Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Naiomba Serikali imkamate huyu Mganga wa Kienyeji kwa kusababisha vifo vingi vya Wagonjwa ktk wiki hii!! ni jana tu nimemzika Shangazi yangu aliyefariki huko Loliondo mara tu baada ya kunywa kikombe kimoja cha dawa ili kutibu gonjwa la kisukari!!! Marehemu Shangazi langu aliishi na ugonjwa huo zaidi ya miaka 20 lakini alipoambiwa kuna Mchungaji anatibu papohapo tulimpeleka Shangazi na kupewa hiyo dawa na tukiwa njiani kurudi nyumbani Shangazi aliaga dunia!!

Tunasikitika kumpoteza Shangazi wetu mpendwa na nimesikia kuna wagonjwa wengi waliofariki mara baada ya kunywa dawa za huyo Mchungaji na kunipa hofu na kukumbuka kisa cha Mchungaji mmoja huko Uganda miaka ya 90 alichoma Kanisa Moto na kuteketeza maelfu ya Waumini waliokuwa humo ndani kwa kudai alioteshwa na Mungu kuwa wakifia Kanisani kwa kujichoma moto basi wataenda mbinguni!!!

Naiomba Serikali imchukulie hatua kali huyu Mchungaji wa Loliondo kwani amesababisha madhara makubwa kwa Wananchi na hata kuharibu mazingira kwa kuwakusanya maelfu ya watu mahali finyu bila choo wala mahala pa kulala na pa kula!!

Familia yetu iko mbioni kushika wakili ili tumfungulie kesi kwa kusababisha kifo cha Shangazi wetu mpendwa!

Wananchi tuwe macho na hawa WACHUNGAJI NA MAPADRE wenye kudai kutibu maradhi baada ya kuoteshwa ndoto na Mungu wakiwa wamelala!!!!!!!!!

Siku nyengine Zubeda msikurupuke mie nina dada yangu ameathirika alinipigia simu kwa ushauri nikamuuliza je huyo babu wewe yale maji mnayokunywa masafi? Pili vikombe vya kushare si ndio mwanzo wa kupeana TB?, Tatu nikamuuliza kweli unadhani Ukimwi unatibiwa huko? Nikamwambia kaa utulie uendelee na shughuli zako mpaka serikali itakapothibitisha kama kweli hiyo dawa inafaa au la ili ukifa tuishtaki serikali kwa udanganyifu. Pole sana dada innallilahi waina ilaihi rajiun!!!!
 
Pole kwa msiba wa shangazi yako, lakini mimi sioni kwa nini serikali mchukulie hatua kwa kifo cha shangazi yako, kwani ripoti ya daktari inaonesha kufa kifo chake kimesababishwa na dawa ya mchungaji? na pili mbona kuna watu wengi tu wamekunywa hiyo dawa na wakarudi majumbani kwao salama? na mwisho ni lini mchungaji huyo aliweka bango kutangaza kuwa anatibu kwa dawa yake hiyo, maana kwa mujibu wa habari zilizopo ni kuwa habari za kuwepo dawa hiyo zilizambazwa na wagonjwa waliokunywa na kupona na sio mchungaji huyo, kwa maana hiyo kusema yeye ndio anaesababisha mkusanyiko huo pale kijijini kwake mi naona ni kama kumuonea tu, watu wanaenda wenyewe kwa shida zao nae hawazi wafukuza na ndio maana ametoa wito kwa serikali imsaidie kupeleka ulinzi na kujenga vyoo vya muda nakurekebisha barabara iendayo huko, kafanya yote haya kwa kujali maslahi ya wagonjwa haohao! najua inauma sana kumpoteza mpendwa wenu, lakini pia si vyema kutupa lawama kwa mchungaji huyo maana yeye alimpa shangazi yako dawa kwa nia njema tu, ni wagonjwa wangapi wanakufa mahospitalini baada ya kupata tiba na wala hatusikii ndugu na jamaa wakiomba serikali ichukue hatua! Kuwa mvumilivu kazi ya Mungu haina makosa! Inna lillah wa inna lillah lajuu'um
 
pole kwa msiba huo mkubwa

kwa hiyo unasema amefariki kwa sababu;

a) aliishi akiwa mgonjwa wa kisukari kwa miaka 20
b) amekunywa dawa ya babu wa loliondo
c) amekunywa dawa ya babu na alikuwa ana kisukari

ripoti ya post-mortem (kama imefanyika) inasemaje?

again, pole sana na may she rest peacefully. Nina kisukari for about 10 years and everybody in the family is urging me to go!
 
Tumetoka kwenye udongo na tutarudi kwenye udongo!kufa ni wajibu kwa binadamu!wakati wake ulifikia wa kifo
 
RIP Shangazi. Inasikitisha lakini tungekuwa na taarifa ya daktari ingekua much better
 
Wananchi tuwe macho na hawa WACHUNGAJI NA MAPADRE wenye kudai kutibu maradhi baada ya kuoteshwa ndoto na Mungu wakiwa wamelala!!!!!!!!!

Peleka maiti ya shangazi yako kwa Mganga Majungu wa Selous atamfufua.
 
Pole sana!
Ushuhuda wa wengi umeonesha ni dawa imeponya wengi. Unaweza kumlaumu mchungaji endapo tu utaelekeza fikra kuwa Mchungaji anatibu kama uwashavyo bulb ya umeme pale nyumbani yaani unabonyeza switch na taa inawaka instantly lahasa dawa hiyo inatibu kama ilivyo dawa nyingine yaani inachukua siku kadhaa hd mgonjwa ku-recover.

