Baba mwenye nyumba hataki nifanye biashara ya pombe kali

Kama ni hivyo basi hauna sifa ya kuitwa mkataba, lakini nijuavyo mkataba ni makubaliano kukiwa na mashahidi uwe wa maandishi au sauti.
Yaani mkuu huyo anaongea tu😂.

Mtu kalipa kodi almost6 month, kafanya matengenezo makubwa Halafu unaniambia mimi siruhusu kuuza pombe?

Na hakuna sehemu kwenye mkataba unasema hivyo?

Yaani angelipa kila kitu.
 
Mkuu SONDR kama unahitaji wanasheria niambie huyo babu atalipa mpaka pesa ya nauli na chakula atalipa wazee majeuri ndio wazuri.
 
Mueleweshe vzuri Mzee, inawezekana yeye ameambiwa unafungua grocery watu watakaa wanakunywa pombe hapo ndomana anaakataa. Na kama fremu ipo kwenye makazi ya familia na biashara kama ya grocery kweli sio sawa.
Ila kama wananunua na kwenda zao mueleweshe vzuri atakuelewa
 
1. Akurudishie pesa ya matengenezo yako yote uliyafanya ili uhamie pengine.

2. Akurudishie kodi ya nyumba uliyolipa ukaanze pengine.

3. Endelea na msimamo wako kwamba wazo la biashara ni lako huna wajibu wa kumwambia mtu mwingine as long as ni biashara halali kisheria. Ama alitaka umwambie wazo lako yeye akugeuke aanzishe hiyo biashara yeye? Wazo la biashara ni private.

Kama yeye ana ishu za kiimani ama binafsi kuhusu biashara flani yeye ndio alipaswa aweke wazi mapema kwamba biashara flani hazitaki kwenye nyumba yake.
Mkuu kukuongezea fungua na endelea na biashara yako kwa kuzingatia mkataba huo wa awali, maana tayari upo ndani ya mkataba.

Akitaka auvunje mkataba huo wa awali, avunje kwa maandishi akiambatanisha minutes za kikao hicho walichokaa kama familia, akupe NOTISI kwa mujibu wa sheria, akulipe kodi ya miezi yote ya mkataba, akulipe the assumed opportunity utakayoikosa kwa kipindi chote cha mkataba na gharama zote za usumbufu.

Mkuu mengine wanasheria na mawakili nguli kama legendary Pascal Mayalla watakusaidia zaidi!
 
Wanajamvi habari za muda huu, poleni na majukumu ya kutafuta ridhiki. Niende kwenye mada moja kwa moja.

Nimepangisha fremu kwenye NYUMBA moja mjini kwa lengo la kufungua biashara ya pombe Kali yaani liquor store.

Nikaingia mkataba na mwenye nyumba wa miezi kumi wakati huo yeye hajui nataka kufanya biashara gani. Nikanza maandalizi ya kufungua biashara yangu Jana nikaleta mzigo wa pombe Kali ambazo nimefungasha kutoka jijini Dar es salaam.

Baada ya kumaliza kushusha na kuingiza mzigo wangu kwenye fremu yangu nikaondoka nikarudi nyumbani kwangu nikisubiri mzigo mwengine ufike ili niaze kufanya biashara mnamo tarehe moja January 2024.

Cha kushangaza asubuhi ya leo Kama saa kumi na mbili na nusu napokea simu ya baba mwenye nyumba akisema amekaa na familiya na wamekubaliana hawaruhusu biashara ya pombe kwenye nyumba yao nilichoka na kukosa cha kumjibu.

Nikamhoji mbona hukuliweka Hilo kwenye mkataba na kwanini hukusema wakati na kodisha akasema Mimi sikumuambia nataka nifanye biashara gani. Nikamueleza wazo la biashara nilangu ww umekodisha fremu ili Mimi nifanye biashara halali ambayo haivunji Sheria za nchi.

