Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...


Siku nyengine Zubeda msikurupuke mie nina dada yangu ameathirika alinipigia simu kwa ushauri nikamuuliza je huyo babu wewe yale maji mnayokunywa masafi? Pili vikombe vya kushare si ndio mwanzo wa kupeana TB?, Tatu nikamuuliza kweli unadhani Ukimwi unatibiwa huko? Nikamwambia kaa utulie uendelee na shughuli zako mpaka serikali itakapothibitisha kama kweli hiyo dawa inafaa au la ili ukifa tuishtaki serikali kwa udanganyifu. Pole sana dada innallilahi waina ilaihi rajiun!!!!
 
Pole kwa msiba wa shangazi yako, lakini mimi sioni kwa nini serikali mchukulie hatua kwa kifo cha shangazi yako, kwani ripoti ya daktari inaonesha kufa kifo chake kimesababishwa na dawa ya mchungaji? na pili mbona kuna watu wengi tu wamekunywa hiyo dawa na wakarudi majumbani kwao salama? na mwisho ni lini mchungaji huyo aliweka bango kutangaza kuwa anatibu kwa dawa yake hiyo, maana kwa mujibu wa habari zilizopo ni kuwa habari za kuwepo dawa hiyo zilizambazwa na wagonjwa waliokunywa na kupona na sio mchungaji huyo, kwa maana hiyo kusema yeye ndio anaesababisha mkusanyiko huo pale kijijini kwake mi naona ni kama kumuonea tu, watu wanaenda wenyewe kwa shida zao nae hawazi wafukuza na ndio maana ametoa wito kwa serikali imsaidie kupeleka ulinzi na kujenga vyoo vya muda nakurekebisha barabara iendayo huko, kafanya yote haya kwa kujali maslahi ya wagonjwa haohao! najua inauma sana kumpoteza mpendwa wenu, lakini pia si vyema kutupa lawama kwa mchungaji huyo maana yeye alimpa shangazi yako dawa kwa nia njema tu, ni wagonjwa wangapi wanakufa mahospitalini baada ya kupata tiba na wala hatusikii ndugu na jamaa wakiomba serikali ichukue hatua! Kuwa mvumilivu kazi ya Mungu haina makosa! Inna lillah wa inna lillah lajuu'um
 
pole kwa msiba huo mkubwa

kwa hiyo unasema amefariki kwa sababu;

a) aliishi akiwa mgonjwa wa kisukari kwa miaka 20
b) amekunywa dawa ya babu wa loliondo
c) amekunywa dawa ya babu na alikuwa ana kisukari

ripoti ya post-mortem (kama imefanyika) inasemaje?

again, pole sana na may she rest peacefully. Nina kisukari for about 10 years and everybody in the family is urging me to go!
 
Tumetoka kwenye udongo na tutarudi kwenye udongo!kufa ni wajibu kwa binadamu!wakati wake ulifikia wa kifo
 
RIP Shangazi. Inasikitisha lakini tungekuwa na taarifa ya daktari ingekua much better
 
Wananchi tuwe macho na hawa WACHUNGAJI NA MAPADRE wenye kudai kutibu maradhi baada ya kuoteshwa ndoto na Mungu wakiwa wamelala!!!!!!!!!

Peleka maiti ya shangazi yako kwa Mganga Majungu wa Selous atamfufua.
 
Pole sana!
Ushuhuda wa wengi umeonesha ni dawa imeponya wengi. Unaweza kumlaumu mchungaji endapo tu utaelekeza fikra kuwa Mchungaji anatibu kama uwashavyo bulb ya umeme pale nyumbani yaani unabonyeza switch na taa inawaka instantly lahasa dawa hiyo inatibu kama ilivyo dawa nyingine yaani inachukua siku kadhaa hd mgonjwa ku-recover.

My take:
upo uwezekano wa kifo hicho kuwa kimesababishwa na uchovu maradufu ambao umesababishwa na safari ndefu, huduma duni na kusubiri muda mrefu kupata matibabu.

Usielekeze lawama kwa mchungaji mtoa tiba, angalia upande mwingine pia, na huko kukamatwa unakosema kutasababisha wagonjwa wenye kuhitaji tiba watapoteze maisha kwa sababu ya kukosa tiba kutoka kwa mchungaji unayetaka akamatwe.
 
Yu masti bi jiniaz.
 

Hapo kwenye rangi ndo kuna kasoro: Kuna harufu ya UDINI. Nani alikulazimisha uende huko kutibiwa?? ulivutwa kwa mnyororo. Mchungaji amekuambia dawa yake inatibu kutegemea na imani ya mgonjwa-na hilo ulijua-je unajuaje shangazi yako alikuwa na imani ya dawa?? mbona mimi jirani yangu alikwenda akiwa anaumwa na yupo anajieeleza kuendelea vema!!! kwa sasa wakati uchunguzi wa kisayansi haujafanywa kuhusu ubora na uhahakika wa dawa, yeyote aendapo kutibiwa kwa dawa hiyo aende kwa imani yake na awe tayari kubeba dhamana ya mafanikio au madhara yeye mwenyewe (he/she has to take risk or responsibility him/herself).
 
Mada haina ukweli wowote bali kuna harufu ya udini. Hivi unajisikiaje kumzushia ndugu yako kafa kisa tu kueneza udini?
 
Pole sana.ila hata mahospiali makubwa duniani wagonjwa wanakufa.Haina maana kufikiri kwamba ukinywa dawa ya babu hufi.
La msingi mfanye uchunguzi wa hospitali kujua chanzo cha kifo.
 
nadhani alichojaribu kueleza kaka ni msisittizo tu hana uhusiano wa moja kw moja na mskitini anajaribu kueleza hisia zake ni jins gani amekwazwa na jambo hli,tumuelewe wana JF.
Mkuu.
Usimtete huyu ndugu..aje mwenyewe aeleze alikusudua nini au afute usemi huu. Kwa nini hakusema hekalu la wayahudi au hekalu la wahindu au kanisani?

Kumtetea wakati anaendeleza stereo typing sio vizuri.
 
Shukuru shangazi kafa maana gharama za maisha zitapungua
 
Kweli?? Patachimbika ..Wengine tumetoka Malawi ndo tuko njiani..Kama ni vyoo...Andengenye na vijana wake wapiga mabomu si waende kuchimba vyoo.....
 
Yale yale, kutoka kwa mtu yule yule, na upande ule ule!
 
Kama kweli shangazi yako kafa nampa pole. Nasema hivyo kwa sababu sina uhakika na dhamira yako.
Unachopaswa kujua ni kimba sii kila anywae dawa hupona, kwani kama ingekuwa hivyo hospitali zisingejenga vyumba vya kuhifazi maiti.
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…