Baba mwenye nyumba hataki nifanye biashara ya pombe kali

Baba mwenye nyumba hataki nifanye biashara ya pombe kali

Wanajamvi habari za muda huu, poleni na majukumu ya kutafuta ridhiki.
Niende kwenye mada moja kwa moja
Nimepangisha fremu kwenye NYUMBA moja mjini kwa lengo la kufungua biashara ya pombe Kali yaani liquor store.

Nikaingia mkataba na mwenye nyumba wa miezi kumi wakati huo yeye hajui nataka kufanya biashara gani.
Nikanza maandalizi ya kufungua biashara yangu Jana nikaleta mzigo wa pombe Kali ambazo nimefungasha kutoka jijini Dar es salaam.

Baada ya kumaliza kushusha na kuingiza mzigo wangu kwenye fremu yangu nikaondoka nikarudi nyumbani kwangu nikisubiri mzigo mwengine ufike ili niaze kufanya biashara mnamo tarehe moja January 2024.

Chakushangaza asubuhi ya leo Kama saa kumi na mbili na nusu napokea simu ya baba mwenye nyumba akisema amekaa na familiya na wamekubaliana hawaruhusu biashara ya pombe kwenye Nyumba yao nilichoka na kukosa Cha kumjibu.

Nikamhoji mbona hukuliweka Hilo kwenye mkataba na kwanini hukusema wakati na kodisha akasema Mimi sikumuambia nataka nifanye biashara gani
Nikamueleza wazo la biashara nilangu ww umekodisha fremu ili Mimi nifanye biashara halali ambayo haivunji Sheria za nchi.
Kama unaitikadi zako kuhusu biashara flani ilikupasa uweke kwenye mkataba ili mimi nikisoma naelewa kwakua siwezi kujua itikadi yako Kama hujasema au kuweka wazi.

Wakuu nachanganyikiwa sielewi nimeshatumia pesa ya kutosha alafu mwenye nyumba anakuja na hoja Kama hii naombeni ushauri wenu wakuu.
1. Akurudishie pesa ya matengenezo yako yote uliyafanya ili uhamie pengine.

2. Akurudishie kodi ya nyumba uliyolipa ukaanze pengine.

3. Endelea na msimamo wako kwamba wazo la biashara ni lako huna wajibu wa kumwambia mtu mwingine as long as ni biashara halali kisheria. Ama alitaka umwambie wazo lako yeye akugeuke aanzishe hiyo biashara yeye? Wazo la biashara ni private.

Kama yeye ana ishu za kiimani ama binafsi kuhusu biashara flani yeye ndio alipaswa aweke wazi mapema kwamba biashara flani hazitaki kwenye nyumba yake.
 
Nini maana ya mkataba, au hapa huwa mnasaini tu, na je ipoje mkataba unapovunjwa ....kiufupi hapo unastahili fidia ya kodi yako plus muda na hasara ya kuleta mzigo hapo halafu akakubadilikia...nenda mahali tafsiri ya mikataba inapofanyika utafsiliwe huo mkataba.
 
Wanajamvi habari za muda huu, poleni na majukumu ya kutafuta ridhiki.
Niende kwenye mada moja kwa moja
Nimepangisha fremu kwenye NYUMBA moja mjini kwa lengo la kufungua biashara ya pombe Kali yaani liquor store.

Nikaingia mkataba na mwenye nyumba wa miezi kumi wakati huo yeye hajui nataka kufanya biashara gani.
Nikanza maandalizi ya kufungua biashara yangu Jana nikaleta mzigo wa pombe Kali ambazo nimefungasha kutoka jijini Dar es salaam.

Baada ya kumaliza kushusha na kuingiza mzigo wangu kwenye fremu yangu nikaondoka nikarudi nyumbani kwangu nikisubiri mzigo mwengine ufike ili niaze kufanya biashara mnamo tarehe moja January 2024.

Chakushangaza asubuhi ya leo Kama saa kumi na mbili na nusu napokea simu ya baba mwenye nyumba akisema amekaa na familiya na wamekubaliana hawaruhusu biashara ya pombe kwenye Nyumba yao nilichoka na kukosa Cha kumjibu.