My take:
upo uwezekano wa kifo hicho kuwa kimesababishwa na uchovu maradufu ambao umesababishwa na safari ndefu, huduma duni na kusubiri muda mrefu kupata matibabu.

Usielekeze lawama kwa mchungaji mtoa tiba, angalia upande mwingine pia, na huko kukamatwa unakosema kutasababisha wagonjwa wenye kuhitaji tiba watapoteze maisha kwa sababu ya kukosa tiba kutoka kwa mchungaji unayetaka akamatwe.
 
Mmmh isijekuwa ni ya kupunguza watu ila wakubwa waende kwa kujinafasi na baadae tutangaziwa hivi:-"Uchunguzi wa kimaabara umeonyesha kuwa dawa ya babu haina madhara kiafya. Aidha, utafiti wa kisayansi umeshindwa kuthibitisha kama kweli dawa hiyo ina uwezo wa kutibu magonjwa yanayosadikiwa kutibika kwa dawa hiyo. Hata hivyo, kwa kuwa suala lenyewe linahusu imani zaidi, Serikali haina kipingamizi".
Yu masti bi jiniaz.
 
Naiomba Serikali imkamate huyu Mganga wa Kienyeji kwa kusababisha vifo vingi vya Wagonjwa ktk wiki hii!! ni jana tu nimemzika Shangazi yangu aliyefariki huko Loliondo mara tu baada ya kunywa kikombe kimoja cha dawa ili kutibu gonjwa la kisukari!!! Marehemu Shangazi langu aliishi na ugonjwa huo zaidi ya miaka 20 lakini alipoambiwa kuna Mchungaji anatibu papohapo tulimpeleka Shangazi na kupewa hiyo dawa na tukiwa njiani kurudi nyumbani Shangazi aliaga dunia!!

Tunasikitika kumpoteza Shangazi wetu mpendwa na nimesikia kuna wagonjwa wengi waliofariki mara baada ya kunywa dawa za huyo Mchungaji na kunipa hofu na kukumbuka kisa cha Mchungaji mmoja huko Uganda miaka ya 90 alichoma Kanisa Moto na kuteketeza maelfu ya Waumini waliokuwa humo ndani kwa kudai alioteshwa na Mungu kuwa wakifia Kanisani kwa kujichoma moto basi wataenda mbinguni!!!

Naiomba Serikali imchukulie hatua kali huyu Mchungaji wa Loliondo kwani amesababisha madhara makubwa kwa Wananchi na hata kuharibu mazingira kwa kuwakusanya maelfu ya watu mahali finyu bila choo wala mahala pa kulala na pa kula!!

Familia yetu iko mbioni kushika wakili ili tumfungulie kesi kwa kusababisha kifo cha Shangazi wetu mpendwa!

Wananchi tuwe macho na hawa WACHUNGAJI NA MAPADRE wenye kudai kutibu maradhi baada ya kuoteshwa ndoto na Mungu wakiwa wamelala!!!!!!!!!

Hapo kwenye rangi ndo kuna kasoro: Kuna harufu ya UDINI. Nani alikulazimisha uende huko kutibiwa?? ulivutwa kwa mnyororo. Mchungaji amekuambia dawa yake inatibu kutegemea na imani ya mgonjwa-na hilo ulijua-je unajuaje shangazi yako alikuwa na imani ya dawa?? mbona mimi jirani yangu alikwenda akiwa anaumwa na yupo anajieeleza kuendelea vema!!! kwa sasa wakati uchunguzi wa kisayansi haujafanywa kuhusu ubora na uhahakika wa dawa, yeyote aendapo kutibiwa kwa dawa hiyo aende kwa imani yake na awe tayari kubeba dhamana ya mafanikio au madhara yeye mwenyewe (he/she has to take risk or responsibility him/herself).
 
Mada haina ukweli wowote bali kuna harufu ya udini. Hivi unajisikiaje kumzushia ndugu yako kafa kisa tu kueneza udini?
 
Pole sana.ila hata mahospiali makubwa duniani wagonjwa wanakufa.Haina maana kufikiri kwamba ukinywa dawa ya babu hufi.
La msingi mfanye uchunguzi wa hospitali kujua chanzo cha kifo.
 
nadhani alichojaribu kueleza kaka ni msisittizo tu hana uhusiano wa moja kw moja na mskitini anajaribu kueleza hisia zake ni jins gani amekwazwa na jambo hli,tumuelewe wana JF.
Mkuu.
Usimtete huyu ndugu..aje mwenyewe aeleze alikusudua nini au afute usemi huu. Kwa nini hakusema hekalu la wayahudi au hekalu la wahindu au kanisani?

Kumtetea wakati anaendeleza stereo typing sio vizuri.
 
Shukuru shangazi kafa maana gharama za maisha zitapungua
 
Kweli?? Patachimbika ..Wengine tumetoka Malawi ndo tuko njiani..Kama ni vyoo...Andengenye na vijana wake wapiga mabomu si waende kuchimba vyoo.....
 
Yale yale, kutoka kwa mtu yule yule, na upande ule ule!
 
Kama kweli shangazi yako kafa nampa pole. Nasema hivyo kwa sababu sina uhakika na dhamira yako.
Unachopaswa kujua ni kimba sii kila anywae dawa hupona, kwani kama ingekuwa hivyo hospitali zisingejenga vyumba vya kuhifazi maiti.
.
 
Back
Top Bottom