Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...


Hapo penye rangi sijakuelewa!!! fafanua zaidi unamaana gani?
 
Mada haina ukweli wowote bali kuna harufu ya udini. Hivi unajisikiaje kumzushia ndugu yako kafa kisa tu kueneza udini?

Yawezekana kweli kafa maana tumesikia mama mmoja wa hapa moshi kapelekwa huko na jana tu kazikwa! Inawezekana ni kweli ila hakuna aliyeambiwa eende huko. Mtu anaenda kwa hiari yake. Ni upuuzi kusema kuwa watu wapuuze wachungaji na mapadre! Ni utoto na ujinga wa hali ya juu. Kuna gazeti nimesoma kuwa ustaadhi sijui nani vile anatibu kwa kutumia gongo, bangi na kila aina ya takataka! Kwa hiyo tuwapuuze maustaadhi wote?
 


pole sana MS, familia ya mzee ngoda, jeykey. mimi sikujua kama ulikuwa loliondo
 
Wamekurupuka hao! Babu ni mjanja hii kitu ni 'Intellectual Property' yake kwa hiyo ni lazima wakubaliane kwanza. Hao wanataka kumuingiza mujini ili wai-patent kazi yake...

Bravo Babu wa Loliondo...:wink2:

Nafikiri ana haki ya kuamua kama wanaweza kuifanyia utafiti au la! Na waganga wengi wanaotoa tiba asili kama ile ya kutibu mifunjiko ya mifupa wamekuwa hawataki kushirikiana na watafiti kwa hofu ya kupoteza haki za kazi zao. Na wengine wanadai kwamba, ''...watakuambia dawa yako haifai lakini baadae watachukua na kujifanya wao ndio wamegundua''.
 
hao wametumwa wamwache huyu mtalaamu wa mitishamba aendelee kula kuku
na h uku akitoa huduma zake kwa wateja zake, ila nimekumbuka uchunguzi wa niuklia kule edeni
 

Tafadhali usinipachikie nisilosema mdomoni!!! mimi sijasema tuwapuuze Wachungaji na Mapdre wote, ila nimesema tuwapuuze tu wakija na kauli za kuoteshwa usiku na Mungu ili watibu wagonjwa! na hili linawahusu pia Mashehe wenye kutabiri mambo yanayokuja! ili kuondoa dhana yenu ya UDINI!!! imebidi nimseme na Shehe Yahya ambae kazi yake ni kutabiri bila kumsahau Askofu Kakobe na kazi yake ya kuombea wagonjwa ambao hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha wamepona!!!

Hawa Wachungaji na Mashehe hewa ndio wakuepukwa kama ukoma na nawashangaa watu wanaokuja hapa na kumtetea huyo Mchungaji wa LOLIONDO na hapa naanza kuaminini kuwa nchi yetu imeingia ktk giza tororo la imani za kichawi!!!!!!
 
Hii ni sawa, lakini kama serikali inabidi/ni muhimu ijiridhishe pia kwamba dawa hiyo licha ya kuponya kama inavyodaiwa haina madhara mengine makubwa kwa mtumiaji (sasa na baadae). serikali ina jukumu la kulinda afya na maisha ya watu wake.

Imeshindwa nini kulinda afya za wakaz wa bulyankhulu waliofoukiwa kupisha uchimbaji wa dhahabu? Huo muda si wautumie kuokoa maisha ya kina mama wajawazito wanaokosa hela za kujifungua? Hawa wamefata hiyo dawa au "pa diem"
 
Watanzania mkimfungia huyo babu, anaweza kuchukuliwa na nchi jirani, akasaidiwa mazingira mazuri, then hiyo huduma mtakuwa mnaifuata huko.

Hili ndo tatizo la kuamini vitu vinavyogunduliwa na wazungu na kudharau vya kwetu. Hebu jiulize kuna dawa ngapi za kienyeji za kichina zipo sokoni zinauzwa, tumewahi kuona mazingira wanayotengenezea?

