Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada, mama abaki analia akizunguka kuomba msaada

Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada, mama abaki analia akizunguka kuomba msaada

Ona akili za maskini zinavyowaza, mnaelewa procedures za kuadapt mtoto Tanzania?
We ndo una akili za kimaskini afu muoga wa maisha usitulishe maneno, kuadapt mtoto si aende vituo vya watoto yatima mbona vimejaa tele, watoto wa mitaani wasio na pakula wala kulala unataka kusema hawaoni.
Dunia ni zaidi ya uijuavyo hizo unazoziita akili za kimaskini ndo matajiri wanazitumia ku'make' kaa kwenye password
 
We ndo una akili za kimaskini afu muoga wa maisha usitulishe maneno, kuadapt mtoto si aende vituo vya watoto yatima mbona vimejaa tele, watoto wa mitaani wasio na pakula wala kulala unataka kusema hawaoni.
Dunia ni zaidi ya uijuavyo hizo unazoziita akili za kimaskini ndo matajiri wanazitumia ku'make' kaa kwenye password
Kwahiyo kwa akili zako za kuvukia barabara Watoto yatima ndio sahihi watolewe kwenda kufanyiwa makafara?
 
Hakuna Cha labour ,usituaminishe uongo ambao hamunyi .umezungumza Kwa mtazamo wa aina Moja kana kwamba wanawake wote waliozaaa Wana uchungu na watoto na kitu ambacho hakipo
Just imagine na wewe jiulize
1. Ni mara ngapi watu wanapenda labour Bado mtu anadumbukiza mtt chooni
2.ni mara ngapi mwanamke anamfanyia mtoto matendo ya kikatili
3. Binadam usimuamini kama uwazavyo


Anaweza akaongea uongo au asiongee uongo
We ni pimb*, nini hao unaowazungumzia ni kweli wapo ila hatuwaongelei hao tunamungelea mama wa Mwanza anayehangaika kumrudisha nyumbani mwanae baada ya kuporwa na wapuuzi wakishirikiana na baba lisiloijua labor lenye akili mgando linalodhani Canada ni peponi na muhindi ndio malaika wa riziki
 
Huyo mama msukuma aache umbiwga mtoto akikua mkubwa akajua alimkazia jwenda canada atamtukana mitusi ya nguoni mtoto anaenda kula maisha.
Nampa big up babalai wa mtoto bongo kama mzimuni
 
Katika hali ambayo inaweza kuacha maswali mengi na mtazamo tofauti, mtoto Yusuph Issa Juma mwenye umri wa miaka 8, Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Istiqaama iliyopo Ilemela Jijini Mwanza amesafirishwa kwenda Nchini Canada bila ridhaa ya mama yake.

Mtoto huyo ameondoka katika mazingira tata akiongozana na Watanzania wawili wenye asili ya India, baada ya baba mzazi kutoa ruhusa huku mama mzazi akiwa hana taarifa.
View attachment 2701382

CHANZO CHA MKASA
Mama mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Khadija akiwa mfanyabishara maeneo ya Makoroboi, Mwanza, alianza kuzoeana na dada mwenye asili ya India anayefahamika kwa jina la Narina Haji Dawood.

Nariana alimpenda Yusuph kuanzia akiwa na umri wa mwaka mmoja, alipofikisha mwaka mmoja na nusu akawa anamuomba Khadija amchukue mtoto (Yusuph) akae kwake wakati yeye (mama mtu) akiendelea na biashara zake, Khadija hakupinga hilo.

Baadaye Narina akahamia Kiseke kutoka Makoroboi, akiwa huko akaomba akae na Yusuph na amsomeshe kwa makubaliano kuwa mama mtoto anaweza kwenda kumuona muda wowote na mtoto atakuwa anarudi kwa mama mzazi pindi anapopata nafasi.

MKASA UKAANZA
Baada ya kuishi na Yusuph kwa miaka kadhaa, Narina akaomba kwa mama mzazi ruhusa kuwa anataka kwenda likizo Canada aongozane na mtoto, Khadija akakataa ombi hilo.

Miezi kadhaa baadaye Narina akamjulisha Khadija kuwa ana mpango wa kuhamia Canada, akaomba aondoke na Yusuph, mama mzazi akashikilia msimamo wake wa kukataa ombi kwa mara nyingine.
View attachment 2701383

BABA MZAZI AKAANZA KUSHAWISHIWA
Baada ya kuona mama mzazi ameshikilia msimamo, ikabidi Narina aanze kumshawishi baba mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Issa Juma, wakaanza kumpoa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha.

Baada ya muda wakamshawishi kuwa wana mpango wa kwenda na mtoto Canada, ikabidi baba mtu afungue kesi Mahakamani ya kutaka akae na mtoto.

Inadaiwa Mahakama ikaagiza Mtoto Akaishi na baba, ndipo baba mtu akatumia nafasi hiyo kuanza kufanya mipango kwa kushirikiano na familia ya kina Narina kwa ajili ya mtoto kusafiri.

