Baba wa Manabii na Mitume wote Ibrahimu au Abrahamu alikuwa Dini gani?

heshima gani ninayeitaka humu mimi nisiye na umaarufu humu kati ya members zaidi ya laki sita? Kwa hiyo unajibu kipuuzi kwa kuwa una jazba. We dini huijui kaa kimya
 
Wakini mwingine muwe makini enyi waumini wa dini, tulizeni munkari na jazba humu kuna watu wanajua kucheza na akili za watu, ukijua haya hautatokwa na povu
 
Wanasema ni dini iliyokamilika tangu imekuja lakini.

Mud ndio laleta nguzo 5 hivyo kabla kama ilikuwepo wakati wa Ibrahim zilikuwepo nguzo ngapi.

Sasa hivi wakokunasa ili ujiunge nao Wana shahada sijui ni ya sheria au ya udaktari wanakuambia utamke, Sasa kama hicho kitabu hakikuwepo na huyo mud hakuwepo hiyo shahada enzi hizo ilikuwa inatamkwaje au mshkaji aliichomekea ili awe anatakiwa tajwa?
 
Naomba unisaidie kufahamu. Ili uwe muislamu ni lazima ushuhudie kuwa mwenyezi mungu ni mmoja na Muhammad ni mtume wake. Yaani ni lazima utoe shahada.

Sasa nafahamu Ibrahimu alikuwepo kabla ya mtume Muhammad. Je, aliisema hii shahada au alifanyaje akawa muislamu? Asante.
 
Sheikh, tuliza kwanza mzuka! Kwa hiyo unataka kusema Uislamu ulikuwepo hata kabla ya kuzaliwa Mtume wenu Muhammad SAW? Siku zote nilijua yeye Mtume Muhammad ndiye muasisi wa Uislamu!

Maana kwenye Biblia, Ibrahimu anaonekana kuwepo miaka mingi iliyopita! Yaani kabla ya Yesu kuzaliwa karne ya 1 AD, na pia Mtume wenu miaka zaidi ya 500 AD!
 
Mimi simjuzi sana ila uchache wangu wa elimu jibu lako ni kuwa:
1. Shahada hutumiwa kwa mtu aletoka kwenye dini nyengine kuingia kwenye uislam, kwa mfano wa Abraham yeye hakuwa katika dini nyengine kwa hio hakusilimu.
2. Kwa kilamtume kutoka Adam wanaposilimu huwa wanatoa shahada kwa kukubali kuwa Muungu ni mmoja na mtume wa wakati huo kuwa ni mtume wa Muunge kwamfano kipindi cha Abraham utashahadia kwa kusema Allan ni mmoja na Abraham ni mtume wa Allah, kipindi cha Yesu (Issa bin maryyam) utashuhudia kuwa Allah ni mmoja naYesu ni mtume wa Allah nk
3. Shahada yeyote huwa ina maneneo ya kumtambua kuwa Allah ni mmoja na kwa upande wa pili Mtume wa wakati husika ni mjumbe wa Allah.
Ndio maana kwa waislamu lazima uwaamini mitume yote yaloopita ni sharti na siombi, kwa kuwa wote wametumwa na Allah
 
Mimi naona wewe ndiyo umeeleza sasa kwa usahihi.
 
Kwa nini nyie waumini mnapenda kuingizwa chaka na mnaingia wote? Jibuni hoja achaneni na mimi mtachoka bure, mtaota sugu vidoleni mwenu kwa kubonyesa kibodi ili mjibizane na mimi ambaye hata sikuanzisha mada
 
Alikuwa myahudi. No 2 ways about it. Japo wazee wa kung’ang’ania vitu vya watu watadai alikuwa team mnyaazi😂 jamaa hawa huenda wakadai hata baraba alikuwa mvaa kubadhi😂. Hawanaga aibu wala haya
 
hili swali nalikalibisha tu,kwa watu wenye uelewe wa mambo ya Dini.

