Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada, mama abaki analia akizunguka kuomba msaada

Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada, mama abaki analia akizunguka kuomba msaada

Hapa hakuna shida yoyote ila kama mjuavyo kawaida ya wabongo ni kukuza mambo.
acha mtoto akasome elimu bora na kupata maisha bora.
kamwe mwenye asili haachi asili yake.
baba wa mtoto ana busara ndio maana ameamua kuluzungumzia suala hili kwa uwazi bila kuficha hata nukta.
MWacheni mtoto akale maisha canada
 
Yaani mijitu iko serious inajikuta imeelimika na kustaarabika inatetea upumbavu kama huu,
Ingieni labor ndo mtajua thamani ya mtoto, eti 'atakuja kuisaidia familia' , mama anayejua thamani ya mtoto hawezi kufanya huo upuuzi bora afe na umaskini wake, halafu riziki haipo mikononi mwa muhindi riziki popote.
Eti ushamba sijui umaskini nyie mnaotetea ndo washamba na maskini wa roho hata kama mna za kubadilishia mboga
 
Huyo mtoto ndio mrithi wa benefit zote za huyo muhindi in case amefariki.

Yani ukisikia wanaadapt mume unitonye tu.
Nahisi huyu dada hana uwelewa huo, hajui kwamba hiyo ndio njia moja wapo ya kuuaga umasikini.
Hha kuu unataka kuadaptiwa, mbona yapo majimama na yanajitokezaga yanatafuta wanaume wa kuwaleleka nje huko kazi ni moja tu "kumfurahisha" mengine kuhusu maisha anashugurikia yeye😃😃
 
Yaani mijitu iko serious inajikuta imeelimika na kustaarabika inatetea upumbavu kama huu,
Ingieni labor ndo mtajua thamani ya mtoto, eti 'atakuja kuisaidia familia' , mama anayejua thamani ya mtoto hawezi kufanya huo upuuzi bora afe na umaskini wake, halafu riziki haipo mikononi mwa muhindi riziki popote.
Eti ushamba sijui umaskini nyie mnaotetea ndo washamba na maskini wa roho hata kama mna za kubadilishia mboga
Na hawa wanaotupa vichanga vyao huwa wametoka TLP?

Hovyo, yani unadhani sisi siyo Wazazi?

Ndio maana umaskini hautakaa uishe Tanzania maana kuna umaskini unawapendeza sana.
 
Kama umesoma hiyo story utakuwa umeelewa vizuri, nia ni njema kabisa na kwa wanaojuwa mchakato wa kuasili mtoto Tanzania si mchakato wa kitoto kama wengi wanavyodhani, wangeshachukuliwa wengi tu kwenye vituo vya Watoto yatima.
Kwenye hili suala huyo mwenye mtoto angetumia akili kuliko hisia kwa wakati huu
Mtoto ameota mpaka kitambi asubiri arudishiwe akakae nae makoroboi
 
Nahisi huyu dada hana uwelewa huo, hajui kwamba hiyo ndio njia moja wapo ya kuuaga umasikini.
Hha kuu unataka kuadaptiwa, mbona yapo majimama na yanajitokezaga yanatafuta wanaume wa kuwaleleka nje huko kazi ni moja tu "kumfurahisha" mengine kuhusu maisha anashugurikia yeye😃😃
Tangu lini muhindi amkapenda muafrika?
Kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia ,huyo dada achunguzwe .
 
Wengi hua hawaelewi na kikubwa mtoto atakua na future nzuri tena nchi yenyewe canada, huyo mama atulie tu dogo atakuja kumlaumu baadae akijua mama alizingua
Huyu dogo akiambiwa anarudi mazima naamini atalia mpka kitambi kitayeyuka
 
Yaani mijitu iko serious inajikuta imeelimika na kustaarabika inatetea upumbavu kama huu,
Ingieni labor ndo mtajua thamani ya mtoto, eti 'atakuja kuisaidia familia' , mama anayejua thamani ya mtoto hawezi kufanya huo upuuzi bora afe na umaskini wake, halafu riziki haipo mikononi mwa muhindi riziki popote.
Eti ushamba sijui umaskini nyie mnaotetea ndo washamba na maskini wa roho hata kama mna za kubadilishia mboga
Hakuna Cha labour ,usituaminishe uongo ambao hamunyi .umezungumza Kwa mtazamo wa aina Moja kana kwamba wanawake wote waliozaaa Wana uchungu na watoto na kitu ambacho hakipo
Just imagine na wewe jiulize
1. Ni mara ngapi watu wanapenda labour Bado mtu anadumbukiza mtt chooni
2.ni mara ngapi mwanamke anamfanyia mtoto matendo ya kikatili
3. Binadam usimuamini kama uwazavyo

Anaweza akaongea uongo au asiongee uongo
 
Ona akili za maskini zinavyowaza, mnaelewa procedures za kuadapt mtoto Tanzania?
Wewe akili yako inawaza pesa tu Wala huwazi upendo wa mzazi kwa mwanae? Mtoto bado mdogo tena inaweza ukakuta wana mtoto huyo tu pekee.

