Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada, mama abaki analia akizunguka kuomba msaada

Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada, mama abaki analia akizunguka kuomba msaada

Mkuu kuna watu wana akili za ajabu kweli kweli. Eti umpe mtu mtoto wako wa kumzaa kwa sababu tu wewe ni maskini na yeye ni tajiri. Akili za kijinga kabisa hizi.
Ila watu wa Mwanza nahisi mna shida mahali...

Soma hii


Mwanza hapako sawa kabisa.
 
Soma uzi. Mhindi anaishi na mtoto since 1year!! manyanyaso hapo yangekuwepo ingejulikana tayari.

hawa watu ni wanyama hakuna kama Wahindi,Mwaka mmoja kitu gani?Malengo hapo ni malengo yao,Project hiyo watu wanajua kuigiza,why asiende kuadopt wahindi wenzake huko India,Akaenda nae Canada.Kama anawapenda na kwanin asiiache nyumba kwa wazazi wa hyo dogo amemwachia mtu baki?Kuna kitu hakipo sawa hapa.Ogopa mama akianza kuhisi kitu hakipo sawa, Mama ako connected na mtoto kiasi kwamba kama kuna kitu hakipo sawa nafsi yake haitulii.
 
Mama mzazi alishaonyesha dalili zakuzingua.

Upendo una nguvu sana, ndio maana Mhindi akaamua kuanza kudeal na BABA mtoto.

Kuhusu majina kubadilisha, hiyo ndio ilikuwa njia rahisi sana kwa huyo dogo kusepa.

Majina sio issue sana lakini, kwa wewe unaitwa macho?
Usiwe na akili za kimaskini namna hii! Hivi wewe unaweza kabisa kutoa mtoto wako umpe mtu mwingine kwa sababu tu yeye ana uwezo? Mama alikuwa sahihi kabisa. Hilo li-baba limeweka njaa mbele.
 
Hivi mtu amchukue mtu kutoka hapa kwenda Canada, kwa ajili ya kwenda kumnyanyasa! Hahaha!.
Si rahisi kwa kweli, ameshindwa kumnyanyasa hapa, akafanya hivyo Canada?

By the way kwa wenzetu sheria zao ziko wazi balaa.
Huruhusiwi hata kumchapa mtoto akalia.

Watu wa makoroboi huko mwanza wanawaza manyanyaso 😀
 
Katika hali ambayo inaweza kuacha maswali mengi na mtazamo tofauti, mtoto Yusuph Issa Juma mwenye umri wa miaka 8, Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Istiqaama iliyopo Ilemela Jijini Mwanza amesafirishwa kwenda Nchini Canada bila ridhaa ya mama yake.

Mtoto huyo ameondoka katika mazingira tata akiongozana na Watanzania wawili wenye asili ya India, baada ya baba mzazi kutoa ruhusa huku mama mzazi akiwa hana taarifa.
View attachment 2701382

CHANZO CHA MKASA
Mama mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Khadija akiwa mfanyabishara maeneo ya Makoroboi, Mwanza, alianza kuzoeana na dada mwenye asili ya India anayefahamika kwa jina la Narina Haji Dawood.

Nariana alimpenda Yusuph kuanzia akiwa na umri wa mwaka mmoja, alipofikisha mwaka mmoja na nusu akawa anamuomba Khadija amchukue mtoto (Yusuph) akae kwake wakati yeye (mama mtu) akiendelea na biashara zake, Khadija hakupinga hilo.

Baadaye Narina akahamia Kiseke kutoka Makoroboi, akiwa huko akaomba akae na Yusuph na amsomeshe kwa makubaliano kuwa mama mtoto anaweza kwenda kumuona muda wowote na mtoto atakuwa anarudi kwa mama mzazi pindi anapopata nafasi.

MKASA UKAANZA
Baada ya kuishi na Yusuph kwa miaka kadhaa, Narina akaomba kwa mama mzazi ruhusa kuwa anataka kwenda likizo Canada aongozane na mtoto, Khadija akakataa ombi hilo.

Miezi kadhaa baadaye Narina akamjulisha Khadija kuwa ana mpango wa kuhamia Canada, akaomba aondoke na Yusuph, mama mzazi akashikilia msimamo wake wa kukataa ombi kwa mara nyingine.
View attachment 2701383

BABA MZAZI AKAANZA KUSHAWISHIWA
Baada ya kuona mama mzazi ameshikilia msimamo, ikabidi Narina aanze kumshawishi baba mzazi wa mtoto anayefahamika kwa jina la Issa Juma, wakaanza kumpoa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha.

