Anaweza akalipa lakini afikrie muda atakaopoteza! Na unajua ujinga wa kesi za madai, zee linaweza kusema litamlipa kidogo kidogo sasa hapo itakuwa imetoka hiyo!Joking ila mzee gharama lazima alipe.
Wewe mkuu ndiye unaongelea nadharia. Hivi ulishawahi kusimama mahakamani hata siku moja? Usumbufu wa mahakamani wacha kabisa, hakuna watu pale! Ningekuwa Rais ningevunja mahakama zote nikawapa JWTZ! Kuna ujinga mwingi sana pale! Huyo ndugu yako akifuata ushauri wako huu haki ya nani atafirisika jumla!Wewe endelea kutetea wazee wapumbavu.
Wewe unaongelea nadharia hujui uchungu wa kuanzisha biashara Halafu mzee mjinga tu akuambie mimi siruhusu.
Kama unataka kujua hili andika mkataba kama wa huyo mzee Halafu mpangishe mtu mwambie hayo anayosema huyo mzee.
Hakuna ushauri mpe nyumba yake akupe pesa yako!Wanajamvi habari za muda huu, poleni na majukumu ya kutafuta ridhiki. Niende kwenye mada moja kwa moja.
Nimepangisha fremu kwenye NYUMBA moja mjini kwa lengo la kufungua biashara ya pombe Kali yaani liquor store.
Nikaingia mkataba na mwenye nyumba wa miezi kumi wakati huo yeye hajui nataka kufanya biashara gani. Nikanza maandalizi ya kufungua biashara yangu Jana nikaleta mzigo wa pombe Kali ambazo nimefungasha kutoka jijini Dar es salaam.
Baada ya kumaliza kushusha na kuingiza mzigo wangu kwenye fremu yangu nikaondoka nikarudi nyumbani kwangu nikisubiri mzigo mwengine ufike ili niaze kufanya biashara mnamo tarehe moja January 2024.
Cha kushangaza asubuhi ya leo Kama saa kumi na mbili na nusu napokea simu ya baba mwenye nyumba akisema amekaa na familiya na wamekubaliana hawaruhusu biashara ya pombe kwenye nyumba yao nilichoka na kukosa cha kumjibu.
Nikamhoji mbona hukuliweka Hilo kwenye mkataba na kwanini hukusema wakati na kodisha akasema Mimi sikumuambia nataka nifanye biashara gani. Nikamueleza wazo la biashara nilangu ww umekodisha fremu ili Mimi nifanye biashara halali ambayo haivunji Sheria za nchi.
Kama unaitikadi zako kuhusu biashara flani ilikupasa uweke kwenye mkataba ili mimi nikisoma naelewa kwakua siwezi kujua itikadi yako Kama hujasema au kuweka wazi.
Wakuu nachanganyikiwa sielewi nimeshatumia pesa ya kutosha alafu mwenye nyumba anakuja na hoja Kama hii naombeni ushauri wenu wakuu.
Wewe mwambie akurudishie pesa yako ukatafute sehemu nyingine
Hata kama mkataba haujasema hivyo , wewe ulitakiwa uwe muwazi.
Watu wana heshima zao hawawezi kukupa fremu uuzie pombe, watu wapige makelele, watukanane, wapigane, wawachukize watu nk
Yote haya yeye atalazimika kupata lawama kwa majirani
Ukitaka kufanya biashara ya pombe kakodi fremu kwa walevi wenzako.
NB
Ukienda kwa mwanasheria utajisumbua na kupoteza pesa tu
Huwezi kumlazimisha mtu ufanye biashara asiyoitaka kwenye jengo lake
Kwa akili za mleta mada anataka aachiwe hata akitaka kufungua danguro kwa sababu tu ametoa kodi ya miezi 10! Shenzy!