Kwa akili zako za kijinga umewaza pesa tu, si ajabu ingekuwa wewe ungeombwa hata MATAKO ungetoa tu.
 
Na hawa wanaotupa vichanga vyao huwa wametoka TLP?

Hovyo, yani unadhani sisi siyo Wazazi?

Ndio maana umaskini hautakaa uishe Tanzania maana kuna umaskini unawapendeza sana.
Umasikini haumalizwi kihivyo sema we ndo unamawazo ya kimaskini afu muoga wa maisha. Uza wanao kama kweli unao
Wangapi wamelala chumba kimoja na mbuzi, kuku na saivi wametusua maisha, kusikia canada ndo unaona kutoboa wangapi wameenda huko wamerudi mateja wengine mashoga, baki na ujinga wako usinishirikishe.
Mwanaume kamili anayejiamini mwenye mbegu zake na mwenye imani hawezi fanya huo uduanzi, labda bwabwa tu anaweza kuwa na mawazo mgando hivyo
 
Tangu lini muhindi amkapenda muafrika?
Kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia ,huyo dada achunguzwe .
Inategemea mkuu, wataka kuniambia hilo jambo alilolitaka kulitelekeza ni tangia mtoto akiwa na mwaka mmoja akamkuza mpaka umri wa miaka 7 ndio atimize mission yake baada ya muda wote huo? Actually mhindi anamtaka mtoto kwasababu hana mtoto, hajawahi kuzaa maisha yake yote na wala hana mwanaume
 
Huyu dogo akiambiwa anarudi mazima naamini atalia mpka kitambi kitayeyuka
Hawezi kurudi, Canada ndio Nyumbani kwa human Rights.

Kuna mwaka walileta ndege kubwa Tanzania ikawachukuwa wakimbizi wengi sana wa Burundi makambini na kuwapeleka Canada.

Huyo muhindi ana haki zote za kisheria kumlea huyo mtoto, na wazungu huwezi kuwaconvice eti Canada na Tanzania huyo mtoto atapata matunzo na elimu bora Tanzania.

Imeenda hiyo.
 
Hakuna Cha labour ,usituaminishe uongo ambao hamunyi .umezungumza Kwa mtazamo wa aina Moja kana kwamba wanawake wote waliozaaa Wana uchungu na watoto na kitu ambacho hakipo
Just imagine na wewe jiulize
1. Ni mara ngapi watu wanapenda labour Bado mtu anadumbukiza mtt chooni
2.ni mara ngapi mwanamke anamfanyia mtoto matendo ya kikatili
3. Binadam usimuamini kama uwazavyo

Anaweza akaongea uongo au asiongee uongo
Hao wanawake wanaofanya hivyo mara nyingi ni ugumu wa maisha na amekimbiwa na mumewe na hajui atamlisha nini huyo mtoto.
 
Katika hali ambayo inaweza kuacha maswali mengi na mtazamo tofauti, mtoto Yusuph Issa Juma mwenye umri wa miaka 8, Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Istiqaama iliyopo Ilemela Jijini Mwanza amesafirishwa kwenda Nchini Canada bila ridhaa ya mama yake.

Mtoto huyo ameondoka katika mazingira tata akiongozana na Watanzania wawili wenye asili ya India, baada ya baba mzazi kutoa ruhusa huku mama mzazi akiwa hana taarifa.
View attachment 2701382

CHANZO CHA MKASA
Mama mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Khadija akiwa mfanyabishara maeneo ya Makoroboi, Mwanza, alianza kuzoeana na dada mwenye asili ya India anayefahamika kwa jina la Narina Haji Dawood.

Nariana alimpenda Yusuph kuanzia akiwa na umri wa mwaka mmoja, alipofikisha mwaka mmoja na nusu akawa anamuomba Khadija amchukue mtoto (Yusuph) akae kwake wakati yeye (mama mtu) akiendelea na biashara zake, Khadija hakupinga hilo.

Baadaye Narina akahamia Kiseke kutoka Makoroboi, akiwa huko akaomba akae na Yusuph na amsomeshe kwa makubaliano kuwa mama mtoto anaweza kwenda kumuona muda wowote na mtoto atakuwa anarudi kwa mama mzazi pindi anapopata nafasi.

MKASA UKAANZA
Baada ya kuishi na Yusuph kwa miaka kadhaa, Narina akaomba kwa mama mzazi ruhusa kuwa anataka kwenda likizo Canada aongozane na mtoto, Khadija akakataa ombi hilo.

Miezi kadhaa baadaye Narina akamjulisha Khadija kuwa ana mpango wa kuhamia Canada, akaomba aondoke na Yusuph, mama mzazi akashikilia msimamo wake wa kukataa ombi kwa mara nyingine.
View attachment 2701383

BABA MZAZI AKAANZA KUSHAWISHIWA
Baada ya kuona mama mzazi ameshikilia msimamo, ikabidi Narina aanze kumshawishi baba mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Issa Juma, wakaanza kumpoa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha.