Baada ya muda wakamshawishi kuwa wana mpango wa kwenda na mtoto Canada, ikabidi baba mtu afungue kesi Mahakamani ya kutaka akae na mtoto.

Inadaiwa Mahakama ikaagiza Mtoto Akaishi na baba, ndipo baba mtu akatumia nafasi hiyo kuanza kufanya mipango kwa kushirikiano na familia ya kina Narina kwa ajili ya mtoto kusafiri.

JINA LA MTOTO LABADILISHWA
Ili kufanikisha mtoto kusafiri ikabidi majina ya mbele ya Yusuph yabadilishwe, kutoka Yusuph Issa Juma na kuwa Yusuph Haji Dawood zikatengenezwa nyaraka zinazoonesha Narina amemuasili (adapt) Yusuph na nyaraka nyingine kadhaa kisha Julai 20, 2023 wakasafiri kuelekeza Canada huku mama mtu akiwa ajui kinachoendelea.

BABA AELEZEA
Issa Juma alipoulizwa amesema “Kweli mtoto ameondoka kwenda Canada, familia iliyomchukua imesema itamsomesha, mimi sina kazi ya maana, nauza maziwa tu mtaani na sina uwezo wa kumsomesha, ni kweli pia uamuzi wa kuondoka kwa mtoto umefanywa kwa upande mmoja.

“Mzazi mwenzangu hakukubali uamuzi huo, tumeshazungumza na Ustawi wa Jamii na Uhamiaji kuhusu hili, msimamo wa mama mtoto ni kuwa anataka mtoto arudi.

“Familia iliyomchukua nimewasiliana nao, mtoto yuko salama na wameahidi kuwa watakuwa wanamrejesha kila baada ya miaka miwili kuja kusalimia.

“Ni kweli pia majina ya mbele yamebadilishwa ili kule anapokwenda ionekane kuna uhusiano kati yao.

“Huyo dada aliyemchukua mtoto hajaolewa wala hana mtoto wa kumzaa, anaishi yeye na kaka yake.”

BABA ASEMA YUPO TAYARI MTOTO ARUDISHWE
“Kwa hiki kinachoendelea, sikuzoea kuishi kwa wasiwasi, kama itawezekana basi wamrudishe tu mtoto, sina nia mbaya ndio maana nazungumza kwa uwazi.

“Maisha yangu ni magumu na sio kwamba nimemuuza mtoto kama inavyosemwa, zaidi nilipewa kompyuta tu, sio kweli kuwa nimepewa nyumba na gari, hiyo nyumba inayosemwa ameachiwa Mzee Felix ambaye ni mtu wa karibu na familia hiyo ya hao Wahindi.”

MAMA WA MTOTO AANGUA KILIO
Akizungumza huku analia, Khadija anasema “Ninachotaka mtoto wangu arudi, niliiachia hiyo familia imlee kwa kuwa waliomba na wakasema watamlipia ada lakini sikutaka waende naye nje ya nchi, nilimwambia msaada wowote anaotaka kwa mtoto autoe akiwa hapa Nchini.

“Nimeshaenda Ustawi wa Jamii, Polisi na Uhamiaji kote sijapata msaada, kwa sasa nipo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ili kutafuta msaada zaidi.”

MAELEZO YA AFISA ELIMU
Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Ilemela, Marco Busungu anasema: Hayo masuala ya Wanandoa sisi tumesumbuka nayo sana, mimi siwezi kulisemea hilo kwa kuwa sijapata taarifa, pia hata kama lingefika tungeangalia ametoroshwa akishwa shuleni au nyumbani? Kwa kuwa baba mzazi yupo na anahusika basi aulizwe yeye kwa kuwa anajua kinachoendelea.

MAELEZO YA AFISA USTAWI WA JAMII
Afisa wa Ustawi wa Jamii, Edith Ngowi anasema “Khadija alikuja kupata ufafanuzi, tulimsindikiza Polisi, tukashauriwa kwenda Uhamiaji, tulipoenda tulioneshwa taratibu zote zimefuatwa na baba mtu akakiri alidanganya ili upatikane uhalali wa mtoto kusafiri.

Lengo lake lilikuwa mtoto apate kuasiliwa na aende akasomeshwe, tumeshauri familia ikae pamoja na Wazazi wa pande zote kuangalia jinsi ya kulimaliza nak ama ni kumrejesha mtoto wafanye hivyo.