Kama unaitikadi zako kuhusu biashara flani ilikupasa uweke kwenye mkataba ili mimi nikisoma naelewa kwakua siwezi kujua itikadi yako Kama hujasema au kuweka wazi.

Wakuu nachanganyikiwa sielewi nimeshatumia pesa ya kutosha alafu mwenye nyumba anakuja na hoja Kama hii naombeni ushauri wenu wakuu.
Kwa hiyo kijana umeona ni bora ukimbilie huku kuja kunishitaki?
 
Sasa ushauri wa kitu gani hapa una hitaji? si ni akili ndogo tu wewe udai kodi yako ukatafute mahali pengine, kwani sehemu ni moja tu?
 
Kwa akili za mleta mada anataka aachiwe hata akitaka kufungua danguro kwa sababu tu ametoa kodi ya miezi 10! Shenzy!
 
Mkuu dronedrake,

Kama mzee atashindwa kumpisha jamaa akafanya kazi. Pesa yote mpaka kwa mwanasheria atailipa yeye.

Kama hataki hayo akae pembeni atulie. Asubiri anmalize mkataba au jamaa afanye busara kuchukua kodi yake aondoke.
Ww jamaa mbona unachukilia mambo kirahisi rahisi ? Kumbuka hii ni bongo na bongo mambo mengi huwa yanaenda kijanja janja na kujuana kwingi huwezi jua huyo mzee anajiamini nn.

Jamaa achukue hela yake ya pango na matengenezo aliyo yafanya asepe kwani nyumba ni hiyo tu?
Mm ninacho kiona hapa ww unataka huyu jamaa hata hako kamtaji aliki nako kaishe kwa shugulikua kesi za madai ya fidia.
 
Nafkiri hujaelewa pointi tangu mwanzo.

Nisikilize hapa.

Jamaa atamuuliza mzee kama atarudisha pesa na gharama zote au laaah!

Mzee akigoma anaenda kwa mwanasheria anampeleka mkataba walioingia, pale inafatwa sheria tu hakuna maneno ya kusema mimi sitaki tunataka mkataba unasema nini.

Itaandikwa statement kutoka kwa advocate akiombwa arudishe gharama zote pamoja na za mwanasheria ataziambatanisha atapelekewa.

sasa hapo ni yeye mzee aamue kuongea na jamaa wayamalize na hata wakiyamaliza atapaswa kulipa pesa ya mwanasheria sababu kamuingiza gharama zingine.

Na akiamua kutumia nguvu huyo mzee kutoa vitu, hiyo ni kesi nyingine.

Mimi nishakutana na hicho Kisanga. Acha kutisha watu, hatuwezi kuendekeza wazee wapumbavu watu wanapoteza muda na pesa.

Huyo pesa analipa yote. Hataki usumbufu akae pembeni watu wauze pombe.
 
"Eti kujuana kwingi". Jamaa asidai haki yake Kwa kumuogopa Mzee! Ile ni biashara.
 
Wanajamvi habari za muda huu, poleni na majukumu ya kutafuta ridhiki. Niende kwenye mada moja kwa moja.

Nimepangisha fremu kwenye NYUMBA moja mjini kwa lengo la kufungua biashara ya pombe Kali yaani liquor store.

Nikaingia mkataba na mwenye nyumba wa miezi kumi wakati huo yeye hajui nataka kufanya biashara gani. Nikanza maandalizi ya kufungua biashara yangu Jana nikaleta mzigo wa pombe Kali ambazo nimefungasha kutoka jijini Dar es salaam.

Baada ya kumaliza kushusha na kuingiza mzigo wangu kwenye fremu yangu nikaondoka nikarudi nyumbani kwangu nikisubiri mzigo mwengine ufike ili niaze kufanya biashara mnamo tarehe moja January 2024.

Cha kushangaza asubuhi ya leo Kama saa kumi na mbili na nusu napokea simu ya baba mwenye nyumba akisema amekaa na familiya na wamekubaliana hawaruhusu biashara ya pombe kwenye nyumba yao nilichoka na kukosa cha kumjibu.