Nikamhoji mbona hukuliweka Hilo kwenye mkataba na kwanini hukusema wakati na kodisha akasema Mimi sikumuambia nataka nifanye biashara gani
Nikamueleza wazo la biashara nilangu ww umekodisha fremu ili Mimi nifanye biashara halali ambayo haivunji Sheria za nchi.
Kama unaitikadi zako kuhusu biashara flani ilikupasa uweke kwenye mkataba ili mimi nikisoma naelewa kwakua siwezi kujua itikadi yako Kama hujasema au kuweka wazi.

Wakuu nachanganyikiwa sielewi nimeshatumia pesa ya kutosha alafu mwenye nyumba anakuja na hoja Kama hii naombeni ushauri wenu wakuu.
Wewe mwambie akurudishie pesa yako ukatafute sehemu nyingine

Hata kama mkataba haujasema hivyo , wewe ulitakiwa uwe muwazi.

Watu wana heshima zao hawawezi kukupa fremu uuzie pombe, watu wapige makelele, watukanane, wapigane, wawachukize watu nk

Yote haya yeye atalazimika kupata lawama kwa majirani

Ukitaka kufanya biashara ya pombe kakodi fremu kwa walevi wenzako.

NB

Ukienda kwa mwanasheria utajisumbua na kupoteza pesa tu

Huwezi kumlazimisha mtu ufanye biashara asiyoitaka kwenye jengo lake
 
Nini maana ya mkataba, au hapa huwa mnasaini tu, na je ipoje mkataba unapovunjwa ....kiufupi hapo unastahili fidia ya kodi yako plus muda na hasara ya kuleta mzigo hapo halafu akakubadilikia...nenda mahali tafsiri ya mikataba inapofanyika utafsiliwe huo mkataba.
Huo mkataba umeuona ?

Mkataba wa mpangaji huwa unabase kwenye malipo tu

Ukizingua unatolewa muda wowote na huna cha kufanya
 
Mosi,
Pole sana mkuu. Gharama na muda uliotumia kutafuta mpaka kupata hiyo nafasi ya biashara hapo.

PIli, muulize mzee yeye anasemaje? Kama anataka kurudisha pesa ni sawa ila tu alipe na gharama zako zote za kuleta mzigo na usumbufu, na hilo likiwa gumu yeye kulitekeleza omba ushauri kwa wanasheria wakuandikie statment ya msimamo wake maana yeye kwenye mkataba hakusema biashara gani si ruksa kufanya hapo kwake.

Hii ishu nishawahi kutana nayo. Nilienda kwa mwanasheria yule bibi mwenye fremu kuona vile akaniambia mwanangu tuongee tuyamalize.

Asitake kusumbua watu, tena alipe gharama zote
Huu ndio ushauri sahihi hapa.
 
Huu ndio ushauri sahihi hapa.
Yaani mkuu mimi ilishawahi nitokea.

Nikamfata bibi nikamwambia bibi nataka utoe tamko watoto wake wakawa wanaleta maneno ya kejeli.

Nikasimama nikaondoka kwenda kumueleza mwanasheria, akaandika statment ndani ya siku 3 watoe tamko aidha sheria ichukuliwe.

Bibi yule alinifata akaniambia mwanangu naomba tuyaongee yaishe
tuongee kindugu tu.

Huyo babu anapima upepo yaani sema tu jamaa asifatilie.atalipa mpaka pesa ya bodaboda ningemuhesabia.
 
Kwenye masharti ya mkataba wake kuna kipengele kinakataa biashara ya pombe? Kama hakipo january endelea na biashara yako kama kawaida
Kwenye mkataba wake hakuna kifungu kinachokataza aina ya biashara ila mkata unainisha kunga chumba kwa ajiri ya biashara
 
Wewe mwambie akurudishie pesa yako ukatafute sehemu nyingine

Hata kama mkataba haujasema hivyo , wewe ulitakiwa uwe muwazi.

