Baba yangu alipomuacha mama akatafuta mwanamke mwingine nilimchukia sana wakati ule,hivi Sasa ndiyo naelewa

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Nisamehe sana baba ,wakati ule nilikuwa bado mdogo sikujuwa jambo lolote!

Wakati tunakuwa Mimi na ndugu zangu tulikuta mzee (baba) ameacha na mama,binafsi kwakuwa nilikuwa Nina shinda na mama yangu mara zote,alikuwa akiniambia mambo mengi ya ovyo kuhusu Baba yangu

Baba yangu yeye hajawahi kabisa kuniambia jambo lolote kuhusu mama yangu pamoja na Kuwa karibu naye!,Mwanzo kabla sijakuwa na ufahamu mkubwa nilidhani Baba yangu ni mwenye makosa lakini baada ya Kuwa mtu mzima na kuingia kwenye mahusiano na kupata watoto ndipo nimeelewa ya kwamba Baba yangu hakuwa na kosa,kumbe tatizo lilikuwa Kwa Bi mkubwa (mama).

Yaani mambo yote aliyokuwa akiniambia mama nimegundua ilikuwa ni uongo,zilikuwa njama na hila za mama ili tumchukie mzee,baada ya kuishi na mwanamke ndiyo nimekuja kugundua hili jambo !

Eeeh Baba yangu nisamehe!

Haupo Duniani lakini maneno yako bado nayakumbuka ule mwaka 1997,uliniambia ya kwamba "Wanawake Duniani wapo Kutuongezea matatizo siyo kupunguza matatizo "😭

Rest in peace dady!
 
Wewe Dokta Pori umeelewa kilichoandikwa?
Nimeelewa sana. Unless unaangalia mambo kwa ufinyu.

Huyu Mwamba anataka kulinganisha aliyopitia akiwa mtito hadi Baba yake kumwacha mama yake. Na sasa anataka kusema mke wake naye ameanza visa na ku conclude kwamba huenda ndio maana Baba yake alimwacha Mama yake.

Hii ni ku compare vitu visivyofanana.
 
Nisamehe sana baba ,wakati ule nilikuwa bado mdogo sikujuwa jambo lolote!
UKWELI siku zote huwa unachelewa tu kufika, ila ni lazima Utafika. Huwa ni swala la muda tu.

Hili ulilofanya ni hatua kubwa sana kwenye mafanikio yako katika ulezi wa familia, Litafanya ufanye maamuzi sahihi kama Baba kwakuwa umeshajua "What it takes to be a FATHER".

Be a Man.
 
Wewe Dokta

Nimeelewa sana. Unless unaangalia mambo kwa ufinyu.

Huyu Mwamba anataka kulinganisha aliyopitia akiwa mtito hadi Baba yake kumwacha mama yake. Na sasa anataka kusema mke wake naye ameanza visa na ku conclude kwamba huenda ndio maana Baba yake alimwacha Mama yake.

Hii ni ku compare vitu visivyofanana.
Ukipigwa limbwata hauwezi kuona ya TUKANA UONE.
 
Same story na Familia yangu.

Kuna siku nikiwa na miaka 6, nilimuuliza baba hv ni kwann ulimuacha mama, ukatufufuza nyumbani, baba alijibu wewe bado mdg ukikua utajua.

Sasa nimekua, najua mengi kuhusu wanawake na familia. Nabaki kusema R.I.P my dady.

Japo kwa upande wa mama alijitahidi kunipa story za kufanya nimchukie mzee na upande wa baba kitu ambacho kamgu hakikufanya kazi. Japo sipo nao karibu kivile, lkn siwachukii.
 
Nisamehe sana baba ,wakati ule nilikuwa bado mdogo sikujuwa jambo lolote!

Wakati tunakuwa Mimi na ndugu zangu tulikuta mzee (baba) ameacha na mama,binafsi kwakuwa nilikuwa Nina shinda na mama yangu mara zote,alikuwa akiniambia mambo mengi ya ovyo kuhusu Baba yangu

Baba yangu yeye hajawahi kabisa kuniambia jambo lolote kuhusu mama yangu pamoja na Kuwa karibu naye!,Mwanzo kabla sijakuwa na ufahamu mkubwa nilidhani Baba yangu ni mwenye makosa lakini baada ya Kuwa mtu mzima na kuingia kwenye mahusiano na kupata watoto ndipo nimeelewa ya kwamba Baba yangu hakuwa na kosa,kumbe tatizo lilikuwa Kwa Bi mkubwa (mama).

Yaani mambo yote aliyokuwa akiniambia mama nimegundua ilikuwa ni uongo,zilikuwa njama na hila za mama ili tumchukie mzee,baada ya kuishi na mwanamke ndiyo nimekuja kugundua hili jambo !

Eeeh Baba yangu nisamehe!

Haupo Duniani lakini maneno yako bado nayakumbuka ule mwaka 1997,uliniambia ya kwamba "Wanawake Duniani wapo Kutuongezea matatizo siyo kupunguza matatizo "😭

Rest in peace dady!
Bora umelitambua hilo.
 
Jamaa unatumia hisia sana hauko Logical ...!!

Makosa ya mkeo unahisi ndio sawa na aliyoyafanya mama yako kwa baba yako ...!!

Yaani kiufupi, kwasasa hivi mkuu unaamini ndoa zote zinazovunjika, Mwanamke ndio tatizo...!!

Tumia akili sio hisia mkuu ...!! Be smart
 
Nimeelewa sana. Unless unaangalia mambo kwa ufinyu.

Huyu Mwamba anataka kulinganisha aliyopitia akiwa mtito hadi Baba yake kumwacha mama yake. Na sasa anataka kusema mke wake naye ameanza visa na ku conclude kwamba huenda ndio maana Baba yake alimwacha Mama yake.

Hii ni ku compare vitu visivyofanana.
In short hayuko Logical bali Emotional....
 
Baba akiwa na mke mwingine haina noma ila mama akitaka kuleta baba mwingine lazima ulete noma sisi watoto wakiume huwa hatutaki watu wazoee mama zetu kabisa tunawivu nao mbaya kabisa wivu wa upendo.
 
Mara nyingi sis wanaume ni mara chache sana kuwajaza sumu watoto wachukie mama zao, ila wanawake wengi ni kawaida yao.
 
Mambo ya wazazi wako waachie wenyewe hebu zingatia uzazi wako mkuu..Jenga familia yako kwanza kwa mtazamo wako
 
Mara nyingi sis wanaume ni mara chache sana kuwajaza sumu watoto wachukie mama zao, ila wanawake wengi ni kawaida yao.
Ndivyo walivyoumbwa, na hawatabadilika....kizuri watoto wakikua wanakuwa wapole hasa wa KIUME, wa kike imekula kwa BASHA wake.......sababu maisha yake ni machale machale ya kuachwa....so wanakuwa na wivu usio na kichwa wala miguu....
 
Back
Top Bottom