Baba wa Manabii na Mitume wote Ibrahimu au Abrahamu alikuwa Dini gani?

Baba wa Manabii na Mitume wote Ibrahimu au Abrahamu alikuwa Dini gani?

Kuna kitu huwa tunashindwa kuelewa kuhusu dini, maranyingi Wakristo wamekuwa wakiwakebehi Waislam wasemapo kwamba manabii ama mitume fulani waliokuwepo miaka mingi nyuma kabla ya Uislam ni Waislam. Hamtakiwi kukebehi kuhusu hili maana ndio imani yao na vitabu vyao vimeandika hivi.

Kinachofurahisha Wakristo wao hujiona wako sahihi kusema Manabii hao wlikuwa upande wao wakati Ukristo umekuja baadae sana.

Iko hivi: Wayahudi wanaamini maandiko yao matakatifu (Torah). Wakristo wameandika katika biblia yao takatifu kuhusu Moses na maandiko yake lakini hii haiwezi kuwashawishi Wayahudi waamini kwamba Ukristo ulikuwepo tangu kipindi cha Musa. Vivyo hivyo kwa Waislam, Quran imeandika kuhusu Musa na hata Yesu lakini hiyo haitawafanya Wakristo waamini kwamba Uislam ulikuwepo kabla ya Yesu.

Mkijua hili wala hakuna haja ya kumsema mwenzako wakati hata wewe umefata mfumo huo huo. Wakristo wanaamini Wayahudi walimkataa Yesu na walijutia kwa hilo baada ya kumuua lakini ukweli hadi leo hii Wayahudi hawamuamini Yesu kama messiah. Waislam wanaamini Muhammad ni muendelezo wa mpango wa Mungu kuwaleta wasaidizi wake kueleza utukufu wake lakini Wakristo hawaamini katika hilo.

Anayewaita wenzake wafia dini yeye keshaoza katika dini yake[emoji23]
Wasipokuelewa hapa mkuu basi tena.
 
Umeeleza vizuri sana, Dini ni mfumo wa maisha kwa nabii Ibrahimu mfumo huo ulikuwa haujakamilika na umekuja kukamilika kwa mtukufu mtukufu mtume (saw) na hapo ndio Allah akaupa jina Islam na akauwekea nguzo 5, huko nyuma kwakuwa haukuwa kamili Allah hakuupa jina lolote mfumo huo bali walioufuata mfumo huo Walitambulika kama Waisilamu kwa maana ya unyenyekevu.

Sisi leo tunaitwa Waisilamu kwa maana mbili:- 1 --kwasababu ni wanyenyekevu, 2-- kwasababu ya kushika dini hii yenye jina Islamu iliyokamilika chini ya mtume (saw) ikiwa na nguzo zake 5..

Ndio maana nasema Uisilamu au mfumo wa maisha wa nabii Ibrahimu ambao haukuwa kamili ni huo wa aina ya kwanza ambao haukujengwa katika nguzo tano za Uisilamu huu wa mtume (saw) japokuwa unakurubiana.

Watu wasiokuwa waisilamu wanahitaji maelezo kama haya ili waelewe kwani mtu ukimwambia Nabii Ibrahimu alikuwa Muisilamu bila kumpa maelezo kwamba alikuwa Muisilamu kwa namna ipi, yeye akili yake moja kwa moja inampeleka kwamba Muisilamu ni mfuasi wa dini hii ya kiisilamu iliyokamilika kwa mtukufu mtume (saw) ambayo mfuasi wake lazima atamke shahada, Aswali sala 5, atoe zaka, afunge Ramadhani, Ahiji makka ambapo kwa manabii waliopita hawakufanya baadhi ya nguzo.

Hivyo unapozungumzia juu ya dini na Uisilamu wa.manabii waliopita inahitajika ufafanuzi ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza.
Mkuu!Kuwa makini sana na hawa watu wa upande wa pili.
Angalia mfano huu:-
 
Ibrahim alimzaa Ishmael,
Ishmael akamzaa KEDARI,
KEDARI akazaa wana 12 ambao ndiyo makabila 12 ya waarabu (Waislamu).
So, kama Ibrahim ndiye chanzo cha hao Waislamu, jibu ni wazi tu kuwa alikuwa Muislamu.


[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaani kirahisi tu!.
Huu ni upotoshaji.
 
Hata Tunapomsalia Mtume Tunasema:

Allahumma Sali 'alaa Muhammad wa'alihy Muhammad Kamma Salayta 'alaa Ibrahim wa'alihy Ibrahim....na Salam kama inavyoendelea
Hii manake kulikuwa kuna namna ya kumsalia Nabii Ibrahim wakati Alipokuwa Mtume wa Allah

So Ibrahim Alikuwa ni Muislam
 
Mkuu mimi hapo sijaelewa kitu.
Hapo linaoneshwa jina Mahammad katika lugha ya asili yaani Kiebrania.Lakini kwenye mstari huohuo ulitafsiriwa kwa lugha ya Kiingere,wameweka tafsiri yao na hivyo kulificha jina Mahammad.Iangalie hiyo video.

Nini maana yangu sasa,maana yangu ni kukujulisha kuwa uwe makini katika maandiko ya asili na majina kwa maana tafsiri ya jina ulenga kupotosha wakati mwingine.
 
