Baba mwenye nyumba hataki nifanye biashara ya pombe kali

Baba mwenye nyumba hataki nifanye biashara ya pombe kali

Joking ila mzee gharama lazima alipe.
Anaweza akalipa lakini afikrie muda atakaopoteza! Na unajua ujinga wa kesi za madai, zee linaweza kusema litamlipa kidogo kidogo sasa hapo itakuwa imetoka hiyo!
 
Unapoenda kukodi pango ulitakiwa kumueleza mwenye nyumba kuwa utafanya biashara gani kwenye jengo lake na sio kukaa kimya eti biashara ni ya kwako hizo mambo tunafanya tukiwa na eneo la kwako mwenyewe ukiamua iwe garage sawa mwezi ujao unabadili inakua Car wash sawa mwaka ujao utabadili kuwa Super Market ni wewe ila sio eneo la mtu upange wewe aina ya biashara bila kumshirikisha...
 
Iyo mikataba yenu ya uchochoroni uku mahakamani ni useless
 
Wewe endelea kutetea wazee wapumbavu.

Wewe unaongelea nadharia hujui uchungu wa kuanzisha biashara Halafu mzee mjinga tu akuambie mimi siruhusu.

Kama unataka kujua hili andika mkataba kama wa huyo mzee Halafu mpangishe mtu mwambie hayo anayosema huyo mzee.
Wewe mkuu ndiye unaongelea nadharia. Hivi ulishawahi kusimama mahakamani hata siku moja? Usumbufu wa mahakamani wacha kabisa, hakuna watu pale! Ningekuwa Rais ningevunja mahakama zote nikawapa JWTZ! Kuna ujinga mwingi sana pale! Huyo ndugu yako akifuata ushauri wako huu haki ya nani atafirisika jumla!
 
Wanajamvi habari za muda huu, poleni na majukumu ya kutafuta ridhiki. Niende kwenye mada moja kwa moja.

Nimepangisha fremu kwenye NYUMBA moja mjini kwa lengo la kufungua biashara ya pombe Kali yaani liquor store.

Nikaingia mkataba na mwenye nyumba wa miezi kumi wakati huo yeye hajui nataka kufanya biashara gani. Nikanza maandalizi ya kufungua biashara yangu Jana nikaleta mzigo wa pombe Kali ambazo nimefungasha kutoka jijini Dar es salaam.

Baada ya kumaliza kushusha na kuingiza mzigo wangu kwenye fremu yangu nikaondoka nikarudi nyumbani kwangu nikisubiri mzigo mwengine ufike ili niaze kufanya biashara mnamo tarehe moja January 2024.

Cha kushangaza asubuhi ya leo Kama saa kumi na mbili na nusu napokea simu ya baba mwenye nyumba akisema amekaa na familiya na wamekubaliana hawaruhusu biashara ya pombe kwenye nyumba yao nilichoka na kukosa cha kumjibu.

Nikamhoji mbona hukuliweka Hilo kwenye mkataba na kwanini hukusema wakati na kodisha akasema Mimi sikumuambia nataka nifanye biashara gani. Nikamueleza wazo la biashara nilangu ww umekodisha fremu ili Mimi nifanye biashara halali ambayo haivunji Sheria za nchi.

Kama unaitikadi zako kuhusu biashara flani ilikupasa uweke kwenye mkataba ili mimi nikisoma naelewa kwakua siwezi kujua itikadi yako Kama hujasema au kuweka wazi.

Wakuu nachanganyikiwa sielewi nimeshatumia pesa ya kutosha alafu mwenye nyumba anakuja na hoja Kama hii naombeni ushauri wenu wakuu.
Hakuna ushauri mpe nyumba yake akupe pesa yako!
 
Wewe mwambie akurudishie pesa yako ukatafute sehemu nyingine


Hata kama mkataba haujasema hivyo , wewe ulitakiwa uwe muwazi.

Watu wana heshima zao hawawezi kukupa fremu uuzie pombe, watu wapige makelele, watukanane, wapigane, wawachukize watu nk


Yote haya yeye atalazimika kupata lawama kwa majirani

Ukitaka kufanya biashara ya pombe kakodi fremu kwa walevi wenzako.


NB

Ukienda kwa mwanasheria utajisumbua na kupoteza pesa tu

Huwezi kumlazimisha mtu ufanye biashara asiyoitaka kwenye jengo lake

hujielewi wewe embu jisome tena ulichokiandika[emoji30][emoji30]
 
Kwa akili za mleta mada anataka aachiwe hata akitaka kufungua danguro kwa sababu tu ametoa kodi ya miezi 10! Shenzy!

Biashara ya Danguro nikosa kisheria, kifungu gani cha sheria kinachokataza biashara ya pombe??
 
Back
Top Bottom