JINA LA MTOTO LABADILISHWA
Ili kufanikisha mtoto kusafiri ikabidi majina ya mbele ya Yusuph yabadilishwe, kutoka Yusuph Issa Juma na kuwa Yusuph Haji Dawood zikatengenezwa nyaraka zinazoonesha Narina amemuasili (adapt) Yusuph na nyaraka nyingine kadhaa kisha Julai 20, 2023 wakasafiri kuelekeza Canada huku mama mtu akiwa ajui kinachoendelea.

BABA AELEZEA
Issa Juma alipoulizwa amesema “Kweli mtoto ameondoka kwenda Canada, familia iliyomchukua imesema itamsomesha, mimi sina kazi ya maana, nauza maziwa tu mtaani na sina uwezo wa kumsomesha, ni kweli pia uamuzi wa kuondoka kwa mtoto umefanywa kwa upande mmoja.

“Mzazi mwenzangu hakukubali uamuzi huo, tumeshazungumza na Ustawi wa Jamii na Uhamiaji kuhusu hili, msimamo wa mama mtoto ni kuwa anataka mtoto arudi.

“Familia iliyomchukua nimewasiliana nao, mtoto yuko salama na wameahidi kuwa watakuwa wanamrejesha kila baada ya miaka miwili kuja kusalimia.

“Ni kweli pia majina ya mbele yamebadilishwa ili kule anapokwenda ionekane kuna uhusiano kati yao.

“Huyo dada aliyemchukua mtoto hajaolewa wala hana mtoto wa kumzaa, anaishi yeye na kaka yake.”

BABA ASEMA YUPO TAYARI MTOTO ARUDISHWE
“Kwa hiki kinachoendelea, sikuzoea kuishi kwa wasiwasi, kama itawezekana basi wamrudishe tu mtoto, sina nia mbaya ndio maana nazungumza kwa uwazi.

“Maisha yangu ni magumu na sio kwamba nimemuuza mtoto kama inavyosemwa, zaidi nilipewa kompyuta tu, sio kweli kuwa nimepewa nyumba na gari, hiyo nyumba inayosemwa ameachiwa Mzee Felix ambaye ni mtu wa karibu na familia hiyo ya hao Wahindi.”

MAMA WA MTOTO AANGUA KILIO
Akizungumza huku analia, Khadija anasema “Ninachotaka mtoto wangu arudi, niliiachia hiyo familia imlee kwa kuwa waliomba na wakasema watamlipia ada lakini sikutaka waende naye nje ya nchi, nilimwambia msaada wowote anaotaka kwa mtoto autoe akiwa hapa Nchini.

“Nimeshaenda Ustawi wa Jamii, Polisi na Uhamiaji kote sijapata msaada, kwa sasa nipo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ili kutafuta msaada zaidi.”

MAELEZO YA AFISA ELIMU
Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Ilemela, Marco Busungu anasema: Hayo masuala ya Wanandoa sisi tumesumbuka nayo sana, mimi siwezi kulisemea hilo kwa kuwa sijapata taarifa, pia hata kama lingefika tungeangalia ametoroshwa akishwa shuleni au nyumbani? Kwa kuwa baba mzazi yupo na anahusika basi aulizwe yeye kwa kuwa anajua kinachoendelea.

MAELEZO YA AFISA USTAWI WA JAMII
Afisa wa Ustawi wa Jamii, Edith Ngowi anasema “Khadija alikuja kupata ufafanuzi, tulimsindikiza Polisi, tukashauriwa kwenda Uhamiaji, tulipoenda tulioneshwa taratibu zote zimefuatwa na baba mtu akakiri alidanganya ili upatikane uhalali wa mtoto kusafiri.

Lengo lake lilikuwa mtoto apate kuasiliwa na aende akasomeshwe, tumeshauri familia ikae pamoja na Wazazi wa pande zote kuangalia jinsi ya kulimaliza nak ama ni kumrejesha mtoto wafanye hivyo.

UHAMIAJI MWANZA WAULIZWA
Alipoulizwa Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Peter Mbaku juu ya kudaiwa kuchezewa kwa nyaraka za mtoto na hadi kubadilishwa kwa jina kisha kuruhusiwa kwenda Canada, amesema: “Naomba muda nifuatilia hizo taarifa.”
Wewe mleta mada inaonesha unawajuwa hawa watu.


Mwacheni huyo mtoto, kishapata maisha mema, mshaurini vizuri huyo mama. Awe na contacts zao tu, asiwe na wasiwasi, huyo ni mkubwa hatowasahau wazazi wake na alipotoka. Hiyo ni fursa ambayo wengi wanaitafuta.
 
Watanzania uchawi ni asili yetu, yani umaskini walionao Wazazi hawaridhiki mpaka mtoto naye arithi dhiki?

Kwa ninavyojuwa Mimi hapo kuna proper communication na huyo muhusika kwa Mimi binafsi sioni tatizo kabisa, kwa asiyeelewa vizuri mambo haya hawezi kuelewa na atamlaumu baba.

