Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada, mama abaki analia akizunguka kuomba msaada

Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada, mama abaki analia akizunguka kuomba msaada

Kama mtoto kaenda kweli Canada, hata kama angekuwa ametoroshwa poa tu.

Ila kama kaenda huko Uhindini basi kuna wasiwasi.

Ila Canada, tena mmama wa Watu ka-apply kabisa makaratasi, My instincts can tell, ana nia njema.

Ila kwa hizi kelele, kule Wakisikia just on spot mtoto atarejeshwa. Na pengine kumuweka huyo mama kwenye matatizo.
 
Huna huelewa wa haya mambo kwa wenzetu hasa wale wanawake ambao hawajazaa wana mapenzi ya dhati na Watoto.

Akiadapt mtoto ujuwe mtoto amekula maisha na ndio anamuandikisha kama mrithi wake kwenye life insurance.

Mtoto wa rafiki yangu yupo Marekani kwa style kama hii ya adaption na sasa hivi ni RAIA na ndio amemaliza mafunzo kwenye Jeshi la Marekani na uzuri Baba yake pia yupo Marekani kwa mambo yake kitambo tu.
Mkuu, utaratibu wa ku adopt nchini Tanzania upo tofauti kidogo.
Mtoto ili kumu adopt inabidi asiwe na ndugu wanaojulikana au kama wapo basi anaye adopt hapaswi kujua ndugu wa mtoto na kama ndugu wapo na hawakumchukua, basi hawapaswi kujua kachukuliwa na nani.
Kwa kesi ya huyu jamaa hapa, hii siyo ku adopt, hii ni kuuza tu kama bidhaa nyingine.
 
Kama mtoto kaenda kweli Canada, hata kama angekuwa ametoroshwa poa tu.

Ila kama kaenda huko Uhindini basi kuna wasiwasi.

Ila Canada, tena mmama wa Watu ka-apply kabisa makaratasi, My instincts can tell, ana nia njema.

Ila kwa hizi kelele, kule Wakisikia just on spot mtoto atarejeshwa. Na pengine kumuweka huyo mama kwenye matatizo.
namhurumia kwa kweli, ukute mama mtoto anachochewa na watu wenye wivu tu.

Wakijua kabisa siku sio nyingi na huyo MAMA wa makoroboi atapanda ndege kwenda Canada kwa mtoto wake.
 
Kama aliweza kumuachia mtoto akiwa na mwaka mmoja aishi nae, anashindwa nini kwenye miaka 8?
Huyo Mama aache kushikwa masikio na wasiopenda maendeleo yake, amuache mtoto akatengeneze future.
Wapashkuna wa mtaani kwake hawapendi maendeleo yake.

Washaona kuna siku na yeye atapanda ndege kwenda Canada, awavimbie.
 
Mkuu, utaratibu wa ku adopt nchini Tanzania upo tofauti kidogo.
Mtoto ili kumu adopt inabidi asiwe na ndugu wanaojulikana au kama wapo basi anaye adopt hapaswi kujua ndugu wa mtoto na kama ndugu wapo na hawakumchukua, basi hawapaswi kujua kachukuliwa na nani.
Kwa kesi ya huyu jamaa hapa, hii siyo ku adopt, hii ni kuuza tu kama bidhaa nyingine.
Mkuu wewe huoni LOVE? Muhindi amejuana na baba wa mtoto baada ya mama kuzingua.

Na adoption imetumika hapo ili tu kurahisisha maswala.
 
Sijui mnaonaje hili Mimi ni Baba kukaa na wanangu mbali ni Mwiko.Kama kupambana wacha nipambane mimi wao wawe na Maisha mazuri,sio kutafuta shortcut,Haya Ndio tunekataa Dp World kuja kuchukua vyetu muda usio eleweka.Mtoto ananyanyasika huko aanze kuwalaani akawe Mtumwa wa watu nchi za kigeni.
Soma uzi. Mhindi anaishi na mtoto since 1year!! manyanyaso hapo yangekuwepo ingejulikana tayari.
 
Watanzania uchawi ni asili yetu, yani umaskini walionao Wazazi hawaridhiki mpaka mtoto naye arithi dhiki?

Kwa ninavyojuwa Mimi hapo kuna proper communication na huyo muhusika kwa Mimi binafsi sioni tatizo kabisa, kwa asiyeelewa vizuri mambo haya hawezi kuelewa na atamlaumu baba.

