Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Baada ya siku kadhaa mbele, utasikia Hakimu aliyetoa hiyo hukumu amekula uteuzi!! Maana hapa ndipo tulipofikia kama Taifa.
Kama anastahili asiteuliwe kuogopewa kusemwa "...ni sababu ya ileeee hukumu"?!!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]
 
Mchungaji Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa Mnatuona Manyaji amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali.

Pia soma: 'Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi' Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi
Acha tutafika taratibu maan hili litawagharimu!! Kuna yule ambae mchungaji au mtumishi wa MUNGU akimkosoa alikua anawakamata na kuwahoji uraia but mwisho wake unajulikana!! Jifunzeni kwa herode!!
 
Unaweza kuabudu 'roho' ukiwa nyumbani kwako.

Kitendo cha kutenga eneo la pamoja kwa ajili ya huduma sio tu za 'kiroho' tayari mnafanya makutano yanayohitaji ithibati ya ulinzi wa watu wanaokutana.

Kwanini usajili wa nyumba za ibada unafanyika Wizara ya Mambo ya Ndani wakati usajili wa Asasi za Kiraia unafanyika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, hali ya kuwa na dini ni miongoni mwa Asasi za Kiraia?
Akikujibu plz nitag [emoji120][emoji1666][emoji2956]
 
Siku zite iko hivi, Ukiwa Mstaarabu
hata kama una mapungufu watu hukupuuza ila ukijikuta mjanja watu watataka wakuonyeshe kua hujui.
Ukiamua kukosoa wenzio hakikisha uko smart.
Uko ndani ya gari halafu unaanzisha ugomvi wa MAWE?!!! [emoji1787][emoji1787]
 
Hewaaa....

Imani za MIZIMU hazina shida wala tabu....

Ila.....

Hizi ABRAHAMIC FAITH ndizo za kuzidhibiti.....[emoji120]

Wao ni tofauti sana sana na hizo za asili....

Za asili hazina "connection worlwide"....[emoji1787]
Utajuaje kama hii sio version yangu ya Abrahamic Faith..., Yaani Version 2:0 ?!!; Point yangu kubwa hapa tunaweza ku-open a Can of Worms Mtu ashitakiwe kwa kuvunja sheria za nchi ila sio kuomba ruhusa kufanya kile ambacho yeye na wenzake kama yeye wanaona ni sahihi....
 
Vibali vivunje haki za kikatiba na kibinadamu ?!!![emoji15][emoji1787][emoji1787]

Unaleta fikra isiyo na mashiko.....

Kila eneo la kibiashara linahitajika vibali....

Wahandisi ,matabibu wa kizungu na KIENYEJI ,wanasheria ,wahasibu.....wote hawa vibali vinawahusu....yaani isiwe tu kwa nyumba za ibada ?!!! [emoji15][emoji15][emoji1787]

Fikra ya ajabu kabisa

Usichoelewa ni kwamba, biashara haina protection kama ya "separation of state and religion".

Hao wahandisi, matabibu, waganga wa kienyeji, wanasheria, wahasibu etc, wote hawana protection ya "separation of state and religion"

Dini ina hiyo protection.

Ndiyo maana biashara inatozwa kodi, dini haitozwi kodi.

Nyerere alikuwa anaelezea hoja ya serikali kujua idadi ya Watanzania kwa mujibu wa dini zao, akasema serikali haihitaji kujua watu kwa dini zao, kama mtu anataka kujua idaid hiyo aende kwenye nyumba za ibada.

Alielewa separation of state and religion.

Sasa, hatuoni hizi habari za kusajili nyumba za ibada ni kurudi kule kule alikokataa Nyerere kwenye habari ya serikali kujiingiza katika dini?

Kwa nini serikali ilazimishe kusajili nyumba za ibada?
 
Mkoa huu wa Mbeya ukikamatawachungaji na waganga wasio na vibali gereza lipi litatosha?
 
Mchungaji Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa Mnatuona Manyaji amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali.

View attachment 2766355


================== ==================
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile (39), baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Manyaji”, amehukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kosa la kuendesha huduma ya kiroho bila kibali.

Akizungumza na JamiForums, Wakili Boniphace Mwabukusi amesema “Kweli amehukumiwa lakini Mchungaji alifuata machakato wa kuomba vibali japo Serikali ndio ilikuwa ikichelewesha ukamilishwaji, pia Sheria inasema mtu ambaye yupo katika mchakato wa maombi hawezi kushtakiwa."

Ameongeza "Adhabu aliyofungwa nayo ina faini na kifungo, Hakimu ametoa adhabu ya kifungo bila faini, tunatarajia kukata rufaa Jumatatu (Oktoba 2, 2023)."


=================​
Pia soma: 'Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi' Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi
Je, anayeendesha kilabu ya pombe au madanguro bila kibali anafungwa miaka mingapi?
 
Ukweli ni kwamba wameshindwa kuzivumilia spana za Mchungaji.
 
mbarikiwa ameyataka mwenyewe, Mungu alimwita awe mwimbaji, na alikuwa na nyimbo nzuri, yeye ameng'ang'ania kuwa mchungaji ameacha uimbaji. sidhani kama Mungu yu pamoja naye kwenye hilo, na hata akiwa naye basi for a purpose.
 
Back
Top Bottom