Baada ya muda wakamshawishi kuwa wana mpango wa kwenda na mtoto Canada, ikabidi baba mtu afungue kesi Mahakamani ya kutaka akae na mtoto.

Inadaiwa Mahakama ikaagiza Mtoto Akaishi na baba, ndipo baba mtu akatumia nafasi hiyo kuanza kufanya mipango kwa kushirikiano na familia ya kina Narina kwa ajili ya mtoto kusafiri.

JINA LA MTOTO LABADILISHWA
Ili kufanikisha mtoto kusafiri ikabidi majina ya mbele ya Yusuph yabadilishwe, kutoka Yusuph Issa Juma na kuwa Yusuph Haji Dawood zikatengenezwa nyaraka zinazoonesha Narina amemuasili (adapt) Yusuph na nyaraka nyingine kadhaa kisha Julai 20, 2023 wakasafiri kuelekeza Canada huku mama mtu akiwa ajui kinachoendelea.

BABA AELEZEA
Issa Juma alipoulizwa amesema “Kweli mtoto ameondoka kwenda Canada, familia iliyomchukua imesema itamsomesha, mimi sina kazi ya maana, nauza maziwa tu mtaani na sina uwezo wa kumsomesha, ni kweli pia uamuzi wa kuondoka kwa mtoto umefanywa kwa upande mmoja.

“Mzazi mwenzangu hakukubali uamuzi huo, tumeshazungumza na Ustawi wa Jamii na Uhamiaji kuhusu hili, msimamo wa mama mtoto ni kuwa anataka mtoto arudi.

“Familia iliyomchukua nimewasiliana nao, mtoto yuko salama na wameahidi kuwa watakuwa wanamrejesha kila baada ya miaka miwili kuja kusalimia.

“Ni kweli pia majina ya mbele yamebadilishwa ili kule anapokwenda ionekane kuna uhusiano kati yao.

“Huyo dada aliyemchukua mtoto hajaolewa wala hana mtoto wa kumzaa, anaishi yeye na kaka yake.”

BABA ASEMA YUPO TAYARI MTOTO ARUDISHWE
“Kwa hiki kinachoendelea, sikuzoea kuishi kwa wasiwasi, kama itawezekana basi wamrudishe tu mtoto, sina nia mbaya ndio maana nazungumza kwa uwazi.

“Maisha yangu ni magumu na sio kwamba nimemuuza mtoto kama inavyosemwa, zaidi nilipewa kompyuta tu, sio kweli kuwa nimepewa nyumba na gari, hiyo nyumba inayosemwa ameachiwa Mzee Felix ambaye ni mtu wa karibu na familia hiyo ya hao Wahindi.”

MAMA WA MTOTO AANGUA KILIO
Akizungumza huku analia, Khadija anasema “Ninachotaka mtoto wangu arudi, niliiachia hiyo familia imlee kwa kuwa waliomba na wakasema watamlipia ada lakini sikutaka waende naye nje ya nchi, nilimwambia msaada wowote anaotaka kwa mtoto autoe akiwa hapa Nchini.

“Nimeshaenda Ustawi wa Jamii, Polisi na Uhamiaji kote sijapata msaada, kwa sasa nipo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ili kutafuta msaada zaidi.”

MAELEZO YA AFISA ELIMU
Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Ilemela, Marco Busungu anasema: Hayo masuala ya Wanandoa sisi tumesumbuka nayo sana, mimi siwezi kulisemea hilo kwa kuwa sijapata taarifa, pia hata kama lingefika tungeangalia ametoroshwa akishwa shuleni au nyumbani? Kwa kuwa baba mzazi yupo na anahusika basi aulizwe yeye kwa kuwa anajua kinachoendelea.

MAELEZO YA AFISA USTAWI WA JAMII
Afisa wa Ustawi wa Jamii, Edith Ngowi anasema “Khadija alikuja kupata ufafanuzi, tulimsindikiza Polisi, tukashauriwa kwenda Uhamiaji, tulipoenda tulioneshwa taratibu zote zimefuatwa na baba mtu akakiri alidanganya ili upatikane uhalali wa mtoto kusafiri.

Lengo lake lilikuwa mtoto apate kuasiliwa na aende akasomeshwe, tumeshauri familia ikae pamoja na Wazazi wa pande zote kuangalia jinsi ya kulimaliza nak ama ni kumrejesha mtoto wafanye hivyo.

UHAMIAJI MWANZA WAULIZWA
Alipoulizwa Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Peter Mbaku juu ya kudaiwa kuchezewa kwa nyaraka za mtoto na hadi kubadilishwa kwa jina kisha kuruhusiwa kwenda Canada, amesema: “Naomba muda nifuatilia hizo taarifa.”
Naona hapo mmoja wa wazazi ametumia mihemko badala ya kutumia hekima. Wazazi useless.
 
Back
Top Bottom