Nikamhoji mbona hukuliweka Hilo kwenye mkataba na kwanini hukusema wakati na kodisha akasema Mimi sikumuambia nataka nifanye biashara gani. Nikamueleza wazo la biashara nilangu ww umekodisha fremu ili Mimi nifanye biashara halali ambayo haivunji Sheria za nchi.

Kama unaitikadi zako kuhusu biashara flani ilikupasa uweke kwenye mkataba ili mimi nikisoma naelewa kwakua siwezi kujua itikadi yako Kama hujasema au kuweka wazi.

Wakuu nachanganyikiwa sielewi nimeshatumia pesa ya kutosha alafu mwenye nyumba anakuja na hoja Kama hii naombeni ushauri wenu wakuu.
Mpeleke mahakamani akulipe fidia (hahaha yaani atalipia na hizo pombe kali maana atakuwa kazinunua hahaha) ni mjinga. Wewe endelea na kufungua biashara akuvunjie au aoneshe kitu chochote cha kisheria. Pia hakikisha una lesena ya halmashauri na vielelezo vingine, ukienda mahakamani hiyo gharama unaweza imiliki hiyo nyumba
 
"Eti kujuana kwingi". Jamaa asidai haki yake Kwa kumuogopa Mzee! Ile ni biashara.
Kama kwenye mkataba hakuna sehemu inayosema biashara ya pombe haitakiwi, huyo mzee atalipa.

Swali jepesi, kwani kwanini kuna watu wanasoma mkataba anashindwa kusaini? Si sababu anaona kuna vipengele avimlipi au vinambana.

sasa huyo mzee alitaka mtu anayeuja kupanga ndio aotee yeye hataki pombe, poor Tanzania.
 
Nafkiri hujaelewa pointi tangu mwanzo.

Nisikilize hapa.

Jamaa atamuuliza mzee kama atarudisha pesa na gharama zote au laaah!

Mzee akigoma anaenda kwa mwanasheria anampeleka mkataba walioingia, pale inafatwa sheria tu hakuna maneno ya kusema mimi sitaki tunataka mkataba unasema nini.

Itaandikwa statement kutoka kwa advocate akiombwa arudishe gharama zote pamoja na za mwanasheria ataziambatanisha atapelekewa.

sasa hapo ni yeye mzee aamue kuongea na jamaa wayamalize na hata wakiyamaliza atapaswa kulipa pesa ya mwanasheria sababu kamuingiza gharama zingine.

Na akiamua kutumia nguvu huyo mzee kutoa vitu, hiyo ni kesi nyingine.

Mimi nishakutana na hicho Kisanga. Acha kutisha watu, hatuwezi kuendekeza wazee wapumbavu watu wanapoteza muda na pesa.

Huyo pesa analipa yote. Hataki usumbufu akae pembeni watu wauze pombe.
Yaani ni kesi nzuri sana, jamaa awe procative sana yaani aende afungue tena mapema kabisa na asiogope. Hiyo ni neema Mungu kamletea ya kupiga hela kupitia ujinga wa huyo mzee
 
Sijui watu ni kutoelewa
Hivi unakodisha chumba ina maana kwa muda ulokodisha wewe huhusiki na hicho chumba
Hizo habari za kujua mpangaji kaweka biashara gani
Mtu kalala na nani
Kala nini humo ndani
Anajishughulisha na nini?
Huo ni ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani ni kesi nzuri sana, jamaa awe procative sana yaani aende afungue tena mapema kabisa na asiogope. Hiyo ni neema Mungu kamletea ya kupiga hela kupitia ujinga wa huyo mzee
Tena nzuri sana.

Akijaribu kujifanya mbishi sheria itambana mahakamani atatoa fidia kubwa na gharama zote.
 
Back
Top Bottom