Baba Askofu Bandekile Mwamakula asema inawezekana Job Ndugai alisoma Kitabu cha Animal Farm

Baba Askofu Bandekile Mwamakula asema inawezekana Job Ndugai alisoma Kitabu cha Animal Farm

Hahahaaaa...... Animal Farm?

Matusi ya kidini ni hatari sana bwashee!
The animal farm! kwa staili hii kweli ndungai atapenda kuwepo na Uhuru wa habari,aslani hapana kabisa ka! Hili tusi ni la kidipromasia daraja la five 🌟 🌟 🌟🌟🌟
 
labda unashindwa kuelewa nini maana ya mtumishi wa mungu,na endapo ungeelewa basi usinge bandika bandiko lako hapa
Kama ni mungu uliyeandaika hapa ni sawa.. ila Mungu muumba huandikwa kwa kuanza na herufi kubwa. Ikianza na herufi ndogo inamaanisha mizimu yaani ghost, Lakini Mungu huyu ni Almighty God. Sasa kama huyo mch. anamtumikia mzimu, ni sahihi kufanya siasa
 
Je mliokisoma kitabu hicho mliona nini kwenye maandishi yake ? hebu tusimulieni na sisi wengine tuelewe .

====

Inaonekana Spika Ndugai alisoma kitabu cha Animal Farm! Bunge chini ya uongozi wake halikumpa Tundu Lissu nafasi ya kusikilizwa na kujitetea, lakini alihoji akiwa katika Bunge hilo hilo chini ya uongozi wake kama kumi na kenda wa CHADEMA walipewa muda wa kusikilizwa na kujitetea!

Kitabu kile kwa kifupi kilikuwa kinamhusu mkulima aliyekuwa anafuga mifugo mingi tu wakiwemo ng'ombe, kuku nguruwe na wengine. Siku moja wale wanyama wakakutana na kuamua kumpindua mwanadamu yule maana walichoka na kutawaliwa. Wakampindua na nadhani nguruwe ndiye alichaguliwa kuwa kiongozi wao. Walitunga sheria na moja ya sheria ni "All animals are equal". Baada ya muda nguruwe wakaanza kujipendelea zaidi na ndipo wakaibadilisha hiyo sheria wakasema "All animals are equal but some animals are mor equal than others" ili waweze kufanikiwa kutawala na kujinufaisha zaidi kuliko wanyama wengine. Kitabu hiki kilipigwa markefuku na J. K. Nyerere na kikaachwa kusomwa mashuleni maana kilikuwa kinatumika kwenye somo la kiingereza nadhani english literature. Sikumbuki vizuri maana ni zamani sana.
 
Hivi huyo anayejiita Askofu anahubiri dini au anafanya siasa? Achague moja, au ni msemaji wa CHADEMA?
Tafuta kitabu cha animal farm utamuelewa vizuri Askofu.
 
Askofu ni Akili kubwa, Kuna mazezeta watakwepa kunadili hoja ya Askofu na kukimbilia kumu attack
 
Back
Top Bottom