Watu wana heshima zao hawawezi kukupa fremu uuzie pombe, watu wapige makelele, watukanane, wapigane, wawachukize watu nk

Yote haya yeye atalazimika kupata lawama kwa majirani

Ukitaka kufanya biashara ya pombe kakodi fremu kwa walevi wenzako.

NB

Ukienda kwa mwanasheria utajisumbua na kupoteza pesa tu

Huwezi kumlazimisha mtu ufanye biashara asiyoitaka kwenye jengo lake
Mwenye heshima zake anakuambia masharti yake kabla hajakupangisha. Huyo mwenye fremu ni muhuni TU.

Mind you, katika kutafuta nyumba nishakutana na mwenye nyumba anasema kabisa kuwa "Mimi sipangishi Mkristo", "Mimi siruhusu nguruwe aliwe nyumbani kwangu" na "Mimi sipangishi bachela" na mwingine alisema "sitaki mpangaji mwenye watoto" Haya ni masharti ambayo mtu mwenye busara huyaweka wazi kabla ya kuchukua Hela ya mpangaji.
 
Huo mkataba umeuona ?

Mkataba wa mpangaji huwa unabase kwenye malipo tu

Ukizingua unatolewa muda wowote na huna cha kufanya
Huna cha kufanya ni huko kwenu Kwa wajinga wajinga. Una shida ya Hela ndio maana unapangisha, otherwise Baki na vyumba vyako uweke misukule. Hiyo ni biashara Sio msaada.
 
Pombe haziharibiki, anafaulisha ama kuweka ome akiangalia sehemu ingine
Hiyo pesa yakuanzisha masaji anaipata wapi mtu alishalipia mzigo?

Hapo suala ni moja alipe gharama zote, mpaka mzigo kufika hapo ndani na kama kuna marekebisho jamaa kafanya alipe mpaka pesa aliyokula.

Huyo mzee anatingisha kiberiti.
Kama hawezi aache watu wafanye kazi mpaka mkataba uishe.
 
Kama hiyo ni fremu kama anavyodai mpangaji, ina maana anaweza kufanya biashara yoyote halali. Hilo ni kosa la mwenye fremu, alitakiwa kabla hajampangisha mtu AMPE na masharti ya biashara Gani hataki zifanyike kwenye fremu yake. Kujaa kimya maana yake "fanya biashara yoyote halali ili mradi unilipe Kodi yangu" .

Sheria za nchi ndizo hizo hizo zilizompa uhalali wa Hilo eneo analoliita la kwake kujenga. Usisahau.
Mkuu kumbuka hii ni bongo kila jambo linaenda kijanja janja.
 
kubali hasara, akurudishie kodi ila pesa sijui ya hasara sahau

kwenda kwa mwanasheria unapoteza mda na pesa zako
 
Hili kuondoa mkanganyiko tumia hekima yaani asikuumize na wewe usimuumize.

Maana Kwa imani nikweli baadhi ya WATU wanazichukia Sana pombe .

Mwambie Kwa ustaharabu kuwa akurudishie pesa ikiwemo na fidia ambayo umeingia katika matengenezo.
 
kubali hasara, akurudishie kodi ila pesa sijui ya hasara sahau

kwenda kwa mwanasheria unapoteza mda na pesa zako
Mkuu dronedrake,

Kama mzee atashindwa kumpisha jamaa akafanya kazi. Pesa yote mpaka kwa mwanasheria atailipa yeye.

Kama hataki hayo akae pembeni atulie. Asubiri anmalize mkataba au jamaa afanye busara kuchukua kodi yake aondoke.
 
Huo mkataba umeuona ?

Mkataba wa mpangaji huwa unabase kwenye malipo tu

Ukizingua unatolewa muda wowote na huna cha kufanya
Kama ni hivyo basi hauna sifa ya kuitwa mkataba, lakini nijuavyo mkataba ni makubaliano kukiwa na mashahidi uwe wa maandishi au sauti.
 
Back
Top Bottom