Baby dady Drama: Ni ngumu sana kushindana na baba wa mtoto ukianzisha mahusiano na single maza, ngumu sana!

Ukitaka kuoa singo mama hakikisha unaliona kabuli la Baba mtoto wake la si hivyo yajayo yanaburudisha....
 
😂
 
Sitokuja niguse single mother mpaka naingia kaburini, kilichonikuta ni Siri yangu hao watu ukiwa nae kabla haujaanza Safari mchunguze vizuri kichwa chake ndio uchaguzi unasuka au unanyoa namaanisha kichwa chake sio chako
 
Sitokuja niguse single mother kamwe hao watu napita mbali nao kabisa, sitaki kabisa yaan sijui ni wote ndio wapo hivyo au baadhi Ila nahisi ni wote wapo hivyo aisee ogopa single mother hata akwambie nini kua nae makini hawakawii kugeuza kibao maana anaishi na reserve list sasa wewe jichanganye uambiwe kwani Mwanaume upo peke yako?
 
Hayo ya singo mama yalimkuta mdogo wangu mpaka tukawa tunamshangaa.

Analishwa meza moja na baba wa mtoto, tena nyumbani kwake. Kisa nini? Eti baba kamtembelea binti yake na kaenda muda wa chakula.

Nikamwambia mdogo wangu, haifai hivyo, mwambie mkeo amtayarishe mtoto baba'ke aje kumchukuwa aebde kula nae apendako, tena aishie nje, kwako asiingie kabisa, wala mlangoni asisogee.

Hilo mdogo wangu lilimshinda, eti asionekane wa kizamani. Ikabidi niingilie kati nimweleze mkewe (wifi yangu), akanielewa. Ndiyo ikawa mwisho wa kuja.

Lakini vikaanza visa vingine.
 
Tatizo lipo kwa mdogo wako kujimilikisha shamba la watu, wachaa yamkute labda atatumia kichwa cha juu kufikiri badala ya kutumia kichwa cha chini kufanya maamuzi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…