Lakini kwa maoni yangu baba amefanya uwamuzi wa busara kabisa kumpa kibali huyo muhindi na ameahidi mtoto atakuwa anarudi kwa Wazazi wake, na isitoshe huyo mtoto anakwenda kuwa RAIA wa Canada na amesoma Canada atakuja kuokowa ndugu zake mbele ya safari.
Wamuache aje awatoe kwenye umasikini baadae ama sivyo atakuja kuuza maziwa baadae nayeye
 
Yani dogo aachee kusomea kwenye viyoyozi huko Canada aje kusoma shule za kayumba za kugombaniana madawati?

Huyo Mzazi wa mtoto apewe exposure ya kwenda Canada kusu uza macho na kuona mandhari ya Canada ili kuondoa ujinga kisha nadhani akirudi atakubali mwanaye abakie Canada.
 
Katika hali ambayo inaweza kuacha maswali mengi na mtazamo tofauti, mtoto Yusuph Issa Juma mwenye umri wa miaka 8, Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Istiqaama iliyopo Ilemela Jijini Mwanza amesafirishwa kwenda Nchini Canada bila ridhaa ya mama yake.

Mtoto huyo ameondoka katika mazingira tata akiongozana na Watanzania wawili wenye asili ya India, baada ya baba mzazi kutoa ruhusa huku mama mzazi akiwa hana taarifa.
View attachment 2701382

CHANZO CHA MKASA
Mama mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Khadija akiwa mfanyabishara maeneo ya Makoroboi, Mwanza, alianza kuzoeana na dada mwenye asili ya India anayefahamika kwa jina la Narina Haji Dawood.

Nariana alimpenda Yusuph kuanzia akiwa na umri wa mwaka mmoja, alipofikisha mwaka mmoja na nusu akawa anamuomba Khadija amchukue mtoto (Yusuph) akae kwake wakati yeye (mama mtu) akiendelea na biashara zake, Khadija hakupinga hilo.

Baadaye Narina akahamia Kiseke kutoka Makoroboi, akiwa huko akaomba akae na Yusuph na amsomeshe kwa makubaliano kuwa mama mtoto anaweza kwenda kumuona muda wowote na mtoto atakuwa anarudi kwa mama mzazi pindi anapopata nafasi.

MKASA UKAANZA
Baada ya kuishi na Yusuph kwa miaka kadhaa, Narina akaomba kwa mama mzazi ruhusa kuwa anataka kwenda likizo Canada aongozane na mtoto, Khadija akakataa ombi hilo.

Miezi kadhaa baadaye Narina akamjulisha Khadija kuwa ana mpango wa kuhamia Canada, akaomba aondoke na Yusuph, mama mzazi akashikilia msimamo wake wa kukataa ombi kwa mara nyingine.
View attachment 2701383

BABA MZAZI AKAANZA KUSHAWISHIWA
Baada ya kuona mama mzazi ameshikilia msimamo, ikabidi Narina aanze kumshawishi baba mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Issa Juma, wakaanza kumpoa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha.

Baada ya muda wakamshawishi kuwa wana mpango wa kwenda na mtoto Canada, ikabidi baba mtu afungue kesi Mahakamani ya kutaka akae na mtoto.

Inadaiwa Mahakama ikaagiza Mtoto Akaishi na baba, ndipo baba mtu akatumia nafasi hiyo kuanza kufanya mipango kwa kushirikiano na familia ya kina Narina kwa ajili ya mtoto kusafiri.

JINA LA MTOTO LABADILISHWA
Ili kufanikisha mtoto kusafiri ikabidi majina ya mbele ya Yusuph yabadilishwe, kutoka Yusuph Issa Juma na kuwa Yusuph Haji Dawood zikatengenezwa nyaraka zinazoonesha Narina amemuasili (adapt) Yusuph na nyaraka nyingine kadhaa kisha Julai 20, 2023 wakasafiri kuelekeza Canada huku mama mtu akiwa ajui kinachoendelea.

BABA AELEZEA
Issa Juma alipoulizwa amesema “Kweli mtoto ameondoka kwenda Canada, familia iliyomchukua imesema itamsomesha, mimi sina kazi ya maana, nauza maziwa tu mtaani na sina uwezo wa kumsomesha, ni kweli pia uamuzi wa kuondoka kwa mtoto umefanywa kwa upande mmoja.

“Mzazi mwenzangu hakukubali uamuzi huo, tumeshazungumza na Ustawi wa Jamii na Uhamiaji kuhusu hili, msimamo wa mama mtoto ni kuwa anataka mtoto arudi.

“Familia iliyomchukua nimewasiliana nao, mtoto yuko salama na wameahidi kuwa watakuwa wanamrejesha kila baada ya miaka miwili kuja kusalimia.