Lakini kwa maoni yangu baba amefanya uwamuzi wa busara kabisa kumpa kibali huyo muhindi na ameahidi mtoto atakuwa anarudi kwa Wazazi wake, na isitoshe huyo mtoto anakwenda kuwa RAIA wa Canada na amesoma Canada atakuja kuokowa ndugu zake mbele ya safari.
Wewe angekuwa wa kwako ungempa aende nae???

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
ujamaa ulifanya wazaz na watanzania kuwa mataahira
mm mchaw mama mzaz tambo ningekua raiya norway nikiwq kwetu umeruni mzungu alinitaka kwq kipaj cha ngumi. mama mzaz anasema soma umalize utafute kaz. matokeo yake nabeba tofari saiti na erim ra saba
 
Yaani mijitu iko serious inajikuta imeelimika na kustaarabika inatetea upumbavu kama huu,
Ingieni labor ndo mtajua thamani ya mtoto, eti 'atakuja kuisaidia familia' , mama anayejua thamani ya mtoto hawezi kufanya huo upuuzi bora afe na umaskini wake, halafu riziki haipo mikononi mwa muhindi riziki popote.
Eti ushamba sijui umaskini nyie mnaotetea ndo washamba na maskini wa roho hata kama mna za kubadilishia mboga
Kama labor ingekuwa na thamani kiasi hicho basi kusingekuwa na watoto wa mitaani na watoto kutupwa
 
Huna huelewa wa haya mambo kwa wenzetu hasa wale wanawake ambao hawajazaa wana mapenzi ya dhati na Watoto.

Akiadapt mtoto ujuwe mtoto amekula maisha na ndio anamuandikisha kama mrithi wake kwenye life insurance.

Mtoto wa rafiki yangu yupo Marekani kwa style kama hii ya adaption na sasa hivi ni RAIA na ndio amemaliza mafunzo kwenye Jeshi la Marekani na uzuri Baba yake pia yupo Marekani kwa mambo yake kitambo tu.
Aisee wewe PhD yako na ile ya Magufuli na ya Samia na ya Musukuma ni mapacha. Kweli unaona ni sawa mtoto kuchukuliwa wakati mama yake na baba wapo hai eti kwa sababu tu ya ufukara? Una uhakika gani kuwa atarudishwa wakati mpaka jina limebadilishwa? Pengine hujapata mtoto wewe ndiyo maana unaona ni kuwa mtoto anaweza kuchukuliwa kama bidhaa tu.
 
Kama umesoma hiyo story utakuwa umeelewa vizuri, nia ni njema kabisa na kwa wanaojuwa mchakato wa kuasili mtoto Tanzania si mchakato wa kitoto kama wengi wanavyodhani, wangeshachukuliwa wengi tu kwenye vituo vya Watoto yatima.
Hata Mario Ballotel alichukuliwa(adapt) kwenda kuishi Ital kama ivyo baadae kaja kua star mkubwa kwenye soka. Sasa hao washamba wa Mwanza sijui wamefel wapi
 
Watanzania uchawi ni asili yetu, yani umaskini walionao Wazazi hawaridhiki mpaka mtoto naye arithi dhiki?

Kwa ninavyojuwa Mimi hapo kuna proper communication na huyo muhusika kwa Mimi binafsi sioni tatizo kabisa, kwa asiyeelewa vizuri mambo haya hawezi kuelewa na atamlaumu baba.

Lakini kwa maoni yangu baba amefanya uwamuzi wa busara kabisa kumpa kibali huyo muhindi na ameahidi mtoto atakuwa anarudi kwa Wazazi wake, na isitoshe huyo mtoto anakwenda kuwa RAIA wa Canada na amesoma Canada atakuja kuokowa ndugu zake mbele ya safari.
Kuna usemi 'Mbuzi wa maskini hazai'....

Mama anang'ang'ania kubaki na mtoto wakati hata kumsomesha tu hawezi.

Umaskini wa fikra ni m'baya sana kwa kweli.

Nimesoma uzi nikijua ni ishu ya human traffic kumbe ni maskini flani wasioelewa jambo.

Iko wazi huyo Dada muhindi alimpenda sana huyo mtoto na hiyo ni pure love.

Akawahurumia wazazi wake ambao ni bongo lala.
 
Aisee wewe PhD yako na ile ya Magufuli na ya Samia na ya Musukuma ni mapacha. Kweli unaona ni sawa mtoto kuchukuliwa wakati mama yake na baba wapo hai eti kwa sababu tu ya ufukara? Una uhakika gani kuwa atarudishwa wakati mpaka jina limebadilishwa? Pengine hujapata mtoto wewe ndiyo maana unaona ni kuwa mtoto anaweza kuchukuliwa kama bidhaa tu.
Mbona uzi unaelezea vizuri kabisa mazingira ya muhindi na mtoto? duh!!
 
Back
Top Bottom