimemuuza mtoto kama inavyosemwa, zaidi nilipewa kompyuta tu, sio kweli kuwa nimepewa nyumba na gari, hiyo nyumba inayosemwa ameachiwa Mzee Felix ambaye ni mtu wa karibu na familia hiyo ya hao Wahindi.”

MAMA WA MTOTO AANGUA KILIO
Akizungumza huku analia, Khadija anasema “Ninachotaka mtoto wangu arudi, niliiachia hiyo familia imlee kwa kuwa waliomba na wakasema watamlipia ada lakini sikutaka waende naye nje ya nchi, nilimwambia msaada wowote anaotaka kwa mtoto autoe akiwa hapa Nchini.

“Nimeshaenda Ustawi wa Jamii, Polisi na Uhamiaji kote sijapata msaada, kwa sasa nipo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ili kutafuta msaada zaidi.”

MAELEZO YA AFISA ELIMU
Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Ilemela, Marco Busungu anasema: Hayo masuala ya Wanandoa sisi tumesumbuka nayo sana, mimi siwezi kulisemea hilo kwa kuwa sijapata taarifa, pia hata kama lingefika tungeangalia ametoroshwa akishwa shuleni au nyumbani? Kwa kuwa baba mzazi yupo na anahusika basi aulizwe yeye kwa kuwa anajua kinachoendelea.

MAELEZO YA AFISA USTAWI WA JAMII
Afisa wa Ustawi wa Jamii, Edith Ngowi anasema: Hili suala halikuwa la kwetu, Khadija alikuja kupata ufafanuzi, huku ni Ustawi wa Jamii Nyamagana na suala lake lipo Ilemela, hivyo tulichofanya sisi ni kumshauri na kumsindikisha kwenda Polisi.

Tukiwa Polisi tukashauriwa kwenda Uhamiaji, tulipoenda Uhamiaji tulioneshwa taratibu zote zimefuatwa na baba mtu akakiri alidanganya ili upatikane uhalali wa mtoto kusafiri.

Lengo lake lilikuwa mtoto apate kuasiliwa na aende akasomeshwe, tumeshauri familia ikae pamoja na Wazazi wa pande zote kuangalia jinsi ya kulimaliza nak ama ni kumrejesha mtoto wafanye hivyo.

UHAMIAJI MWANZA WAULIZWA
Alipoulizwa Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Peter Mbaku juu ya kudaiwa kuchezewa kwa nyaraka za mtoto na hadi kubadilishwa kwa jina kisha kuruhusiwa kwenda Canada, amesema: “Naomba muda nifuatilia hizo taarifa.”

SHULE YA ISTIQAAMA YAULIZWA
Alipotafutwa Kiongozi wa Shule ya Msingi Istiqaama, Rashid Seif Said kisha kuulizwa kuhusu taarifa za mwanafunzi huyo kwamba aliondokaje shuleni na kama alipewa ruhusa au kama wanajua kuhusu safari husika, aliomba jina na taarifa zingine za Mwanafunzi kabla ya kutoa majibu, alipotafutwa baadaye simu haikupokelewa.
huyo mtoto ameenda kwenye neema, mama aache ujinga. uzuri anajulikana amechukuliwa na nani, na mtu aliyekuwa anaishi naye kabla, atasoma shule nzuri atatafuta maisha na atamhamisha mamake huko ilemela na kwenda kuishi pazuri. baba amefanya la maana. kama walishamgawa kwa hao wahindi wa kitanzania tangu akiwa mdogo, shida ni nini kuondoka naye?
 
Sheria ya mtoto lengo lake ni kumnufaisha mtoto. Nobody else counts.
 
Watanzania uchawi ni asili yetu, yani umaskini walionao Wazazi hawaridhiki mpaka mtoto naye arithi dhiki?

Kwa ninavyojuwa Mimi hapo kuna proper communication na huyo muhusika kwa Mimi binafsi sioni tatizo kabisa, kwa asiyeelewa vizuri mambo haya hawezi kuelewa na atamlaumu baba.

Lakini kwa maoni yangu baba amefanya uwamuzi wa busara kabisa kumpa kibali huyo muhindi na ameahidi mtoto atakuwa anarudi kwa Wazazi wake, na isitoshe huyo mtoto anakwenda kuwa RAIA wa Canada na amesoma Canada atakuja kuokowa ndugu zake mbele ya safari.
Hizi PhD za mchongo ni janga kwa Taifa.

Kwamba huoni shida kwa mtoto kuasiliwa huku mama akiwa hajui na kwa umri mtoto huoni shida kwamba baadaye anaweza kujazwa sumu juu ya wazazi wake? Kwamba kwenu mkiwa maskini na akatokea tajiri anataka kununua watoto wenu utakubali kiroho safi kisa mwanao asirithi umasikini? Una uhakika gani na uwezo kiuchumi wa hiyo familia iliyomuasili huko kwao ukoje? Au ndio walewale wanaoamini kila anauetokea ulaya na marekani basi ni tajiri? Umewaza kuhusu usalama wa mtoto?
 
