Baba adaiwa kumuuza mtoto, asafirishwa kwenda Canada, mama abaki analia akizunguka kuomba msaada



Uko sahihi sana.
 
Watu mnamlaumu mama.Kama hao watu wahind na baba wangekuwa na nia njema kwa pamoja wangechukua muda kukaa na mama kumuelemisha faida zote za hiyo issue.Lakn pia hata huko kwenye taasisi za serikal mama angeitwa kuelimishwa.Lakn hiki walichofanya sio kitu kizur.
 



Inawezekana kabisa huyo mama muhindi ana dhamira njema na ya dhati kabisa kuhusu huyo mtoto.

Lakini Mama wa mtoto asikilizwe wasiwasi wake. Aulizwe mashaka yake ni yapi na vikwazo vinatoka wapi.

Taasisi za Serikali zinazohusika na mambo Kama haya, huyo muhindi na baba wa mtoto wazungumze nae kwa kina na ikiwezekana mtoto pia ashiriki hayo maazungumzo na maamuzi. (Nimeona picha ni mkubwa kiasi)

Lakini Kama dhamira ni ovu na mbaya kabisa, nani yupo tayari kubeba lawama za baadae?

Dunia kwa sasa imesimama pabaya sana kuhusiana na hizi kesi za usafirishaji, utumikishwaji na udhalilishwaji kingono na uasili wa watoto.

Kuna kimbunga kibaya sana huko huku wadhalilishaji watoto nao wakifukua “matundu “ ya kisheria yatakayowawezesha “kupewa” haki zao katika jamii Kama kundi lenye mahitaji maalum Kama walivyofanya wale wa Bendera ya marangi mengi mengi Kama upinde wa mvua.

Mwisho kabisa huyo mama mwenye mtoto, huyo ni mtoto wake wa kumzaa, damu na nyama yake. Anayo haki ya asilimia mia moja kukataa hayo makubaliano kati ya baba na huyo muhindi. Sheria na Katiba ya nchi ndio mlinzi wake.

KTY; wasiwasi ndio akili.
 
Kitendo cha muhindi kumchukua mtoto bila ruhusa ya mama yake. Yani hata hajataka mtoto kumuaga mama yake. Hiyo tu inaonyesha muhindi hakuwa na nia njema kwa huyo mtoto na wala hampendi na kafanya kitendo kikatili sana. Mungu amlinde mtoto maana yupo katika hatari kubwa sana maskini
 
Alafu utakuta huyo mama anasumbua watumishi makanisani kwa maombi kuwa MUNGU amfanyie miujiza mtoto wao apate elimu na maisha bora!
 

“Kaishapata maisha mema “



Wallaih I never thought I would live to a day where I will read disgusting crap from you. Complete & all round brokenness. Utumwa na after effects zake vipo kwenye rojo za mifupa yako! It will be centuries before yote ikuishe through your generation, unless you work on it. Bado uko hai.

Wewe na wengine wengi sana humu wenye mitazamo ya utegemezi kwenye hii mada. Tena wengi ni wanaume?!? Yani uzalishe na uzae wewe utegemee kulelewa? How do you preserve your DNA and millions of years of culture & your peoples roots? Your histories?

Nawe mwanamke tena mama na bibi! Yaani kwamba bila huyo mtoto kwenda Canada maisha yake ndio yamehitimishwa?!?! Doh! Una mitazamo ya kitumwa sana. Sana!
 

“Upendo Una nguvu sana”

Hivi mnajisikia vizuri ndani ya vichwa vyenu as you type ama kuna mawimbi yanawazonga fikra zenu?

Upendo kati ya mama mtu mzima asiye na uwezo wa kuzaa watoto wake mwenyewe na mtoto mdogo chini ya miaka 10 asiye na uwezo wa kutambua jema na ovu kinagaubaga?

Upendo ndio umemtuma mpaka kughushi nyaraka za serikali ili kufanikisha jambo lake?

Ndugu yangu, nenda kafanye hivi huko kwao India ama huko Canada halafu lisanuke Kama hivi, child trafficking haikuachi. Mpaka waone huo “Upendo Una nguvu” Una mvi na cheo cha nyampara Gereza la Kisongo ya Canada!

Pesa inamfanya mwanaadam kuwa kiumbe wa ajabu sana. Hawa viumbe wa hii mada ni balaa!
 
Uchungu wa mwana aujuae mzazi...

huyo mama wa kihindi angetakiwa kupata consent ya wazazi wote wawili...

Kama ni maisha bora kwa mtoto angeweza kumtafutia mtoto international school,na kutuma allowance kwa wazazi wake kila mwezi....bado mtoto angekuwa comfortable tu...

Kumchukua mtoto kwa ridhaa ya mzazi mmoja tu inaonyesha alivyo na kiburi/manipulative...

Desperation yake ya kukosa mtoto inamfanya amekuwa selfish,kujali interests zake tu...

Kama ni watoto mbona wako mtaani wengi tu hawana wazazi..

Kumchukua mtoto in this aggressive way kutoka kwa mama yake...NO!,
 
Unakuta hata uwezo wa kumpa mtoto milo miwili kwa siku hana.

Akirudishiwa mtoto anaanza kushindwa ustawi wa jamii kushinikiza baba wa mtoto ahudumie.
 


Kichwa cha habari kilinisisimua, mwacheni mtoto asome, kulaneni Mzae mwingine
 
Si rahisi kwa kweli, ameshindwa kumnyanyasa hapa, akafanya hivyo Canada?

By the way kwa wenzetu sheria zao ziko wazi balaa.
Huruhusiwi hata kumchapa mtoto akalia.

Watu wa makoroboi huko mwanza wanawaza manyanyaso 😀




Kwamba hao Canadians ni watakatifu sana?

Katika hili jambo, mama wa mtoto asikilizwe kwanza wasiwasi wake ni upi na wampe majibu ya kuridhisha kwa kila inquiry yake na Kama bado akiona haiwezekani basi wamrudishe mtoto mpaka pale wazazi wawili wa huyo mtoto watakapokubaliana bila njama ovu wala ulaghai kati yao.

Tuache kuongozwa na hisia zetu na roho zetu za utegemezi na umarioo.

Utaratibu na sheria vifuatwe na haki itendeke na ionekane imetendeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…