Mohamed Abubakar
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 984
- 1,179
Mna hakika Sifa Bujune (25) ni mwanawe na sio kondoo wa mchungaji
39 - 25 = 14.
Je ni kweli mchungaji kapata mtoto akiwa nae mtoto?
Walianza kucheza lini.
Wakaoana lini.
39 - 25 = 14.
Je ni kweli mchungaji kapata mtoto akiwa nae mtoto?
Walianza kucheza lini.
Wakaoana lini.
Mchungaji Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa "Mnatuona Nyani tu" amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali.
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile (39), baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”, amehukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kosa la kuendesha huduma ya kiroho bila kibali.
Akizungumza na JamiiForums, Wakili Boniphace Mwabukusi amesema “Kweli amehukumiwa lakini Mchungaji alifuata machakato wa kuomba vibali japo Serikali ndio ilikuwa ikichelewesha ukamilishwaji, pia Sheria inasema mtu ambaye yupo katika mchakato wa maombi hawezi kushtakiwa."
Ameongeza "Adhabu aliyofungwa nayo ina faini na kifungo, Hakimu ametoa adhabu ya kifungo bila faini, tunatarajia kukata rufaa Jumatatu (Oktoba 2, 2023)."
Pia soma: 'Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi' Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi
=================