“Ni kweli pia majina ya mbele yamebadilishwa ili kule anapokwenda ionekane kuna uhusiano kati yao.

“Huyo dada aliyemchukua mtoto hajaolewa wala hana mtoto wa kumzaa, anaishi yeye na kaka yake.”

BABA ASEMA YUPO TAYARI MTOTO ARUDISHWE
“Kwa hiki kinachoendelea, sikuzoea kuishi kwa wasiwasi, kama itawezekana basi wamrudishe tu mtoto, sina nia mbaya ndio maana nazungumza kwa uwazi.

“Maisha yangu ni magumu na sio kwamba nimemuuza mtoto kama inavyosemwa, zaidi nilipewa kompyuta tu, sio kweli kuwa nimepewa nyumba na gari, hiyo nyumba inayosemwa ameachiwa Mzee Felix ambaye ni mtu wa karibu na familia hiyo ya hao Wahindi.”

MAMA WA MTOTO AANGUA KILIO
Akizungumza huku analia, Khadija anasema “Ninachotaka mtoto wangu arudi, niliiachia hiyo familia imlee kwa kuwa waliomba na wakasema watamlipia ada lakini sikutaka waende naye nje ya nchi, nilimwambia msaada wowote anaotaka kwa mtoto autoe akiwa hapa Nchini.

“Nimeshaenda Ustawi wa Jamii, Polisi na Uhamiaji kote sijapata msaada, kwa sasa nipo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ili kutafuta msaada zaidi.”

MAELEZO YA AFISA ELIMU
Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Ilemela, Marco Busungu anasema: Hayo masuala ya Wanandoa sisi tumesumbuka nayo sana, mimi siwezi kulisemea hilo kwa kuwa sijapata taarifa, pia hata kama lingefika tungeangalia ametoroshwa akishwa shuleni au nyumbani? Kwa kuwa baba mzazi yupo na anahusika basi aulizwe yeye kwa kuwa anajua kinachoendelea.

MAELEZO YA AFISA USTAWI WA JAMII
Afisa wa Ustawi wa Jamii, Edith Ngowi anasema “Khadija alikuja kupata ufafanuzi, tulimsindikiza Polisi, tukashauriwa kwenda Uhamiaji, tulipoenda tulioneshwa taratibu zote zimefuatwa na baba mtu akakiri alidanganya ili upatikane uhalali wa mtoto kusafiri.

Lengo lake lilikuwa mtoto apate kuasiliwa na aende akasomeshwe, tumeshauri familia ikae pamoja na Wazazi wa pande zote kuangalia jinsi ya kulimaliza nak ama ni kumrejesha mtoto wafanye hivyo.

UHAMIAJI MWANZA WAULIZWA
Alipoulizwa Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Peter Mbaku juu ya kudaiwa kuchezewa kwa nyaraka za mtoto na hadi kubadilishwa kwa jina kisha kuruhusiwa kwenda Canada, amesema: “Naomba muda nifuatilia hizo taarifa.”
Huna hela unahangaika kujumua maziwa na imeambiwa mtoto atakuwa anakuja kukusalimia sasa ngoja arudi umlishe matembele akuchukie hadi uyachukie maisha yako.
 
Sijui mnaonaje hili Mimi ni Baba kukaa na wanangu mbali ni Mwiko.Kama kupambana wacha nipambane mimi wao wawe na Maisha mazuri,sio kutafuta shortcut,Haya Ndio tunekataa Dp World kuja kuchukua vyetu muda usio eleweka.Mtoto ananyanyasika huko aanze kuwalaani akawe Mtumwa wa watu nchi za kigeni.
Mkuu kuna watu wana akili za ajabu kweli kweli. Eti umpe mtu mtoto wako wa kumzaa kwa sababu tu wewe ni maskini na yeye ni tajiri. Akili za kijinga kabisa hizi.
 
Nimesoma na nikaelewa. Mhindi kukaa na mtoto tangu akiwa mdogo haihalalishi kumbadilisha jina na kumchukuwa huku akidanganya kuwa amem-adopt bila mama mzazi kujua.
Mama mzazi alishaonyesha dalili zakuzingua.

Upendo una nguvu sana, ndio maana Mhindi akaamua kuanza kudeal na BABA mtoto.

Kuhusu majina kubadilisha, hiyo ndio ilikuwa njia rahisi sana kwa huyo dogo kusepa.

Majina sio issue sana lakini, kwa wewe unaitwa macho?
 
Back
Top Bottom