Point yangu ni kwamba huyo mtoto huko alikopelekwa ni kweli anapelekwa kusoma au kuna mengine?.Km walimpeleka kwa nia njema kwanini walimbadilishia majina?.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
Kama huna exposure yeyote ya kuishi ulaya au America mambo mengine kwako ni usiku wa Giza.

Huyo waziri wenu wa fedha Mwigulu Nchemba unayajuwa majina yake halisi? Je huyo Hamisi Kigwangwalah unayajuwa majina yake halisi?

Tundu Lisu na Alluthe Mughwai ni ndugu baba mmoja na mama mmoja ni kwa nini hawafanani majina?

Stupid (in Samia voice )
 
Sasa upweke na kumtia mtoto dhiki na umaskini vina faida gani?

Kwanza huyu muhindi wakikaa naye vizuri kutuma tickets na viza document kwa mama mzazi wala siyo issue, anakwenda Canada mwezi mmoja anafuta tongotongo anarudi Mwanza kula mapanki.
Inawezekana hana uwezo wa kuzaa , ni sawa, ila Shida yote ya nini, si aende hospitali kuna watoto wametelekezwa huko akachukue mmoja alee? Kwani lazima huyo ambae wazazi wapo?
 
Huna huelewa wa haya mambo kwa wenzetu hasa wale wanawake ambao hawajazaa wana mapenzi ya dhati na Watoto.

Akiadapt mtoto ujuwe mtoto amekula maisha na ndio anamuandikisha kama mrithi wake kwenye life insurance.

Mtoto wa rafiki yangu yupo Marekani kwa style kama hii ya adaption na sasa hivi ni RAIA na ndio amemaliza mafunzo kwenye Jeshi la Marekani na uzuri Baba yake pia yupo Marekani kwa mambo yake kitambo tu.
Huyo muhindi tuseme hakuwahi ona wahindi wenzake
 
Na ndo hicho muhindi keshaona nyota hapo, watoto zao wenyewe wakuwazaa wanawageuza mandondocha wanawaweka store duka lipate wateja
Karne hii mnaamini haya mambo. Babu zako si wangeyatumia kuwaandoa Wakoloni..
 
Watanzania uchawi ni asili yetu, yani umaskini walionao Wazazi hawaridhiki mpaka mtoto naye arithi dhiki?

Kwa ninavyojuwa Mimi hapo kuna proper communication na huyo muhusika kwa Mimi binafsi sioni tatizo kabisa, kwa asiyeelewa vizuri mambo haya hawezi kuelewa na atamlaumu baba.

Lakini kwa maoni yangu baba amefanya uwamuzi wa busara kabisa kumpa kibali huyo muhindi na ameahidi mtoto atakuwa anarudi kwa Wazazi wake, na isitoshe huyo mtoto anakwenda kuwa RAIA wa Canada na amesoma Canada atakuja kuokowa ndugu zake mbele ya safari.
Ili mradi wasimbadilishe Jinsia Kama yule Mtoto wa Malawi aliyechukuliwa na Madona! Let us hope for the best for him!!
 
Kama huna exposure yeyote ya kuishi ulaya au America mambo mengine kwako ni usiku wa Giza.

Huyo waziri wenu wa fedha Mwigulu Nchemba unayajuwa majina yake halisi? Je huyo Hamisi Kigwangwalah unayajuwa majina yake halisi?

Tundu Lisu na Alluthe Mughwai ni ndugu baba mmoja na mama mmoja ni kwa nini hawafanani majina?

Stupid (in Samia voice )
Wewe inabidi uchunguzwe,ukute ndio unajishughulisha na biashara ya human trafficking
 
Mambo mengine haya ni ya kuelewana tu mbona mtoto akisoma nje akija kusaidia wazazi ni nzuri zaidi..
Sema ile Bond ya Mzazi na Mtoto inakua haipo,na Mtoto anaweza hata asikujali kwa lolote lile na akawa ame bond sana na mlezi wake!!
 
Sijui mnaonaje hili Mimi ni Baba kukaa na wanangu mbali ni Mwiko.Kama kupambana wacha nipambane mimi wao wawe na Maisha mazuri,sio kutafuta shortcut,Haya Ndio tunekataa Dp World kuja kuchukua vyetu muda usio eleweka.Mtoto ananyanyasika huko aanze kuwalaani akawe Mtumwa wa watu nchi za kigeni.
Unaweza kupambana na bado maiaha yasiwe mazuri. Km kuna tobo la shortcut bora ulitumie kuliko uje ujute.
 
Back
Top Bottom