Hili swali nalikalibisha tu,kwa watu wenye uelewe wa mambo ya Dini.

Huyu ni nabii na mtume wa Mwenyezi Mungu, ambaye anakubaliki na Dini zote, kuanzia Uyahudi, Ukristo mpaka Uisilamu, na hawa wote ibada zao zimetofautiana.

Je, niwapi wanaomfata?
nendeni jumuia watakufunza
 
Hivi ni vichwa vya Train vyenye njia tofauti za kuendesha injini,zinazotofautiana kutokana na wakati.

Kichwa cha kwanza kiliitwa steam Locomotive engine,kilitumia mvuke miaka ya 1800 hukoo!.
Kichwa cha pili, kinaitwa Deasel Locomotive engine ambacho kiligunduliwa miaka ya 1900 huko na
Kichwa cha tatu,kinaitwa electrical locomotive engine.

Mkuu!Pamoja na vichwa hivi kutofautiana katika mfumo wa kuendeshea ingini,bado vyote vinapita katika njia yenye kufanana yaani Rail.

Sasa na katika Uslamu ni hivyohivyo kwa maana mitume wote walipita katika Dini(njia) ya Uslamu lakini kwa nguzo tofauti.

View attachment 2588718View attachment 2588719View attachment 2588720
"bila shaka katika haya kuna mazingatio (dalili/mifano ya wazi kabisa) lakini je yupo katika wao anayetafakari? ni wachache sana wenye kukumbuka na kutafakari"

nimejikuta nimeandika maneno hayo yanafanana fanana na quran kidogo japo sijui ni sehemu gani katika quran
 
Mkuu, very nice.

Tafadhali nitafutie ile aya ambamo Allah anasema maneno yanayofanana na haya; "Amewausia manabii dini--- ya kwamba wasimshirikishe Allah na chochote---"

Hiyo aya inayo maneno yanayofanana na hayo niliyoyaandika ila nimesahau mtiririko wake na ipo wapi katika Qur'an , hiyo aya ndiyo inajibu nini maana ya neno الدين lilotumika hapo kwenye hiyo aya uliyoileta kwani neno Dini, mbali, na maana ya Religion linazo maana zingine nazo waweza kuzipata kulingan na context ya aya.

Mfano katika 1:5,
ملك يوم الدين Maliki yaumi din, yaani; Mmiliki wa SIKU YA MALIPO, hapo utaona neno "Dini" limetafsiriwa kuwa "malipo" ya siku ya Qiyama..
Quran hii iliyoandikwa kwa lugha ya kiarabu haitafsiriwi hivyo, mujitahid yes, lakini ongeza juhudi ya kuijua.
 
"bila shaka katika haya kuna mazingatio (dalili/mifano ya wazi kabisa) lakini je yupo katika wao anayetafakari? ni wachache sana wenye kukumbuka na kutafakari"

nimejikuta nimeandika maneno hayo yanafanana fanana na quran kidogo japo sijui ni sehemu gani katika quran
[emoji23][emoji23][emoji23] Hayo maneno Mwenyezi Mungu ameyaleta katika Aya nyingi tu ndani ya Quran.
 
Kwa mujibu wa Quran kitabu cha mwisho kutoka kwa Mwenyezimungu, Ibrahim alikuwa Mwislamu akiabudu Mungu mmoja.

"Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina." Quran 3:67

Aidha Uislamu ndio uliofunuliwa kwa mitume mingine.

"Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi." Quran 4:163
 
Msingi wa hizo dini korofi tatu ni maandishi ya gospels ambazo zilikuwepo luluki.

Kitu pekee ambacho gospel imesaidia dunia ni kuleta dhana ya mungu mmoja aliye mbinguni.

Tatizo la awali kabla ya gospel kukusanywa na kuandikwa kwa vitabu vya dini. Ilikuwa fujo kwenye kuabudu japo watu waliamini mungu mmoja na kufuata hizo gospel ila kila mtu alifanya mambo kwa mtindo wake.

Unakuta utaratibu wa kanisa A na B mtaa wa pili kwenye kufanya ibada ni tofauti. Ukienda mile 100 ndio kabisa na si ajabu hiyo gospel yenyewe washaichakachua wana version yao. Kwa hivyo kukawa na version nyingi sana za story za Abraham, Adam and Eve na wengineo.

Ilikuwa ivyo mpaka Constantine alipo tawala Roman emoire na kuwaita wahubiri na kuwaambia waandike biblia moja ambayo kila mtu ataifuata na kuwe na namna sahihi ya kufanya ibada. Sasa kabla ya biblia kuandikwa hao maaskofu, ilibidi wajadiliane na wakubaliane gospel zipi muhimu kwao na version zipi ni muhimu kwa dini yao kwa kupiga kura.

You get the ideas na Jews na waislamu na wenyewe wakaenda na mtindo huo huo kwenye kuandika vitabu vyao kuchukua versions zinazowafaa wao. Na kuna versions luluki inasadikika bado zipo ambazo hakuna dini ilizi adapt.

Hizo ndio sababu mitume wote wa hizi dini tatu korofi ndio wale wale; ila version zao ndio zinapishana na huo ukorofi mpaka leo unaendelea; mada hii ni kielelezo cha hizi dini tatu korofi.
 


A very interesting documentary to open minded people wishing to understand the sources of the so called holy books.
 
Back
Top Bottom