Mi nakwambia babu kama huyu angekwepo China serikali ingemsadia kwa kumpa packaging material kama chupa ambazo ni disposable ili awe ana servia hiyo dawa badala ya kutumia kikombe kimoja, ingempa vyombo vya kuchemshia, jiko la kisasa nk, alafu huduma ingeendelea kadri anavyotaka yeye kwa imani yake.
 

Ni vizuri kuwa na mashaka lakini ni bora kuelewa kuwa katika mambo haya imani ndiyo inatakiwa kutangulizwa. Kwani imeandikwa "heri aaminiye bila kuona."
 
Kitaalamu magonjwa yote anayoyatibu babu yanatokana na vyanzo tofauti; cha ajabu inaelekea anatumia dawa ile ile ya aina moja kutibu hayo magonjwa yenye vyanzo tofauti. Hao maafisa kutoka wizarani kama wangelikuwa watu makini, walitakiwa waanze kuchunguza kama ni kweli watu wenye magonjwa tofauti wanaponyeshwa na dawa ya aina moja. Baada ya kuridhibitisha hilo, hapakuwepo haja ya kuipima hiyo dawa, kwa maana ukweli huo ungelikuwa umethibitisha ya kuwa dawa ya Babu huyo inaanzia mahali ambapo sayansi inaishia.
 
watibishe basi ili tupate nafasi nzuri ya kuanzia mgomo mama lao. Wamehisi babu ni Cdm sasa wanaanza upupu wao. Tena nawaambieni , huyo aliyempa babu nguvu ana mamlaka kulioko Wakwere wote na majuha yao.
Unaweza kutupa angalau vidokezo vichache juu ya uhusiano wa Babu na Chadema?
 

Ni kweli kabisa ndugu yangu kwani wagonjwa walioko hospitalini huwa hawafi ila wale wanaokwenda kwa Babu!
 
Mkuu tusiilaumu sana serikali,inatimiza wajibu wake.leo ile dawa ikileta madhara tutaanza kutoa lawana tena.ni vizuri kujiridhisha kuwa dawa hizo si sumu wala haina madhara yoyote. .................
 

Huu ni ukweli kabisa kwani hata ile ndoto ya Ali Juuyawatu kuhusu Tanzanite kuwa pale Mererani ni uongo mtupu. Watu walipokwenda kuchimba Tanzanite pale Mererani walikuta kuwa yale ni mawe tu na huyo Ali Juuyawatu amebakia kuwa tapeli mkubwa kwani Tanzania sasa haipati Tanzanite kutoka pale Mererani. Kumbe ndoto zote ni uongo na watu wawakatae wote wanaodai kuoteshwa mambo ya kufanya katika ndoto.
 
mungu hapendi watu wake tuteseke ndio maana kwa huruma yake amemtuma mtumishi wake ili aponye magonjwa yote yanayo mtesa binadam kwa hiyo anayeamin ataenda atapewa dawa. na asiye amin aendelee kusubir hadi hapo uchunguzi utakapo kamilika .
 
Simu yako inakosa namba moja ya mwisho.
 
watu wanywe dawa maadam ni miti ambayo ameumba mungu na hakuna maradhi yasio na dawa.kama kuna mgonjwa amepata reaction hapo lipo la kuchunguza.tena babu amekutajia mti anaotumia!
 
kumfungia babu ....halifai kwani yeye anatoa alternative medicine ......mbona kuna watabiri wanaotoa tabiri zinazotishia usalama wa nchi hawafungiwi......haya mambo ya kiasili waachiwe wananchi ..serikali isimamie usalama wao...kwa hili ingekuwa bora kwa serikali kuboresha miundombinu ili wananchi wasiteseke au wafikirie kumshauri apeleke huduma mjini kwenye huduma hasa malazi na chakula.....na kumsaidia usafiri wa kufuata dawa kijijini....angalizo ni kuwa babu sio mganga wa kienyeji!!..ni mtumishi wa mungu!!..na hatoi huduma kwa ubaguzi wa aiana yeyote!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…