Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Hivi misikiti lazima ipate vibali vya serikali hata Ile midogo isiyo ya ijumaa?

Serikali ya Samia mnataka wenyewe maswali kama haya muanze kuita watu wachochezi wa kidini.
 
Huyu mchungaji na mwanae wachunguzwe siyo bure kuna kitu au alitumwa na babake ule wimbo?
 
Wenyewe si walisema wanaonwa Manyani.. haya sasa wameyatimba.

Mie nilichojifunza katk hii Dunia hasa hapa Tanzania hakuna lolote utakaloweza kulifanya ukatunishiana kifua na MAMLAKA. never, hakuna support yoyotee ile ukijifanya kujitoa muhanga hakuna hata mmoja atakaekukumbuka kipindi unanyea ndoo. Majitu ni manafki.

Tafuta hela jenga familia yako tulia kimya.
 
Asiye na imani ya dini ndiye amekuwa mkweli na mpenda haki kuliko wenye dini zao wanaofunga wenye dini wenzao.
Mkuu,

Mimi naangalia haya mambo kwa mawanda mapana zaidi.

Kiufupi, uhuru wa kuabudu na uhuru wa kutoabudu ni pande mbili za sarafu ile ile moja, uhuru kwenye ibada na freedom of conscience.

Hata kama mimi siamini dini, nasimamia haki za watu kuwa huru katika mambo ya ibada, wawe huru kuabudu au kutoabudu, wanavyotaka.

Nikiruhusu uhuru wa kuabudu wa mtu uingiliwe na serikali, kwa kujua au kutojua, nitakuwa nimeruhusu hata uhuru wangu wa kutoabudu uingiliwe na serikali vile vile.

Ukishaanza kuiruhusu serikali ilazimishe kusajili nyumba za ibada, neno ilazimishe ni muhimu sana hapa, ndiyo utakuwa umeanza kupiga hatua ya kuelekea kuiruhusu serikali kusema ni lazima kila mtu ahudhurie nyumba za ibada zilizosajiliwa na serikali, wakati kuna watu hatutaki kuhudhuria nyumba yoyote ya ibada.

Kwa hivyo, mtu ambaye hana dini, na anafurahia habari hii kwa sababu hana dini, hajaelewa kua habari hii inaweza kumuathiri hata yeye asiye na dini.
 
Siku zite iko hivi, Ukiwa Mstaarabu
hata kama una mapungufu watu hukupuuza ila ukijikuta mjanja watu watataka wakuonyeshe kua hujui.
Ukiamua kukosoa wenzio hakikisha uko smart.
Ni ujinga serikali kuoneshana ujanja na raia wake, wakati umeme umemsinda.
 
Uko sahihi sana mkuu
 
Unabii unaenda kutimia vile vile,

Anaonekana kiongozi aliyeshikilia kitabu akiingia ndani ya Kanisa,na Kutoa maelekezo.

BAADAYE kiongozi huyo huyo anarudi kukabidhi tena Kwa Kanisa..

Tusubiri.
 
Yaani mchungaji kufungwa jela ndo iwe sababu tosha ya kumuondoa Samia madarakani?

Zipo sababu za msingi sio hii.
Ataondolewa tu maana mwenye Mamlaka hapendi uonevu usio na sababu na Mwenyezi Mungu anawachukia sana wapumbavu.
 
Huyu bibi amedhihirisha anachoweza kufanya vizuri ni kufunga ushungi tu.

Mbona matapeli kibao wako kwenye hizo nyumba za ibada.

Hivi mfano mimi kwa umri huu na akili zangu utaanzaje kunishawishi nikuamini eti Masanja Mkandamizaji nae ni mchungaji na ana kanisa na wapo wanaomuamini?
 
Aiseeee,jamaa hanaga woga.

Si wangemhukumu kifo tu.

Maana,MAHAKAMA zinapangiwa Nini Cha kufanya.

Ila Richa ya usomi wao wote,hawana tofauti na ngumbalo.

Aibu kwao,matherfanta kwa wote waliohusika na mchakato.

Ila WAMEYAKANYAGA.

Mavi hayafichwi kwenye mfuko WA KOTI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…