Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
"Wake zetu wanafundishwa namna ya kuja kutushambulia ndani ya familia. Ukisikia vipindi vyote, mwanamke ambaye amekubali kwamba, 'Mimi mume wangu acha atafute, mimi acha nikae na watoto, nilee watoto,' anaonekana ni mjinga kwenye taifa hili.
Wanamtangaza kama mjinga: 'Unakubaliaje kukaa nyumbani? Ene ene...' Mwanaume anachagua mwanamke anayemtaka. Kuna mwanaume anachagua mwanamke anayefanya kazi, na kuna mwanaume anachagua mwanamke anayefanya biashara, na kuna mwanaume anataka mwanamke ambaye atabaki nyumbani na watoto wakati yeye yuko kwenye mapambano.
Sasa, elimu nyingi zinatolewa kwenye vipindi vya redio, ni elimu ambazo zinamwonyesha kwamba mwanamke, 'Lazima utoke, lazima utoke.' Sasa wakati anaanzisha vita ya kutoka kwenye kwenye familia ambayo mwanaume alioa mwanamke ambaye atakaa nyumbani na familia, ndio hapo keka keka zinaanza kutokea.
Mbunge wa Kigoma Mjini Clayton Revocatus (Baba Levo), amesema hayo Juni 1, 2026 akiwasilisha hoja yake bungeni jijini Dodoma wakati bajeti ya Wizara ya wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ikiwasilishwa.