Hivi hata wale wazungu wao nao ni waajabuajabu kama hivi?
Imani ya Mashahidi wa Jehova wazee wa ''Mnara wa Mlinzi'' au ''Watch Tower'' na ''AMKENI''
Charity Organization yao ina nguvu sana CANADA na wana uchumi mkubwa tu na ndio maana hata machapisho yao ni ya standard sana.
Mashahidi wa Jehova ni Wakristo ambao mambo mengi almost 90% wana misimamo kama Wakristo wengine tu, wanapinga dhambi kwa kufuata Amri kumi za Mungu, wanamwamini Yesu Kristo na Mitume wake na shuhuda zake.
•Tofauti kidogo na Madhehebu mengine, wao wana misimamo hii:-
1) Hawaruhusu kabisa Blood Donations, na hawapendekezi waumini wao kutoa au kuwekewa organ yoyote kama Figo ingawa wanawapa Uhuru wa kuamua
2) Hawatumii kabisa damu ya mnyama yeyote kwasababu ni uhai wa mnyama
3) Hawaheshimu, kupigia saluti wala kusimama na kuimba wimbo wa Taifa, kupigia saluti bendera na wala hawaheshimu JESHI, wao wanaamini wa kuheshimiwa na kusujudiwa hivyo ni Mungu pekee
4) Ukihama au kutoka kwenye jumuiya yao Wanakutenga kabisa. Hata kama ni wazazi wako au ndugu wanakuenga na kukata uhusiano.
5) Wanaamini Dhambi lazima ishuhudiwe na Mashahidi wawili ndio iitwe dhambi, yaani kwa mfano ili useme kuwa flani ni Mzinzi ni lazima kuwe na Mashahidi wawili.
Hao ndio Jehova Witnesses