Huyu ni nabii na mtume wa Mwenyezi Mungu,ambaye anakubaliki na Dini zote,kuanzia Uyahudi,Ukristo mpaka Uisilamu,na hawa wote ibada zao zimetofautiana.

Je niwapi wanaomfata?


Mimi kwa mtazamo wangu haijatajwa Nabii Ibrahimu (as) ana dini gani, kilichotajwa ndani ya Qur'an ni kwamba Nabii Ibrahimu alikuwa mnyenyekevu/aliyejitupa kwa Allah na hii unaweza kupata katika Qur'an 2:127-128, ambapo amemuomba Allah amfanye awe mnyenyekevu, neno unyenyekevu ndio "Islam" na mtu mnyenyekevu anaitwa "muslim" kwa kiarabu, hivyo popote nabii Ibrahimu anapotajwa ndani ya Qur'an kwa jina la la "Muslim" maana yake ni hiyo kwamba yeye ni mnyenyekevu na hata manabii wote wanabeba sifa hiyo ya kuitwa "Muslimina" yaani wanyenyekevu mbele ya Allah.

Kitu kinacho wachanganya watu ni kuona manabii wameitwa Muslimina na hivyo kusema kwamba wao ni Waisilamu waliofuata dini ya Kiisilamu dini hii iliyoanzishwa na mtukufu mtume Muhammad (saw)-- kitu ambacho sio sahihi kwani Dini hii ya kiisilamu imejengwa katika nguzo 5 na nguzo ya kwanza (shahadatein) ambayo ili uwe muisilamu lazima uitamke katika kila swala (katika kikao cha attahiyyatu) nk, je kama nabii Ibrahimu alikuwa mfuasi wa dini hii (hata kabla haijaanzishwa) alikuwa akitoa hii shahada hii?? je alifunga swaumu hii ya Ramafhani??, kuna maswali mengi kwa wale wanaoshindwa kujua Nabii Ibrahimu anapoitwa Muslim ina maana gani!!.

Hivyo nabi Ibrahimu (as) ni Muslim kwa maana ya unyenyekevu na sio Muslim kwa maana kwamba yeye ni mfuasi wa dini hii ya Kiisilamu dini iliyoanzishwa na mtukufu mtume Muhammad (saw) ambayo imejengwa katika nguzo tano, na manabii wote wameitwa Muslim kwa maana hiyo ya kuwa wao ni wanyenyekevu mbele ya Allah.
 
Haya ww tuambie Ibrahimu alikuwa dini gani?
 
Alikuwa myahudi. No 2 ways about it. Japo wazee wa kung’ang’ania vitu vya watu watadai alikuwa team mnyaazi[emoji23] jamaa hawa huenda wakadai hata baraba alikuwa mvaa kubadhi[emoji23]. Hawanaga aibu wala haya
Ibrahimu hakuwa myahudi bali alikuwa mkurdi kutoka Iraq.
 
Wakristo wote wanafahamu Ukristo ulianza baada ya Yesu kuja na kwamba agano la kale liliandikwa na watu wa dini ya Uyahudi. Sijui wewe hizi porojo zako na matango pori uliyoandika hapa ulilishwa na nani?!
 
Mimi ninachofahamu hakuwa na dini! Isipokuwa alikuwa ni mtu mkamilifu mbele za Mungu, na hivyo Mwenyezi Mungu kumbariki yeye na ukoo wake.
Una haki ya kuamini hivyo kwa sababu imani yako inakuambia hivyo.

Lakini pia na waislam wana haki ya kuamini kwa mujibu wa imani yao inavyo sema huo ndo unaitwa uhuru wa kuabudu.

Waislam kusema Ibrahim alikuwa muislam haikupunguzii chochote ww mpaka ukereke kwa Ibrahim kuitwa muislam.

Kila mtu ahamini kile anacho amini hakuna haja ya kudhihakiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…