Baba yangu mzazi amepangisha chumba changu

Baba yangu mzazi amepangisha chumba changu

Habari zenu ndugu zangu, naandika nikiwa na hasira kali sana juu ya baba yangu mzazi, mimi ni kijana wa umri wa miaka 48, sijaoa bado ila nina mtoto mmoja, ambaye yupo kwa bibi yake upande wa mama yake.

Mwaka huu mwezi wa tano niliondoka nyumba rasmi baada ya kuona baba yangu ameanza manyanyaso mpaka kufikia hatua ya kuwa nanyimwa chakula, kwa kumuamuru mfanyakazi wa ndani asiwe anapika chochote kile asubuhi na mchana. Baada ya kuona hiyo hali inazidi kuwa mbaya kwangu nikaondoka kabisa nyumba mwaka huu mwezi wa tano.

Nikaenda kupanga chumba maeno ya Mabibo Relini, nimekaa huko kwa muda wa miezi 5 nikiwa nabangaiza hapa na pale, ndugu zangu nikiri kabisa kuwa maisha yamekuwa magumu sana kwangu, nimeamua week hii kurudi nyumbani. Cha kushangaza nafika nyumbani na kukuta chumba changu nilichokuwa nakaa amepangishwa mtu, nilipata hasira sana na kumuambia mzee mimi kama sio mtoto wake aseme.

Ndugu zangu iliniuma sana mzee kusema kuwa ndio sio mtoto wangu na naomba uondoke hapa kwangu haraka sana, anadai sijui amepoteza pesa zake nyingi kunisomesha mpaka level ya degree ila sina msaada wowote.

Nikamuambia kuwa kunisomesha sio tatizo kama ningekuwa sina juhudi za kusoma kwa bidii ningepata hata hiyo degree au kwa kuwa yeye kutoa pesa ndio imekuwa ni sehemu ya kuninyanyasa?

Niliamua kwenda moja kwa moja kwa mjumbe wa nyumba kumi wa hapo mtaani kwetu ila nilichogundua mjumbe na mzee wangu lao ni moja maana nae anadai sina haki yoyote kwa sasa.

Ndugu zangu naadika huku machozi yananitoka naombeni ushauri wangu nataka kusogea ngazi za juu zaidi, ili kupata haki zangu za msingi, maana mzee wangu imefikia hatua amewaambia mpaka askari wa mtaani kwa jina la sungusungu kuwa nikija kwake awape taarifa waje wanitoe kwa nguvu.

Muda huu nimekuja kwa rafiki yangu hapa kujiegesha kidogo huku natafakari hatua za mbele zaidia za kuchukua. Karibu kwa ushauri wenu ndugu zangu.
Ha ha ha !
Nimeanza kusoma tu, nikacheka kwa nguvu.
Ati kijana wa miaka 48, zee zima unamtegemea babaako, yeye ana miaka mingapi hadi akupe uji kwa kijiko cha kimaisha.
 
Mimi nimeomba ushauri badala yake naanza kushambuliwa, nilicho gundua watu wa JamaiiForum ni wivu tuu umewajaa kabisa, Unakuta jiru lipo dar es salaam limepanga ila likisikia sisi wazazi wetu wana nyumba linaanza uona wivu na kuanza kutukana na kutoa maneno ya kashfa
 
Kama unakaa kwa wazazi na una uwezo wa kuwalisha, unashindwa kupanga ili uwe huru zaidi? Mf. Ukioa ukiwa kwa wazazi, ugomvi na mawifi utaweza?

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom