Nafkiri hujaelewa pointi tangu mwanzo.
Nisikilize hapa.
Jamaa atamuuliza mzee kama atarudisha pesa na gharama zote au laaah!
Mzee akigoma anaenda kwa mwanasheria anampeleka mkataba walioingia, pale inafatwa sheria tu hakuna maneno ya kusema mimi sitaki tunataka mkataba unasema nini.
Itaandikwa statement kutoka kwa advocate akiombwa arudishe gharama zote pamoja na za mwanasheria ataziambatanisha atapelekewa.
sasa hapo ni yeye mzee aamue kuongea na jamaa wayamalize na hata wakiyamaliza atapaswa kulipa pesa ya mwanasheria sababu kamuingiza gharama zingine.
Na akiamua kutumia nguvu huyo mzee kutoa vitu, hiyo ni kesi nyingine.
Mimi nishakutana na hicho Kisanga. Acha kutisha watu, hatuwezi kuendekeza wazee wapumbavu watu wanapoteza muda na pesa.
Huyo pesa analipa yote. Hataki usumbufu akae pembeni watu wauze pombe.