Baba wa kambo jela kwa kumuambukiza mtoto UKIMWI kwa makusudi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1685543081129.png
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mara imemuhukumu kwenda jela miaka saba Msirari Muhere (60) mkazi wa Wilaya ya Tarime baada ya kupatikana na hatia ya kumuambukiza ugonjwa wa Ukimwi mtoto wa miaka sita kwa makusudi.

Hukumu hiyo imetolewa mjini hapa leo Mei 31, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu mwenye mamlaka ya ziada ya kusikiliza mashauri ya Mahakama Kuu, Timoth Swai baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.

Awali kesi hiyo ya jinai namba 7/2023 ilifunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime Juni 2021 na kutolewa humu Novemba 2022 ambapo hakimu wa mahakama hiyo ya Tarime aliamuru mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh200,000 au kwenda jela miaka mitano katika kesi hiyo iliyosajiliwa kwenye mahakama hiyo kwa namba 186/2021.

Kufuatia hukumu hiyo mshtakiwa huyo alilipa faini na kisha kuwa huru.

Hakimu Swai amesema kuwa kutokana na hukumu hiyo, Jamhuri ilikata rufaa Mahakama Kuu baada ya kutokuridhishwa na hukumu kwa maelezo ilikuwa kinyume cha Sheria ya Kuzuia Maambukizi ya Ukimwi namba 28 ya mwaka 2008.

"Sheria hii inatamka kuwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kusambaza Ukimwi kwa makusudi hukumu yake ni kifungo cha kati ya miaka mitano hadi 10 jela na hakuna chaguo la faini,"amesema.

Akitoa maelezo ya tukio hilo, hakimu Swai amesema kuwa mwaka 2018 Muhere alioa mke wa pili ambaye alikuwa na watoto watatu ambao aliamua kuishi nao pamoja na mama yao.

Amefafanua kuwa baadaye wanandoa hao waligombana hali iliyopelekea kutengana huku mwanamke huyo akiwaacha watoto wake watatu na baba yao huyo wa kufikia.

Ameongeza kuwa baadaye wanandoa hao walimaliza tofauti zao na kuanza kuishi tena pamoja kama mke na mume na kwamba baada ya muda mwanamke huyo aligundua kuwa mume wake aliwaambukiza watoto wake Ukimwi kwa makusudi.

"Ushahidi umeonyesha kuwa Muhere alichukua sindano na kunyonya damu kutoka kwa mtoto wa mke wake mkubwa ambaye alikuwa ameathirika kisha kuanza kuwadunga watoto wawili wa huyu mke wake wa pili na uchunguzi wa kitabibu umebaini kuwa kati ya hao watoto wawili mmoja wa kiume ameambukizwa ugonjwa wa Ukimwi," amesema.

"Muhere na mke wake mkubwa ni waathirika wa Ukimwi na binti yao alizaliwa na ugonjwa huo kwa hiyo baada ya kutofautiana na mke mdogo aliamua kumkomesha kwa kuwaambukiza watoto wake Ukimwi labda kwasababu hawakuwa wa kwake (Muhere) wa kuzaa," ameongeza.

Katika kesi ya awali jumla ya mashahidi sita walitoa ushahidi wao akiwemo mama pamoja na mtoto ambapo katika rufaa hiyo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali, Felix Mshama na Joyce Matimbwi.

MWANANCHI
 
Hapa mbona adhabu yake ni kama kuua tu, afungwe maisha jela mchawi huyo!!
 
Sheria bado ni nyepesi mno.

Kwa muktadha huo atakaa gerezani kwa miaka minne na point. Wakati ukatili aliowafanyia watoto ni wa maisha.

Sheria inabidi iongezewe meno. 30 years at least.
30 michache sana, kama kweli amefanya hayo (hajasingiziwa), basi kifungo cha maisha jela ni haki yake.., yaani ingekuwa mimi huyo angekula shaba ya kichwa
 
Habari mbaya sana hii kwa siku ya leo.Watoto ?!Kwa nini umefanya hivyo Mzee Muhere?.Anyway Mungu ndio anajua.
 
Sheria bado ni nyepesi mno.

Kwa muktadha huo atakaa gerezani kwa miaka minne na point. Wakati ukatili aliowafanyia watoto ni wa maisha.

Sheria inabidi iongezewe meno. 30 years at least.
Naomba usikilizwe
 
Adhabu iliyo tolewa ni ndogo mno, hizi sheria zipitiwe upya watu kama hawa wawe wananyongwa tu, fala sana hilo lizee.
 
Back
Top Bottom