UHAMIAJI MWANZA WAULIZWA
Alipoulizwa Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Peter Mbaku juu ya kudaiwa kuchezewa kwa nyaraka za mtoto na hadi kubadilishwa kwa jina kisha kuruhusiwa kwenda Canada, amesema: “Naomba muda nifuatilia hizo taarifa.”
Afisa wa Ustawi wa Jamii, Edith Ngowi anasema “Khadija alikuja kupata ufafanuzi, tulimsindikiza Polisi, tukashauriwa kwenda Uhamiaji, tulipoenda tulioneshwa taratibu zote zimefuatwa na baba mtu akakiri alidanganya ili upatikane uhalali wa mtoto kusafiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuna watu wana akili za ajabu kweli kweli. Eti umpe mtu mtoto wako wa kumzaa kwa sababu tu wewe ni maskini na yeye ni tajiri. Akili za kijinga kabisa hizi.

Cha ajabu zaidi nyumba yake tu ameshindwa kuwaachia,amepewa mtu baki kukaa,Mtoto anaenda kuuzwa Figo hapo 200 Milioni nyie mtakuja kuona Kovu tu kuambiwa aliumwa.
 
hawa watu ni wanyama hakuna kama Wahindi,Mwaka mmoja kitu gani?Malengo hapo ni malengo yao,Project hiyo watu wanajua kuigiza,why asiende kuadopt wahindi wenzake huko India,Akaenda nae Canada.Kama anawapenda na kwanin asiiache nyumba kwa wazazi wa hyo dogo amemwachia mtu baki?Kuna kitu hakipo sawa hapa.Ogopa mama akianza kuhisi kitu hakipo sawa, Mama ako connected na mtoto kiasi kwamba kama kuna kitu hakipo sawa nafsi yake haitulii.
Unafikiri kila Mhindi aliyeko tanzania kwao ni India? acha wivu Bro!
 
Huna huelewa wa haya mambo kwa wenzetu hasa wale wanawake ambao hawajazaa wana mapenzi ya dhati na Watoto.

Akiadapt mtoto ujuwe mtoto amekula maisha na ndio anamuandikisha kama mrithi wake kwenye life insurance.

Mtoto wa rafiki yangu yupo Marekani kwa style kama hii ya adaption na sasa hivi ni RAIA na ndio amemaliza mafunzo kwenye Jeshi la Marekani na uzuri Baba yake pia yupo Marekani kwa mambo yake kitambo tu.
nafikiri unahitilafu ya ubongo..wacha kukimbia wajibu na majukumu kama mzazi au wewe ni mtoto wa mwisho nisipoteze muda wangu bure
 
Sijui mnaonaje hili Mimi ni Baba kukaa na wanangu mbali ni Mwiko.Kama kupambana wacha nipambane mimi wao wawe na Maisha mazuri,sio kutafuta shortcut,Haya Ndio tunekataa Dp World kuja kuchukua vyetu muda usio eleweka.Mtoto ananyanyasika huko aanze kuwalaani akawe Mtumwa wa watu nchi za kigeni.
Hawa ishu yao iko tofauti na wewe unavyosema.
Huyu muhind kaanza kumlea huyo dogo tangu akiwa mwaka mmoja, Na kamsomesha hapohapo mwanza had kufikia miaka 8 ila imetokea huyo muhindi kahamisha makazi kwenda canada, Sasa kuna shida gani kwenda nae? kashazoea kuishi nae huyo dogo kama mwanae.
Hapo cha muhimu ni mawasiliano tu kati ya muhind, mama na mtoto mwenyewe.
 
Unafikiri kila Mhindi aliyeko tanzania kwao ni India? acha wivu Bro!

Sioni Wivu kaka,ni jambo la kusikitisha sana hili,ni Biashara ya binadamu Jiulize mtu ameondoka na mwanao lakini ameshindwa kukuachia nyumba tu ukae?Tuanzie hapo.
 
Sioni Wivu kaka,ni jambo la kusikitisha sana hili,ni Biashara ya binadamu Jiulize mtu ameondoka na mwanao lakini ameshindwa kukuachia nyumba tu ukae?Tuanzie hapo.
Vitu viwili tofauti kabisa.

by the way uhusiano wa Baba mtoto na MAMA mtoto sio mzuri, means hawaishi pamoja.

Then Nyumba angeachiwa nani? je, unajua ni nyumba ya aina gani (maintanance)?

Mhindi kaplay a very vital role hapo, baba angeachiwa nyumba si ndio mngekuwa na ushahidi tosha kuwa kumuuza mtoto?
 
Back
Top Bottom