Baba mkwe Shahidi wa Yehova kakataa mahari ya pesa, anataka apelekewe magovi matano ya watu wazima

Baba mkwe Shahidi wa Yehova kakataa mahari ya pesa, anataka apelekewe magovi matano ya watu wazima

Ukiusikia usemi wa watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa basi sasa ndio amini kuwa usemi huo upo na unafanya kazi.

Jumapili iliyopita nilimsindikiza mpwa wangu ( mtoto wa dada yangu yangu) kwenda kujitambulisha na kupangiwa mahari huko kijijini kwa binti (Bibi harusi mtarajiwa)

Kwa kweli mapokezi yalikuwa baridi sana, na tukadhania huenda tungeitiwa wezi. Binti alifichwa na hatukuwa na mwenyeji hata mmoja.

Wenyeji walitupokea, wakatukaribisha chini ya mti na kutuacha kwa zaidi ya masaa manner, huku wao wakiwa ndani wakiendelea na kikao chao.

Baada ya masaa manne kupita hatimaye wakaja tulipo na kuanza kutuuliza maswali ya kebehi sana kuhusu imani yetu.

Wakatuambia wao ni Mashahidi wa Yehova, kwanini tumeenda kumposa binti yao tusitafute binti wa dhehebu letu?

Tukajibu kuwa sisi wote ni Wakristo, lakini hawakuridhishwa na jibu hilo. Dhihaka na kebehi zikaendelea.

Hatukupewa chakula wala maji hadi tunaondoka, tulaambiwa majibu yetu yatafuata kwa barua.

Leo jioni mshenga katuletea barua yenye jibu la ombi letu. Tunatakiwa kupeleka magovi matano ya wanaume watu wazima.

Isome mwenyewe hiyo barua.

Wito wangu kwenu wazazi, kama hamtaki binti yenu aolewe na mtu msiye mtaka, muwe wawazi, sio mnaleta mambo ya ajabu ajabu.

View attachment 2350522
Wakati mwingine uwache utoto! Barua ni ya 2020 nawe unasema ulienda jumapili iliyopita
 
Hapo jamaa ampetipeti vizuri huyo mchumba ampige mimba chap alafu aoe bila hata kuwashirikisha hao miti kunuka......watakitanaga baadaye mbele kwa mbele
 
Hapo jamaa ampetipeti vizuri huyo mchumba ampige mimba chap alafu aoe bila hata kuwashirikisha hao miti kunuka......watakitanaga baadaye mbele kwa mbele
Unazijua gharama za kuzaa mtoto kwenye familia ya kichawi? Tusiendeshwe na hisia za tamaa ya mwili, bali tuendeshwe na utashi na weledi
 
Angekuwa ni baba yangu ningemuuliza, baba unataka Union wewe?
 
pole saaana, haya vipeperushi wanatoa wapi? wanaomba sadaka? ushawahi ona wanaomba chakula, ada hela ya matibabu sehemu?unajua cost ya kipeperushi kimoja chenye rangi?ukiwa interested unapewa Bure.think big ndg!
Kuna shirika lao liko Marekani linaitwa Watch Tower ndio huprint hivyo vijarida
 
Nadhani mtoa mada hajaisema dini, kamsema muumini wa dini. Kwenye dini waumini huwa na mapungufu yao ambayo hayatokani na mafundisho ya dini zao, ndio maana humohumo kwenye watakatifu wamo pia wachawi, je dini unafundisha uchawi?
Me mkristo ila niliwahi pata nafasi ya kujifunza pamoja nao ni watu wema sana wala hawana hizo mambo anazosema mtoa mada.

Sent from my SAMSUNG-SM-N910A using JamiiForums mobile app
 
Mental slavery Ni mbaya mno yaani mno. Binafsi sijataka hata mke wangu aende kanisani. Tunaelekezana Cha kufanya hapa hapa nyumbani. Huko watu wanaenda ku socialize Wala hakuna ka zaidi.
Hongera
 
Nifiriki hakuna ukweli kwenye hili otherwise ulipaswa uripoti polisi sababu amekuagiza ulete kiungo cha binadamu
Also take note hakuna shahidi ya Yehova anaweza kuoa/kuolewa na dini nyingine labda umekuta na watu wanajiita kwa jina lao ila si wao kihalisi
 
Nilipokuwa Russia hiyo dini ya Jehovah Witness ilipigwa marufuku, ni watata sana, bora wafe kuliko kuongezewa damu
Russia hata kutoa ushuzi ni marufuku wamezidiwa padogo sana na Wataleban wa Afghanistan.
 
Mahali sio ishu ishu ni maelewano, binti akisharidhia watapokea mahali akiwa na watoto. Kauzu ufanyiwa kauzu
 
Back
Top Bottom